MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Wewe ni kati ya Watanzania wachache sana waliobahatika kuzaliwa katika familia ya watemi (Chief Ndatulu) na kupata privilege ya kimaisha na kielimu.
Wewe ni kati ya Watanzania wachache sana wenye uelewa mpana katika mambo ya sheria za nchini na kimataifa.
Privilege na uwezo wako kiakili ulikuwezesha kupata Shahada ya Sheria (LLB) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1972 na baada ya hapo uliajiriwa kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Serikali ilikuwezesha kwenda kusomea Shahada ya Umahiri wa Sheria kwenye Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani na kufanya kazi katika Benki ya Dunia na mashirika mengine ya kimataifa.
Mwaka 1978 ulirejea nchini na kuendelea kufanya kazi katika idara ya sheria za kiraia na za kimataifa iliyokuwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Mwaka 1988, Rais Mwinyi alikuteuwa kuwa Mwanasheria Mwandamizi wa serikali na Naibu Mwanasheria Mkuu na mwaka 1991 kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria.
Mwaka 1993 uliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali ambapo ulitumikia nafasi hiyo hadi Desemba mwaka 2005.
Mwaka 2005, Wananchi wa Jimbo la Bariadi Magharibi walikuchagua kuwa Mwakilishi wao Bungeni hadi leo anaendelea kuishikilia nafasi hiyo ambayo ilikufanya kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Miundombinu.
Uelewa wako mkubwa katika utumishi serikalini na kimataifa umekuwa ukiutumia kinyume na malengo ya taifa ambalo limetumia raslimali kubwa kukusomesha ndani na nje ya nchi.
Uchafu ambao Rais Magufuli anajitahidi kuusafisha serikalini unaufahamu kwa sababu wewe ni kati ya wale walioweka misingi ya kisheria na kiutendaji iliyokaribisha uchafu nchini.
Ninafahamu kwa sasa wewe ni tajiri wa ''vijisenti'' katika kundi la Mabilionea nchini na hata kama ukiamua leo kuacha kufanya kazi, standard yako kimaisha itaendelea kuwa ile ile.
Kwa jinsi ulivyo na uelewa wa sheria na uendeshaji wa serikali, hata jipu lako haliwezi kutumbuliwa kisheria. You are too smart and slick to fall into the hands of State and International law enforcement agencies.
Tumia kwa sasa uelewa na uzoefu wako katika kulisaidia taifa kama wataalam wa computer hacking wa nchi za Magharibi wanavyozisaidia nchi zao kupambana na kikundi cha kigaidi kinachojiita ISIS katika intaneti na mitandao ya kijamii wakati theoretically hao wataalam wanatakiwa kukamatwa na kufunguliwa mashitaka.
Serikali pia ijishushe chini na itumie uelewa na uzoefu wako kama plea bargain ili uweze kuisaidia kisheria kupitia Bunge ili kuziba mianya ya rushwa na ufisadi. Siyo kosa kwa Serikali kutumia fire to fight fire in other word, a serial criminal to fight crime!
Wewe kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bunge, it's high time, tumia nafasi hiyo kwa manufaa ya Taifa.