Ally Salum Hapi, Rafiki wa Ridhiwani Kikwete aliyeukwa UDC

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
CUziZqbUwAEWzcW.jpg

Viongozi wa Jukwaa Huru la Wazalendo Kwanza Ndg Ally Salum Hapi (kushoto) na Mtela Mwampamba wakimzungumza na waandishi.

Mkuu wa Wilaya Mpya wa Kinondoni aliyechaguliwa na Rais Magufuli, Bwana Ally Salum Hapi ni kijana mzaliwa wa Nzega mkoani Tabora. Kijana huyu anayetoka katika familia ya kawaida kabisa (si ya kitajiri au uwezo wa kifedha) alipata elimu yake ya shule ya Msingi humo humo Mkoani Tabora. Baadae alichaguliwa Kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya Ufundi ya Wavulana Bwiru iliyoko jijini Mwanza.

Akiwa Bwiru Boys aliweza kuchaguliwa kuwa Kiranja Mkuu (Head Prefect) akiwa kidato cha pili tu. Hii ilichangiwa na uwezo wake wa ushawishi na ujenzi wa hoja kama alivyokuwa amejitanabaisha miongoni mwa wanafunzi. Ni katika Uongozi wake aliwashawishi wanafunzi wenzake kugoma na wao pasipo kujua nia yake walifanya hivyo. Katika mgomo huo aliwasaliti wenzake na akapelekea wanafunzi 15 wakifukuzwa shule ilihali yeye akibaki na hivyo kufanikiwa kumaliza shule japo hakufanya vizuri katika masomo ya ufundi (Technical subjects) hasa Fizikia lililokuwa kiungo kwa machaguo yote na hivyo kutopata chaguo la Serikali.

Kijana huyu alijiunga na masomo ya kidato cha tano katika shule moja ya binafsi jijini Dar es Salaam huku akiamua kusoma masomo HKL (History, Kiswahili and Language). Ikumbukwe kuwa hakuwa kusoma somo la Historia akiwa O level lakini alilazimika kulisoma akiwa A level. Mungu si Athumani Kijana huyu alifaulu kwa Kupata Daraja la Kwanza pointi 4, na hivyo kujiunga na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Kitivo Cha Sheria mwaka wa masomo 2007/2008. Akiwa mwaka wa kwanza alijaribu kujitangaza vya kutosha na hata Kufikishwa katika Kamati ya Maadili na Akina Owawa Stephen na David Silinde (Mbunge wa Mbozi Magharibi kupitia Chadema).

Cha ajabu katika kamati hiyo aliwasingizia kina Silinde, Owawa na Selemani Ally kuwa ndio wahusika wakuu, hivyo aliwasaliti katika makubaliano yao ya mwanzo na ya pamoja. Akiwa Chuoni alifanya harakati ili awe Rais wa serikali ya wanafunzi DARUSO. Katika harakati zake alikutana na vigogo wa CCM katika Hotel ya Travertine iliyoko Magomeni na kupatiwa fedha za kampeni na kuhonga wenyeviti wa Vitivo ili wampitishe. Baada ya hapo alikwenda kwa M/Kiti wa Kamati ya Bunge Mashirika ya Umma (wa Bunge la Tisa) na kuomba laki sita (Tsh 600,000/-) ili afanyie maandalizi ya kuwa mgombea (awahonge wenyeviti).

Baada ya harakati zake zote mwisho wa siku wakambwaga chini maana wanachuo wa UDSM si wakuchezea na alidhani kuwa atawahonga na fedha za mafisadi na kisha atapita. Hela walikula na bado wakamtosa. Hapo ndipo raha ya siasa. Alikuja kuambulia Ubunge wa kuteuliwa kutoka kwenye Kitivo chake cha Sheria. Akiwa Mbunge, Bunge la DARUSO kwa kauli moja lilimwamini na kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mabadiliko ya Katiba ya DARUSO mwezi Machi 2010. Bajeti kwa ajili ya kamati hii ilipitishwa na yeye kama Mwenyekiti wa Kamati alichukua Tsh 1,000,000 kwa ajili ya kazi mbali za Kamati katika kushughulikia Mabadiliko ya Katiba kwa maana ya Kuratibu mapendekezo na maoni ya wanafunzi chuoni. Cha ajabu hakuitisha hata kikao kimoja na wajumbe wake, pesa akala na hakuna mapendekezo yoyote aliyowasilisha. Bunge la wanafunzi lilipotaka kujua sababu za kutokuwepo mapendekezo ya katiba, lilivunjwa eti muda wake umeisha.

Hivi karibuni alipitishwa kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa UVCCM. Sina shaka na siasa zake za jukwaani maana anajenga hoja ipasavyo na anajiamini na hutetea kile anachokiamini hata kama ni cha kiusaliti/kinafiki au kifisadi. Shaka yangu iko katika Uadilifu wake, na Uzalendo wake kwa Vijana wenzake na taifa kwa Ujumla.

Kijana huyu si Mwadilifu na si Mzalendo na anaweza kununuliwa kwa bei rahisi sana kiasi cha kuuza uzalendo kwa wenye pesa. Kwa sasa anafanya kazi Crest Attorneys. Salum Ally Hapi amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu sana na ofisi za Ridhiwani Kikwete za GRK Advocates, Kwani ni Marafiki sana japo sijajua chanzo cha urafik wao

Hongera sana Mkuu wa Wilaya.
 
Nilimdharau sana kwenye makala yake ya wiki iliyopita iliyoletwa humu akimjibu Julius Mtatiro juu ya viwanda na uchumi wa taifa kwa ujumla.nilimwelewa kama anafaa kuwa kibaraka na kueneza propaganda kama akina Hans Polepole.Wanakwepa kusema ukweli ili kukibeba chama chao.amepata nafasi apewe hongera anaweza kubadilika na kutumikia wananchi kama Makonda.
 
Dubu nimekuelewa vizuri sana. Jamaa yaelekea kundi lake UDSM lilikua la wanafiki wanafiki tu. Maana mtu kama Selemani Ally ni bonge la snitch na mbea mbea, mpenda madaraka toka akiwa Tabora boys, Tanga Tech na hata UDSM.
 
Hongera kwa uteuzi huo, hongera kwa kuaminiwa na kukabidhiwa wilaya!

Watanzania mbona tuko hivi jamani!!??, yaani mtu amepewa dhamana, amekuwa recognized, basi tujenge angalau utamaduni wa kumpa 'Hongera' kwanza, kabla ya kumhukumu kwa aliyoyafanya huko nyuma (Kama kweli amefanya), huwezi kujua huko mbeleni anaweza kufanya vizuri sana. Hivi angekuwa ndugu yako ungesema maneno yote hayo??!!
 
Siasa ni unafiki mtupu,yani uweze kuhadaa watu na kugeuza maneno
Anyway hongera sana kwake
 
Haya mambo bwana mheshima sahizi angekuwa anaujua wimbo wa Ombea adui yako aishi siku nyingi iliunapo ....... ajionee kwa macho...... Angekuwa anatikisa kichwa kwa raha zake. Cha msingi achape kazi kuonyesha dhamira yake na kuuthibitishia umma kwama anaweza, allegations nyingine hatuwezi prove ila Utendaji wake kama mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndiyo uwe kipimo.
 
View attachment 340100
Viongozi wa Jukwaa Huru la Wazalendo Kwanza Ndg Ally Salum Hapi (kushoto) na Mtela Mwampamba wakimzungumza na waandishi.

Mkuu wa Wilaya Mpya wa Kinondoni aliyechaguliwa na Rais Magufuli, Bwana Ally Salum Hapi ni kijana mzaliwa wa Nzega mkoani Tabora. Kijana huyu anayetoka katika familia ya kawaida kabisa (si ya kitajiri au uwezo wa kifedha) alipata elimu yake ya shule ya Msingi humo humo Mkoani Tabora. Baadae alichaguliwa Kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya Ufundi ya Wavulana Bwiru iliyoko jijini Mwanza.

Akiwa Bwiru Boys aliweza kuchaguliwa kuwa Kiranja Mkuu (Head Prefect) akiwa kidato cha pili tu. Hii ilichangiwa na uwezo wake wa ushawishi na ujenzi wa hoja kama alivyokuwa amejitanabaisha miongoni mwa wanafunzi. Ni katika Uongozi wake aliwashawishi wanafunzi wenzake kugoma na wao pasipo kujua nia yake walifanya hivyo. Katika mgomo huo aliwasaliti wenzake na akapelekea wanafunzi 15 wakifukuzwa shule ilihali yeye akibaki na hivyo kufanikiwa kumaliza shule japo hakufanya vizuri katika masomo ya ufundi (Technical subjects) hasa Fizikia lililokuwa kiungo kwa machaguo yote na hivyo kutopata chaguo la Serikali.

Kijana huyu alijiunga na masomo ya kidato cha tano katika shule moja ya binafsi jijini Dar es Salaam huku akiamua kusoma masomo HKL (History, Kiswahili and Language). Ikumbukwe kuwa hakuwa kusoma somo la Historia akiwa O level lakini alilazimika kulisoma akiwa A level. Mungu si Athumani Kijana huyu alifaulu kwa Kupata Daraja la Kwanza pointi 4, na hivyo kujiunga na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Kitivo Cha Sheria mwaka wa masomo 2007/2008. Akiwa mwaka wa kwanza alijaribu kujitangaza vya kutosha na hata Kufikishwa katika Kamati ya Maadili na Akina Owawa Stephen na David Silinde (Mbunge wa Mbozi Magharibi kupitia Chadema).

Cha ajabu katika kamati hiyo aliwasingizia kina Silinde, Owawa na Selemani Ally kuwa ndio wahusika wakuu, hivyo aliwasaliti katika makubaliano yao ya mwanzo na ya pamoja. Akiwa Chuoni alifanya harakati ili awe Rais wa serikali ya wanafunzi DARUSO. Katika harakati zake alikutana na vigogo wa CCM katika Hotel ya Travertine iliyoko Magomeni na kupatiwa fedha za kampeni na kuhonga wenyeviti wa Vitivo ili wampitishe. Baada ya hapo alikwenda kwa M/Kiti wa Kamati ya Bunge Mashirika ya Umma (wa Bunge la Tisa) na kuomba laki sita (Tsh 600,000/-) ili afanyie maandalizi ya kuwa mgombea (awahonge wenyeviti).

Baada ya harakati zake zote mwisho wa siku wakambwaga chini maana wanachuo wa UDSM si wakuchezea na alidhani kuwa atawahonga na fedha za mafisadi na kisha atapita. Hela walikula na bado wakamtosa. Hapo ndipo raha ya siasa. Alikuja kuambulia Ubunge wa kuteuliwa kutoka kwenye Kitivo chake cha Sheria. Akiwa Mbunge, Bunge la DARUSO kwa kauli moja lilimwamini na kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mabadiliko ya Katiba ya DARUSO mwezi Machi 2010. Bajeti kwa ajili ya kamati hii ilipitishwa na yeye kama Mwenyekiti wa Kamati alichukua Tsh 1,000,000 kwa ajili ya kazi mbali za Kamati katika kushughulikia Mabadiliko ya Katiba kwa maana ya Kuratibu mapendekezo na maoni ya wanafunzi chuoni. Cha ajabu hakuitisha hata kikao kimoja na wajumbe wake, pesa akala na hakuna mapendekezo yoyote aliyowasilisha. Bunge la wanafunzi lilipotaka kujua sababu za kutokuwepo mapendekezo ya katiba, lilivunjwa eti muda wake umeisha.

Hivi karibuni alipitishwa kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa UVCCM. Sina shaka na siasa zake za jukwaani maana anajenga hoja ipasavyo na anajiamini na hutetea kile anachokiamini hata kama ni cha kiusaliti/kinafiki au kifisadi. Shaka yangu iko katika Uadilifu wake, na Uzalendo wake kwa Vijana wenzake na taifa kwa Ujumla.

Kijana huyu si Mwadilifu na si Mzalendo na anaweza kununuliwa kwa bei rahisi sana kiasi cha kuuza uzalendo kwa wenye pesa. Kwa sasa anafanya kazi Crest Attorneys. Salum Ally Hapi amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu sana na ofisi za Ridhiwani Kikwete za GRK Advocates, Kwani ni Marafiki sana japo sijajua chanzo cha urafik wao

Hongera sana Mkuu wa Wilaya.

Nenda kaliripoti hili katka ofisi za GLOBAL PUBLISHER
 
Back
Top Bottom