amekata tamaa anaitaji ushauri

happy amos

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
251
Reaction score
434
Anaomba ushauri , iko hivi

Ni bint wa miaka 27 hajaolewa kutoka na mazingira ya kijijin kwao mama yake ikawa inamuuma sana bint yake kwanini haolewi japo bint alikua haishi nyumban hapo alikua anajitafutia maisha, siku moja kaenda kusalimia nyumban kakuta mama yake kajadiliana na shoga yake wakamtafutia mchumba huyo jamaa ni doctor nae alimwambia shoga yake mama yake amtafutie bint hapo kijijin wa kuoa, bint kaja kawekwa chini hakuna ubishi unatakiwa ukaonane na kijana kama mtapendana na kukubaliana muoane, kwa bahati nzuri wakapendana na wakakubaliana kuoana.
Haukupita hata mwezi kijana kampeleka bint kwao kamtambulisha na kamvisha pete mbele ya kanisa mwezi uliofuata bint kampeleka kwao na wazazi wa mwanaume wa kaenda kupanga na kutoa mahari nusu.

Kasheshe inaanza
Mipangi ikawa mwez wa tano ndoa wakaanza kubanjuana bint akapata ujauzito kamwambia jamaa kasema inabidi tufanye haraka mipango ya harusi ikashindikana kutokana na kukosa pesa kwa haraka jamaa akamshauri bint aitoe mimba ili mipango yao iende sawa bint kagoma kutoa visa vikaanza kila siku migogoro familia zote wanajua na wakashuri bint ajifungue kwanza ndo mambo ya ndoa badae...
jamaa kapanda bei bint akimpigia kumwambia anaumwa anamjibu kunya, bint hana uwezo wowote kwa sasa yupo nyumbani nako hawana uwezo kijana hata cm hapigi, bint analia tu nashindwa hata nimsaidiaje nyumban hali ngum ya kimaumisha afanyeje?
Ujauzito unamiezi 6 sasa. Mshaurini jaman anatia huruma
 
Amefanya la maana sana kupinga kutoa ujauzito na aendelee na msimamo wake hata hali iwe ngumu vipi asicholopoe.

Wewe cha kufanya kama itawezekana mpe tafu kipindi hiki chote cha ujauzito hadi atakapojifungua
 
mmh maskin haya mambo haya unaweza kudhani umepata kumbe umepatikana.....

wazazi wa huyo kijana washirikishwe na wao maybe waongee na huyo kijana.labda yaweza saidia
 
Mmmh! Mwambie avumilie mimba si ugonjwa as long as haimsumbui.
 
maskini inasikitisha
asikate tamaa aendelee kumtumainia Mungu
yote ni mapito ili utukufu wa Mungu upate kudhihirika
 
Waongee na mama sindo alimconnect wamwite kijana wamuulize kulikon
 
Hii mbona inajichanganya? Isomeni vizuri
 
Eti nyumbani kwao hali ngumu! Hii mambo ya kudekea hela za wenzio haifai kabisa. Mama yake binti amemzaa na kumlea katika umaskini huo huo. Amnyamazie kimya huyo daktari, halafu ajishughulishe hata na kilimo hapo kwao (yes, akimuuliza mama yake aliileaje mimba yake atagundua ndo hayo hayo).

maisha lazma yaendelee, kujiliza hakutatui shida!
 

Ushauri mzuri sana lakin kwa sasa sio mda wa kilimo mpaka mwezi wa 11 au 12 ndo masika inaanza
 
Anaweza kumudu kuilea hio mimba na huyo docta uchwara aachane nae,daktari gani anamwambia mtu atoe mimba yake angali washachumbiana....Na asiegmee shida,kwasababu kila mtu shida anazo zake....
 
eti akimpigia simu anamjibu kunya, ndo aje?

 

Umejuaje mkuu nilitaka niulize huyo mama aliwezaje kumlea mwanae mpaka akawa binti mkubwa pamoja na umasikini wao..ndo ampe njia binti yake za kupambana na hiyo changamoto.,
 
Kwanza amshukuru sana Mungu kwa kumuonesha huyo Daktari ni mtu wa namna gani mapema kabla hajaingia kwenye ndoa.
Umesema bint alikuwa akijishughulisha kutafuta maisha,kwa nini asiendelee? Kama mimba haimsumbui aendelee na shughuli zake ila kama haiwezekani tena basi mama amsaidie mpaka ajifungue ajishughulishe kulea mwanawe maana hamna ndoa tena hapo!!
Natamani wasichana wote wangejua uchumba si ndoa,wakiamua kukubali kufanya ngono na wachumba basi umakini uwepo!!!
 
Pole yake. Ni matokeo ya kuwa desparate.

Alee mimba na atafute vibiashara vya kufanya maisha yasonge.

Walipima ngoma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…