Anayedaiwa kupigwa na mumewe baa afariki dunia

Anayedaiwa kupigwa na mumewe baa afariki dunia

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713


ajichomamoto_300_183.jpg


MWANAMKE Sakina Kopa (41) amefariki dunia siku tatu baada ya kupigwa na kujeruhiwa na mumewe anayedaiwa kuchukizwa kwa kumkuta akiwa baa usiku. Aidha, katika tukio jingine linalohusishwa na wivu, dereva wa bodaboda amemjeruhi kwa visu mpenzi wake ambaye ni Mwalimu, na baada ya kudhani amemuua, naye alijichoma kisu hadi utumbo kutoka nje, ingawa bado yu hai.


Matukio hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Leonard Paul. Tukio la kwanza lilitokea Oktoba 22, mwaka huu saa 4 usiku katika maeneo ya baa ya Mafiga, Manispaa ya Morogoro, likimhusisha Sakina na mumewe.

Kamanda Paul alisema mwanamke huyo alifariki dunia akiwa katika Hospitali ya Mkoa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kufuatia kipigo kutoka kwa mumewe, Hamisi Yohana baada ya kukutwa akiwa katika baa hiyo.

Alisema baada ya mwanamume huyo kumkuta mkewe akiwa baa, alimpiga na kumjeruhi vibaya katika maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo tumboni na usoni, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, Oktoba 25, mwaka huu mwanamke huyo alifariki dunia akiwa hospitali na mtuhumiwa amekamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamni mara uchunguzi utakapokamilika.

Katika tukio la pili lililotokea Oktoba 27, mwaka huu saa 1:30 asubuhi katika Mtaa wa Mkwajuni, Kamanda Paul alisema linamhusisha mwendesha bodaboda, Raphael Bernard (33) mkazi wa Kichangani na Rosemary Mkoba (33), Mwalimu wa Shule ya Msingi Mafisa, mjini Morogoro.

Alisema siku ya tukio, Bernard alikwenda nyumbani kwa mpenzi wake Rosemary kumhoji sababu za kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yao, hali iliyozusha ugomvi baina yao na hivyo kuanza kumchoma kisu mwalimu huyo katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwa ni pamoja na mikononi, tumboni na kichwani.

Aliongeza kuwa, kutokana na kelele za kuomba msaada za mwalimu huyo, watu walianza kukusanyika kwa lengo la kutoa msaada na Bernard alipoona mwenzake anazidiwa, aliamini amemuua hivyo alichukua uamuzi wa kujifungia ndani na kujichoma kisu tumboni hali iliyosababisha utumbo kutoka nje.

Alisema majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wakipatiwa matibabu na kwamba hali zao si nzuri.

Chanzo: Habari leo
 
jamani tunajitoa akili kweli kweli mahaba yenyewe hatuyawezi duh
 


ajichomamoto_300_183.jpg


mwanamke sakina kopa (41) amefariki dunia siku tatu baada ya kupigwa na kujeruhiwa na mumewe anayedaiwa kuchukizwa kwa kumkuta akiwa baa usiku. Aidha, katika tukio jingine linalohusishwa na wivu, dereva wa bodaboda amemjeruhi kwa visu mpenzi wake ambaye ni mwalimu, na baada ya kudhani amemuua, naye alijichoma kisu hadi utumbo kutoka nje, ingawa bado yu hai.


matukio hayo yamethibitishwa na kamanda wa polisi mkoani hapa, leonard paul. Tukio la kwanza lilitokea oktoba 22, mwaka huu saa 4 usiku katika maeneo ya baa ya mafiga, manispaa ya morogoro, likimhusisha sakina na mumewe.

kamanda paul alisema mwanamke huyo alifariki dunia akiwa katika hospitali ya mkoa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kufuatia kipigo kutoka kwa mumewe, hamisi yohana baada ya kukutwa akiwa katika baa hiyo.

alisema baada ya mwanamume huyo kumkuta mkewe akiwa baa, alimpiga na kumjeruhi vibaya katika maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo tumboni na usoni, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini.

kwa mujibu wa kamanda huyo, oktoba 25, mwaka huu mwanamke huyo alifariki dunia akiwa hospitali na mtuhumiwa amekamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamni mara uchunguzi utakapokamilika.

katika tukio la pili lililotokea oktoba 27, mwaka huu saa 1:30 asubuhi katika mtaa wa mkwajuni, kamanda paul alisema linamhusisha mwendesha bodaboda, raphael bernard (33) mkazi wa kichangani na rosemary mkoba (33), mwalimu wa shule ya msingi mafisa, mjini morogoro.

alisema siku ya tukio, bernard alikwenda nyumbani kwa mpenzi wake rosemary kumhoji sababu za kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yao, hali iliyozusha ugomvi baina yao na hivyo kuanza kumchoma kisu mwalimu huyo katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwa ni pamoja na mikononi, tumboni na kichwani.

aliongeza kuwa, kutokana na kelele za kuomba msaada za mwalimu huyo, watu walianza kukusanyika kwa lengo la kutoa msaada na bernard alipoona mwenzake anazidiwa, aliamini amemuua hivyo alichukua uamuzi wa kujifungia ndani na kujichoma kisu tumboni hali iliyosababisha utumbo kutoka nje.

alisema majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa wakipatiwa matibabu na kwamba hali zao si nzuri.

chanzo: Habari leo

salaam kwenu wana jamii,

kwa kifupi sana,uanaume ni pamoja na ustahimilivu wa hali ya juu,hawa wake zetu ni watu dhaifu mno.
Ndo maana imeandikwa tuishi nao kwa akili.

Nazungumza haya kwa sababu jana usiku sikulala kwa ajili ya ugomvi uliotea kwa jirani yangu.

Kisa ati jamaa hajapelekewa maji bafuni daah,kamgarazaga mkewe kiasi cha kumvujisha damu za kutosha na wakati huo mkewe alikuwa jikoni anaandaa riziki ya usiku,zingatia mkewe si mama wa nyumbani nae katoka job vile vile,hatuelewi alimchana na kitu gani kiasi cha kumvujisha damu nyingi kivile na jamaa alikuwa hajalewa labda kuna jambo lingine ndani yake.

Mayowe na vilio vya house girl wao,mwanae wa vidudu(nursery school) pamoja na mwanae mdogo kichanga cha mizezi kadhaa ndio vilitushtua lakini sikutaka kwenda huko,mpaka pale mlinzi alipokuja kutujuza kwamba jamaa anauwa mkewe,ikabidi tuelekee kwenda kumnusuru mama huyu.

Kufika pale jamaa anaanza kutuomba msamaha sisi na kututaka kusaidia kwenda polisi kuchukua pf3 ati kaanguka na pikipiki.(kauli hii kichanga kwa jirani kililia usiku kucha).very sad.

Jamaa walielekea huko pamoja na majirani mpaka alfajiri naondoka hakuna yeyote aliyerudi.

Wanaume tusiwapige hawa viumbe ni dhaifu mno.


i told you people before...
Unabii unazidi kutimia.....
 
Historia inaonyesha wanawake wanaopigwa ni wale wenye "midomo".

Huyo uyo ipigaji kwako ndo asali kwa mwingne
 
i told you people before...
Unabii unazidi kutimia.....

Nashukuru Mungu Kanipatia kamzungu kangu. Kila kazi tunasaidana tukitoka job yeye anasaidia kids with home work mie jikoni. Yeye anaosha dishes mie naogesha watoto,Wanaume was kibongo nourma Sana. Pole Dada.
 
Nashukuru Mungu Kanipatia kamzungu kangu. Kila kazi tunasaidana tukitoka job yeye anasaidia kids with home work mie jikoni. Yeye anaosha dishes mie naogesha watoto,Wanaume was kibongo nourma Sana. Pole Dada.

Hako kamzungu umekatuliza kwa kukapa 0713....! Mbona wanaume Wa ki-Tz wenye kuelewa na kujua kupenda mbona tuko wengi tu! Vijana Wa leo ndio Shida!!
 
Nashukuru Mungu Kanipatia kamzungu kangu. Kila kazi tunasaidana tukitoka job yeye anasaidia kids with home work mie jikoni. Yeye anaosha dishes mie naogesha watoto,Wanaume was kibongo nourma Sana. Pole Dada.

Kuna mamilioni ya wazungu ambao ni wababaishaji tu
 
Back
Top Bottom