Amka kijana, ulimwengu unajongea...

Amka kijana, ulimwengu unajongea...

scope17

Member
Joined
Mar 7, 2017
Posts
35
Reaction score
47
Habari wana jukwaa..!
Kama kichwa kinavo jieleza, nimeamua kuandika Uzi huu mahsusi kwaajili ya vijana wenzangu nikiamin vijana ni nyezo ya muhim Sana katika ujenzi wa taifa..
Vijana ni nguvu kazi, ni mtaji lakini pia ni raw material katika masula yote katika taifa..

Kundi hili kimsingi Lina watu wengi,ukiangilia vyuoni na hata makazini nowadays vijana ni wengi kwelkwel hivyo hakuna njia ya kuliepuka kundi hili..
Kwa kuanza, maudhui ya Uzi huu ni kujarib kutafuta njia ya kuwekeza katika kundi Hili lengo likiwa ni kutengeneza taifa lenye vijana smart wenye postive thinking lakin pia vijana wenye uwezo wa kucreat positive ideas katika suala Zima la kujiletea maendeleo binafsi na Jamii pia.

Kuna siku nilikuwa napiga soga na Mzee mmoja ambaye kwa sasa ni mstaafu, sikumbuki tulianzaje lakini mada ilikuwa ni kwamba kwann wazee weng wanapoataafu hupewa nafasi za kuongoza mambo flani flani katika sector za umma ikiwa umri wao umefikia muda wa kupumzika..!
Kitu alichoniambia yule mzee ni kwamba vijana wa siku hizi hawako smart, hivyo inakuwa ngumu kuaminiwa na kukabidhiwa majukumu..! Nilinot point hyo pemben na kuamua kuitafakari

Pia alichosema kingine ni kwamba, vijana wapo wengi Sana mtaani wanalia hakuna ajira ikiwa wamemaliza vyuo na vyeti safi lakini kinachowapungukia ni skills za kuendana na soko la ajira..!
"Kuna vijana wengi pia makazini lakin ni asilimia chache Kati Yao wanaokidhi matakwa ya waajiri Wao" alisema mzee huyo.

Baada ya kutafakari kiundani suala hili niligundua kuwa maneno ya yule mzee Yana ukwel mtupu, hivyo nikaamua kuangalia jinsi gani naweza kuja na njia ya kujaribu kupunguza tatizo hilo,
Lakin pia tunaweza angalia njia ya kuwawezesha vijana hawa kuwa na uwezo wa kucreat ideas ikiwa ni moja ya nguzo muhim Sana katika kufanikisha movement yoyote mahali penye ushindani (creativity), ili kuwa tofauti.

Niwakumbushe kitu kimoja muhimu Sana "Kila mafanikio yanayoonekana katika uso wa dunia yalianza na wazo" (idea)
So hapa tunaweza kufanya iwekezaji na tukaibadili system iliyopo..
Mfano. Currently kna michezo ya kubahatisha mingi Sana inayoendelea hapa nchini ambayo kimsingi inafaida kubwa Sana katika Jamii husika, hii ilianza na idea kabla ya kuwa kweli..
Pia Kuna campaign nyng Sana zenye matokeo chanya zinazoendeshwa na media mbalimbali hapa nchini, nazo hazikuanza kwa kufanikiwa Bali wazo Kama imagination..!

Point yang hapo ni kwamba, tunaweza fanya innovation za maana Sana Kama tutaitambua thamani ya kuwekeza katika ideas.
Nilichofikiria kufanya ni hiki hapa,
nitengeneze platform moja matata yenye lengo la kuwafua vijana katika mambo ya msingi Sana ambayo hawawezi kufundishwa vyuoni wanapokuwa wakifanya masomo ya taaluma zao.
Lengo ni kuwafanya hawa vijana wawe aware kuhusu dunia halis nje ya vyeti walivyo navyo au wanavyo tarajia kuvipata baada ya kuhitimu vyuoni.Tujue ni jinsi gani tunaweza kumove na ulimwengu wa sasa Kama vijana..hiki
Kitakuwa ni kiwanda cha kuchakata vijana wenye positive mind kiasi kwamba kila mwajiri afurahi kupata product ya kiwanda hiki cha aina yake..! hapo tutaweza kutatua matatizo aliyoyesema mzee yule..

Napenda kuwasirisha mada hii ili nipate mawazo na ushauri kuhsu jins gan lengo hili linaweza fanikiwa..!
Ahsanteni.
 
Hujalijua taifa hili. Hujawajua wafanya maamuzi wa taifa hili
 
Hapa Tz na Africa wazo lako aliwezi kupewa nguvu ...tatizo awo tunaowaita wazee ni selfish sana ...unakuta mzee ...ataki kustaafu au akistaafu anampigia promo mtoto wake ili na yeye aonje keki ya Taifa...The way cha muhimu nikuwaacha tu watu waishi maisha wanayotaka ilimradi awavunji sheria.

Maana hii Dunia sote tunapita ...tu ..ukiweza pata hela yakula...inatosha tu...ukiwaza Ndoto kubwa ..utakuja kufa kibudu.
 
Wazo zuri sana. Vijana tulio wengi tunapenda mafanikio lakini hatupendi kazi. Tunaamini kuwa maisha ni simple sana hasa tunapotazama wale waliokwisha ku struggle na kufanikiwa.

Masikio yetu yabapenda kusikia mafanikio tu lakini hayapendi kusikia mtiririko mzima wa jinsi mafanikio yanyoanza taratibu kwa mipango madhubuti.
Kukushauri tu katika wazo lako, sijui umrjipangaje lakini yote yanawezekana, kiwanda chako cha kufua watu unapaswa kuandaa mitaala na seminar zenye tija kwa vijana, hakikisha elimu utakayowapatia iwe ni elimu mkombozi yenye poaitve impact isiofanana kabsa na ile ya kupata yeti tu na kusubiri matamko ya serikali.
God Bless You
 
Back
Top Bottom