Anayekupenda hawezi kukuliza

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,348
1,805
Hakuna maumivu makali duniani kama kuachwa na mpenzi wako au Mume/Mke wako unayempenda kwa moyo wako wote na akili zako zote na hasa akiwa ndio hazina na faraja ya maisha yako.Maumivu ya mapenzi ni makali sana na huacha kovu la maumivu kwa muda mrefu sana .

Ukiachwa una haki ya kuumia na kulia kwa uchungu na kutoa machozi utakavyo sababu machozi ndio njia pekee itoayo huzuni ya mwanadamu ,mwanaume/mwanamke anayekupenda kwa dhati hawezi kukuliza kwa uchungu na badala yake alitakiwa kukupa machozi ya furaha daima.

Ukiachwa kama una haki na mapenzi ya dhati kwa mpenzi wako au mke/mume wako aliyekuacha huna budi kumshukuru Mungu kwa kukuonyesha ya kuwa mtu uliyekuwa naye hakuwa mtu sahihi kwako na ndio maana amekuacha na simanzi na upweke badala ya kukupa faraja na amani.

Raha ya penzi ni furaha na amani muda wote ijapokuwa tofauti huwa zipo sana na changamoto kubwa huwa hutokea sana ,kitu cha msingi ni wahusika kukaa pamoja na kujadili kwa kina mapungufu yenu na tofauti zenu ili kuweza kutunza na kudumisha upendo wenu.

Siku hizi ndoa nyingi na mauhusiano mengi yamepoa sababu ya ukosefu wa asset muhimu ya mapenzi ambayo ni uvumilivu, uaminifu na pesa ,vimeharibu ndoa nyingi sana na mauhusiano mengi sana,inahitajika hekima na busara sana pale mtu unapoachwa unatakiwa kufanya yafuatayo.........

Itaendelea jumamosi
Don’t trust too much, don’t love too much, don’t care too much because that ‘too much’ will hurt you so much!
GedsellianTz
 
asikuambie mtu hakuna maumivu makali na yasiyofichika kama account zote tigo pesa,m pesa, airtel money, NMB,CRDB kusema huna salio la kungalia salio acha kabisa
 
Kuachwa kupo na ukipata fursa hiyo lia lia lia uwezavyo Ila hakikisha ukimaliza kulia hutarudia kulia kwa mtu huyo huyo tena....
 
Back
Top Bottom