PreGE2025 Amani Manengelo, Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza, ameripotiwa kutekwa na kupotea tangu tarehe 14.02.2025 huko Misungwi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Amani Manengelo, Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza, ameripotiwa kutekwa na kupotea tangu tarehe 14.02.2025 huko Misungwi, Mwanza.

Pia Soma: Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Ameandika Martin Maranja Masese

Amani Manengelo ni kiongozi wa vijana wa CHADEMA mkoa wa Mwanza. Katibu wa BAVICHA Mkoa - Mwanza.
Nimepata habari za kutekwa na kupotea Manengelo nimesikitika sana… kwamba vitendo hivi vinaendelea?
Inaelezwa kwamba, Amani Manengelo alitekwa na watu wasiojulikana siku ya 14.02.2025, Misungwi, Mwanza.

Ni nchi zenye tawala dhalimu za kidikteta neiyo zinaweza kuteka vijana wadogo ambao ni wapinzani wa Serikali.
Nafikiri, sasa ni muda wa kuonesha vitendo dhidi ya maneno. Tuwaoneshe watekaji sisi siyo kuku bandani.

Yaitishwe maandamano makubwa ya kushinikiza watu wote waliotekwa na kupotea, warejeshwe kwa haraka.
Vijana wa CHADEMA Mwanza, ni wakati wa kuonesha nguvu ya umma kushinikiza Manengelo apatikane.

Tusiwaache wahuni kuamua nani atekwe na kupotezwa. Kesho watamteka mwingine na kila kitu kitaendelea.
Tunao uongozi mpya wa chama, na umesisitiza wazi utapambana na vitendo vya utekaji, ni muda muafaka.

Kwa kuwa wanatekwa wenzetu, tuoneshe kwa vitendo vitendo vya utekaji ni ushenzi na ushamba usiokubalika.

Kataa utekaji. Kataa utekaji. Kataa utekaji.

Pia Soma: Mara: Mfanyabiashara adaiwa kutoweka baada ya kuchukuliwa na watu waliojitambulisha kama "Usalama Wa Taifa". Mkewe azungumza kilichotokea!


Soma, Pia: Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi
 
Hatari kubwa sana hii.

Maandamano pekee hayawezi kukomesha vitendo vya Utekaji. Lakini hatua kali zaidi za kupinga vitendo hivi zinapaswa kuchukuliwa, VIta kali Sana kwa sasa inapaswa kuelekezwa kwenye upatikanaji wa Katiba Mpya iliyo nzuri
 
hiyo ni drama,
umendee mke wa wenyewe kisiri, ufumaniwe na kupigwa rungu, halafu mje hapa ati ng'we ng'we ng'we sijui amefanya nini, alaaaa!

kama ametekwa si umuokoe sasa, kumbwelambwela tu 🐒
 
Inatafutwa sababu ya kukamata viongozi wa CHADEMA na kuwaweka ndani wasiongoze harakati za kudai katiba mpya.

Nasisitiza huu ni mtego.
 
Abduction as usual, CCM ndio wahusika wakuu.
 
Tangu waliposema MMM anahisiwa kuwa mtu wa kitengo basi simwamini tena.
 
hiyo ni drama,
umendee mke wa wenyewe kisiri, ufumaniwe na kupigwa rungu, halafu mje hapa ati ng'we ng'we ng'we sijui amefanya nini, alaaaa!

kama ametekwa si umuokoe sasa, kumbwelambwela tu 🐒

..Mwita Waitara wa CCM naye analalamika kuwa kuna vijana wake wanaomuunga mkono wametekwa hawajulikani waliko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…