dedan kimathi
Member
- Dec 5, 2015
- 42
- 24
Wadau nawasalim,
Wadau,
Mimi na mke wangu tumekua na mgogoro wa muda mrefu kuhusu nani amfuate mwenzake, maana tunafanya kazi mikoa tofauti, yeye Dar mimi Bukoba, suala la uhamisho lilishindikana, na hivyo ikaonekana suluhu ni wife kuacha kazi anifuate mimi Bukoba, hata hivyo alikataa na kudai tuwe tunatembeleana mara kwa mara.
Hata hivyo zoezi hilo likawa gumu sana for geographical reason, wote mnajua umbali wa Dar_ Bukoba, sawa ndege zipo lakini ni ghali, zile za bei rahisi unapaswa ku book week kadhaa kabla ya safari, na kazini huwezi jua unapewa ruhusa lini.
Ikafika pahala tunamaliza miezi sita au zaidi bila kuonana, mama yake mzazi alikua akimbembeleza sana anifuate mimi Bukoba tuishi, kwamba ndoa ya mbali ina matatizo binti hataki ku sacrifice kazi yake.
Wakati wote huo wife alikua akiishi nyumbani kwao, nilikua na source wangu ndani ya hiyo nyumba who was a cousin sister to my wife, kwa mujibu wa huyu source mwenendo wa umekua ni mbaya sana, weekend hujipamba na kutoka usiku, hurudi mida mibaya, tena kwa kurudishwa na tinted car, hata week days kwa kawaida hurudi saa nne usiku wakati anafanya kazi serikalini wanakotoka saa tisa kwa kawaida.
Hata hivyo sikua na papara kwa taarifa hizo maana kugoma kwake kuhamia bukoba nilikuchukulia kwa uzito mkubwa kwamba kuna kitu
mwanzoni mwa mwaka huu wife alinipigia simu kuwa amekubali kuacha kazi kunifuata bukoba, tena anataka kuja ndani ya siku mbili, nikashangaa imekuaje all over sudden kubadilisha mawazo, nikainua wire kwa source wangu, it was a bomb shell, aliniambia mkeo ana mimba changa, anataka aje akupe mara moja mbili aseme ni ya kwako, kitu ambacho ni kweli maana wife alikua so desperate kutaka kuja kiasi cha kukata tiketi ya ndege.
Lakini wakati yote haya yanatokea luckily wiki hiyo hiyo likizo yangu ikawa approved, niliiomba December wakakataa wakasema utaenda january, so january wakati wife anadai anajiandaa kuja in two days time mimi nikapewa likizo, akastukia tu ananiona nyumbani kwao dar, nikafika na kuanzisha kesi moja kwa moja mbele ya mama yake na ku demand twende wote mguu kwa mguu tu kacheki mimba marie stopes ambapo ni mtaa wa nyuma tu, akagoma na kuanza kulia, mama alikua kainama tu.
Wote walikua wanajua mimi na wife tuna mwaka bila kuonana hivyo mimba hiyo sio yangu na mama mkwe alilijua hilo na kuvunja ukimya hapo hapo kwa hasira na kumwambia mwanae kuwa ""si nilikwambia uache kazi umfuate mumeo ukaniona mjinga, siwezi kushiriki dhambi yako ya kumbambika huyu bwana mtoto, maadam keshashtuka acha ajue tu, baba ni kweli ana mimba huyu kama ulivyosema".
Ndoa yetu ikawa imeishia hapo,taarifa zilizopo ni kwamba aliitoa mimba hiyo na bado yupo kwao, ingawa haendi kazini sijajua kilimtokea nini, hadi sasa ameshatuma wazee wengi kuja kuzungumza nami ili turudiane, wakiwemo ndugu zangu, ila bahati mbaya nimeshamfuta mazima rohoni mwangu, nikikumbuka nilivyokua namhubiria athari za kuishi mbali mbali na anakua mkaidi siwezi kumsamehe.
Cha msingi nimepona sasa na ninaendelea mbele.
Mungu mkubwa nilikua nibambikwe mtoto na mke wangu.

Last edited by a moderator: