Ana uthubutu ila amekosa uwezo wa kufikiri, ubunifu na umakini

MGANGA MCHAWI

Senior Member
Oct 15, 2015
199
393
Kila mtu ana uwezo mkubwa wa kufikiri na akili nyingi kabla hajaongea chochote.Na thamani ya mtu itapanda au kupungua pale atakapoongea au kufanya kitu.

Ili uweze kufanikiwa katika kitu chochote ni lazima uwe na uwezo wa kufikiri, ubunifu, umakini na UTHUBUTU.Ukiwa na uwezo wa kufikiri,ubunifu na umakini ila ukakosa UTHUBUTU basi uwezekano wa kufanikiwa utakua mdogo sana au unaweza usifanikiwe kabisa maana utakua muoga wa kutekeleza ubunifu wako.Vivyo hivyo kama utakua na UTHUBUTU na ukakosa uwezo wa kufikiri, ubunifu na umakini kwa kuwa utakua unafanya vitu bila kuvijua kiundani.

Utofauti kati ya mwerevu na Mjinga ni kwamba mwerevu anafanya vitu baada ya kuvifikiria na Mjinga anafikiria vitu baada ya kuvifanya.

Mikakati yoyote inayofanikiwa ni ile iliyoanzwa kutekelezwa kichwani na kuwekwa mezani kabla ya kuitelekeza eneo la tukio.

Mh. Makonda ana UTHUBUTU ila amekosa uwezo wa kufikiri, ubunifu na umakini.Anatumia nguvu nyingi kufanya kitu sahihi kwa kutumia mbinu mbovu na zisizotekelezeka.Mtu kama huyu hafai kuwa kwenye maamuzi.

Ni mtu mwenye mawazo mazuri ila anakosa mbinu za utekelezaji mwishoni anatumia mbinu za kijinga ambazo baadae anajkuta hakuna alichofanya.Ujinga zaidi ni pale anaposhindwa kujua nini maana ya kuwa kiongozi.

Kuna muda huwa najiuliza nini hasa lengo lake la hizi harakati?Ana lengo kweli la dhati au anafanya ili aonekane anafanya?

Washauri wana mshauri hivi au yeye ndio anawashauri washauri wake?Hii nchi haiwezi kuendelea kama tutaendelea kuwa na viongozi kama hawa.Viongozi kama hawa hawapaswi kuitwa viongozi.Huwezi kuwa kiongozi kama hujui nini maana ya kiongozi.

Sio lazima kiongozi awe na Shahada ya uchumi ili kuinua uchumi na wala sio lazima kiongozi awe Mhandisi wa viwanda ili aweze kutekeleza ahadi ya Nchi ya Viwanda.

Sitaki kuamini Makonda amekosa watu wenye uwezo wa kutekeleza malengo yake mazuri kwa sababu kwa wadhifa wake ana wataalamu wa kila kitu wamemznguka na walio tayari kufanya kile atakachowaambia.Kwa hiki anachokifanya inajidhihirisha hajui hata nini maana ya kuwa kiongozi.

Ni wakati sasa wa Makonda na viongozi wote wa aina hii kupumzshwa kwa faida zake na faida ya nchi kwa ujumla.

HUWEZI KUTUMIA KIFARU KUWINDA SUNGURA NI UPUUUZI.
 
mambo anayofanya MAKONDA madhara yatokea baada ya miaka miwili. hawa hawa ccm wanaomvimbisha kichwa ndo hao hao watampiga vijembe.
 
Kwani kuna baya gani amefanya,kukarabati magari ya polisi hivi ni kokukosea? mkuu mtoa mada hebu tupe mifano michache ya makosa ya huyu kamanda mchapa kazi.
 
Nimesoma,nimekulewa sasa napita ila ntarudi kuja kusoma michango ya wenzangu.
 
Back
Top Bottom