Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,791
- 31,803
AMAN THANI NA DHANA YA MWAFRIKA ZANZIBAR
4:43 AM Mohamed Said 0 Comments
Aman ThaniAman Thani ni mmoja wa wapigania uhuru wa Zanzibar na alipata kuwa Secretary General wa Zanzibar Nationalist Party mwaka wa 1963 akishika nafasi ya Abdulrahman Babu baada ya Babu kujitoa chama na kuunda chama chake Umma Party. Aliwekwa jela Zanzibar na Tanganyika baada ya mapinduzi. Aman Thani ni kati ya wanasiasa wachache waliobaki katika kundi lile lililopigania uhuru wa Zanzibar. Ameandika kitabu mashuhuri kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, ''Ukweli ni Huu.''
Kauli ya CCM Zanzibar jana kuwa Zanzibar si ya machotara bali ni ya Waafrika imekurupusha sege la nyuki wakali. CCM imekuwa ikilaniwa na kila mtu kote duniani khasa kutoka kwa wafuatiliaji wa siasa za Tanzania hususan visiwani Zanzibar.
Msome Aman Thani akieleza dhana ya Uafrika katika siasa za Zanzibar:
‘’...huenda ikawa tukakosana juu ya hili neno, ‘’Muafrika.’’ Kwangu mimi, ‘’Muafrika,’’ ni yoyote aliyezaliwa na kuishi katika kontineti la Afrika. Si muhimu asli ya kabila lake wala rangi ya mwili wake. Hapana shaka kuwa huu ndio msimamo wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika. Basi sijui kwa wengine Muafrika ni wa namna gani? Suruti awe wa rangi nyeusi na nywele za pilipili? Akiwa mweupe na nyele ndefu za singa, na wazazi wake wote wawili wamezaliwa Zanzibar, huyo hakubaliwi kuwa ni Muafrika?’’
4:43 AM Mohamed Said 0 Comments
Aman Thani