Baada tu ya kifo cha Baba wa Taifa, rushwa ikageuka kuwa ni halali ndani ya chama tawala. Kuna wakati ilifikia kiwango na kuipa jina la "takrima". Kwa sasa inafumbiwa macho kwa kundi fulani la wateule wachache wenye kukubalika mbele ya macho ya Mwenyekiti, ambao hata wakionekana wakijipitisha majimboni na kugawa rushwa kwa uwazi hakuna wa kuwagusa.
Hawa ambao unasikia wanakamatwa na TAKUKURU ni "rejects" ambao wapo ktk orodha ya kukatwa majina yao, hata kama wataongoza ktk kura za maoni. Ebu fikiria mtu kama Polepole ambaye ndiye mwenye kushikilia fungu la kufanya "bargaining & purchasing" kwa njia ya ghiliba ili kuweza kuwanasa waunga juhudi, huyu pia ndiye eti mwenye kuhubiri kuwa anaichukia rushwa.
Rushwa na CCM ni kama maisha ya samaki ndani ya maji. Ustawi wa chama hiki na mchakato wa upangaji wa safu yake ya viongozi toka taifa mpaka matawini kwa sehemu kubwa hutegemea rushwa ya fedha, ngono zembe, uzinzi, upendeleo wa fursa za kimaslahi na hata ushirikina. Bahati mbaya ni kwamba, hiki kitu wapiga kura wengi hawana fursa wala njia ya kupata taarifa sahihi juu ya hao ya viongozi waliojitokeza na wanaopigiwa debe.