Amka Mtanzania Mwenzangu!

Amka Mtanzania Mwenzangu!

Mwaipungu

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
293
Reaction score
138
Kwani hili taifa ni la CCM ama Watanzania?

Takribani miaka 50 mambo ni yale yale hakuna mabadiliko, hivi vichwa tulivyopewa na mungu havina akili ama ni ujinga wakulazimisha? Mtawala na mtawaliwa na bosi?

Ukiweza kujibu haya mswali kiufasaha basi ukombozi wako na wangu ndio umefika. Sioni cha kujivunia hata Amani inayosemwa na watawala sikwl mana Watanzania tunavumilia tu mana taifa letu kwanza, lakini ukitaka kujua kua kila kiumbe kinakikomo chake cha uvumilivu basi mwaka huu ndio kitajulikana. Taifa lenye watu makini na wasomi mtakubaliana na mm kua serekali inayo ongoza kwa propaganda ni serekali iliyo shindwa kuangalia mambo kwa upana na ni serekali lege lege. Taifa hili ni taifa gani kama wasomi wetu akili zao zipo kwenye makaratasi? Sisi hatuwezi kua watumwa wa watu wachache naikifika hatua kama hii basi kiukwl nchi yetu ipo kwenye hatari ambayo itazaa ukabila, udini na nakadhalika.

Naomba niulize hivi CCM imesema ilifanya mapinduzi ni mapinduzi gani wasomi nisaidieni mana mm kwa elimu yangu ni kwamba baada Tanganyika kua tayari kujiendesha ndipo alipewa Nyerere kama Prime minister in 1960's nataka kujua hawa CCM wanasema walifanya mapinduzi ni yapi?

Kama vita vya kumuondoa mkoloni vilifanywa na chiefdoms kama Mkwawa, Mtemi Mirambo na vyengine vya Kinjekitile na Abushiri kwa Zanzibar. Kwa mtazamo wangu kama CCM ilifanya mapinduzi basi si Tanzania bali ni nje ya Tanzania. Tuache ushabiki wakijinga. Wagombea wanasema "Tanzania yangu itakua ya viwanda" sasa hapa anatatua matatizo ama anaongeza matatizo?

Mgombea wengine alisema elimu mana ukiwa na elimu basi ww utakua na maarifa yakujenga na kugundua mashine ambazo zitakua zikitumika viwandani bali viwanda bila elimu ni utumwa mamboleo. Amka mtanzania wenzangu! Na kuikosoa serekali yetu ndio kuiongezea maarifa na kufanya akili zao kufanya kazi vizuri lakini kwa sasa naomba tufike mahali tuseme basi inatosha ili tuangalie wapi pana afadhali, acha uwoga na ufanye mabadiliko ya kwl. Mungu hajaweka limit yoyote kwa mwandamu kwa nini wanadamu atuekee limit dhidi ya maisha yetu?

TAFAKARI NA UFANYE MAAMUZI YA KWELI.
 
Nasema hata NYANI afadhali tumjaribu safari hii. Mara nyingi watu waogopa kitu kigeni lakini mara nyingi hicho ndicho kinachoendeleza. Kama watu walibakia na vitu vile vile walivyozoea, hadi leo tusingekuwa na gari, televisheni, nguo za pamba nk. Mabadiliko hata yakiwa mabaya ni mazuri. At least yanakufunza. Kuzorota kwa Tanzania ni kwa sababu: miaka 25 mtu yule yule, miaka 54 Chama, viongozi wale wale.
 
Hiyo amani isemwayo ni uongo. Watu huteseka mno Tanzania kwa kukosa haki na sheria hata kuliko Zambia, Malawi, Zimbabwe, Botswana, Senegal, Cameroon......nchi zote hizo hazikuingia vitani, si kwamba Tanzania imefanya mwujiza mkubwaaaaa.
 
Mambo mengi yamefanyika katika nchi hii labda mikmbizi ndio hawezi kujua yale yanayojiri na mafanikio yaliyopatikana
 
Mbona kwenye mikutano yenu hamtuambii mnazidi kutuboa na Lowasa kafanya hili, Lowasa yuko vile hivi Lowasa ndiye ilani yenu au ndie taarifa ya utekelezaji wa ilani zeni za mwaka 2005-2010? remember information is power.
 
Mimi aliposema kodi yangu itatoka 18% kwenda 9% alinishawishi...sijui nyie wafanyakazi wengine wa serikali mlijisikiaje??!

Halafu ni jambo ambalo kwa elimu kidogo CCM iliyotusaidia kuipata unaona linawezekana kabisa!

Anyway itafahamika tu...ngoja tusubiri hadi 25/10/2015...
 
Mbona kwenye mikutano yenu hamtuambii mnazidi kutuboa na Lowasa kafanya hili, Lowasa yuko vile hivi Lowasa ndiye ilani yenu au ndie taarifa ya utekelezaji wa ilani zeni za mwaka 2005-2010? remember information is power.

Sorry kwa kuwa mwanasiasa kwa leo...ila kama wale waliokuwa pale ferry jana..WALINIBOAAAAAAAAAA

point pekee niliyoisikia jana ni;

Mwaka 2006 kulikuwa na shule 7 tu za sekondari.

Sasa hivi Kikwete anaondoka kuna shule 30 za sekondari mkoa wa Ilala peke yake.

Kwa bahati mbaya naye aliiharibu hoja yake pale alipotaka kutukumbusha kuwa wakati huo huo (2006) ni wakati Mheshimiwa Sumaye alipoacha kuwa waziri mkuu.

Sikuona umuhimu wa hoja hiyo kabisa maana nilijiuliza je, wakati anaingia madarakani Sumaye zilikuwa ngapi? zilikuwa katika hali gani? je hizo 30 zinaweza kuwekwa na kusifiwa kuwa ni katika shule bora za sekondari au ni majengo 30 yanayoongelewa?

Chama tawala lazima kisimame na kujitambua kama chama tawala...MWAGA FACTS (Umefanya NINI na Utafanya NINI) acha wananchi waamue wenyewe.

In my view, wananchi wanatiwa zaidi hasira na chuki dhidi yake wanapohubiri kukosa amani au kuwaambia polisi ni wabaya au kuwatukana wagombea wengine badala ya kutuambia wamefanya nini kwa miaka 50 waliyoko madarakani.

Yani we jamaa uliyekuwa unaongea jana mida ya 5:15 - 5:40pm uliniboa sana. Unahisi wale askari waliokuwa wanasimamia ulinzi kwenye kampeni yenu walijisikiaje? Wale mapolisi wa kile kituo kidogo pale feryy walijisikiaje? Eti, "Msiwaone hao polisi ni wabaya kweli..watawapigeni na mabomu ya moshi tena siku hizi ni ya maji ya kuwasha ukipulizwa ukajikuna unawashwa na kuvimba mwili mzima... "

Je, ni kweli mapolisi ni wabaya hivyo? Kama ndivyo mmewachukulia hatua gani maana sote tunajua kazi yao sio kuwa wabaya kwa wananchi ni kuwatumikia..kuhakikisha ulinzi wa mali zao na wao wenyewe!

Halafu mkamaliza mkutano wenu saa 6:10pm wanawaangalia tu wala hamkupigwa hata kirungu...bado unahubiri mapolisi ni wabaya!
 
Kwa kwl hii hoja ya polisi kuwa wabaya ni sawa kabisa kaka mana hebu naomba nikukumbushe kidogo maandamano ya watu Arusha watu walipigwa kama siyo wandamu na kidongo chekundu awamu ya Benjamin Mkapa watu waliuwawa na wengine kujeruiwa. Hivi hii ni haki kwa kwl. Wapi haki ya wanadamu. Hivi sisi ni watumwa ama wazawa wa Tanzania?
Watu wakiandamana kwani wanaandamana kwa nini tuache ushabiki kua wanalinda amani, mana amani ilishatoeka miaka mingi sana hivi sasa tunavumilia tu lakini ipo siku watu watachoka kuvumilia na kisha ndipo tutaingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Sasa basi kama watawala wataendelea kufanya wanachofanya basi mark my words we have less than 20 years to head to a civil war. Kumbuka every man has a limit.
 
Hukuelewa point yangu! hata hivyo...
 
tulishaamka sasaivi tunapiga mswaki na kunawa uso halafu tunanowa kikatio kwa ajili ya kuchinja maana hamna namna nyingine
 
Back
Top Bottom