Amuua mama yake mzazi na kumzika chini ya kitanda

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,258
Ama kweli hizi sasa ndizo zile nyakati za mwisho wa dunia zilizotabiriwa na manabii!

Polisi huko nchini Kenya, wanamshikilia kijana mmoja, kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi na kisha kumzika chini ya kitanda!!

Akisimulia mkasa huo wa kuhudhunisha, mmoja wa majirani wa marehemu, anasema walishangaa kutomuona mama huyo baada ya nyumba yake kushika moto! Wengi waliamini kuwa huenda aliungua ndani ya nyumba hiyo.

Lakini cha kushangaza, ni kutopatikana kabisa kwa mwili wa mama huyo. Katika pekua pekua zao, ndipo ghafla wakaligundua 'kaburi' la mama huyo chini ya kitanda chake kilichoungua.

Ndipo wakatoa taarifa polisi ambao nao baada ya uchunguzi, walifanikiwa kumtia mbaroni mwanae mama huyo ambaye alikiri kufanya unyama huo.

Mtuhumiwa anasema alifika kwa mama yake mzazi, akiwa amelewa sana na akajiona ghafla 'anaota' anapambana na majambazi, ambayo katika kujihami, alichukua mchi na kumtwanga mama yake mzazi alyefariki papo hapo! Kisha auchukua mwili huo na kuuzika chini ya kitanda, kabla ya kuitia kibiriti nyumba hiyo!
 
Duuh..kuna yule aliyedandia ndege akasema alikuwa amelewa akadhani ni matatu....Kenya ina mambo
!!!
 
Inasikitisha sana,wala huyu mtuhumiwa inaonyesha wazi hakuwa amelewa,hakuna mlevi mwenye nguvu ya kuuwa na kuzika mwenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Back
Top Bottom