#COVID19 Aliyesimamishwa kazi asema video zilizosambaa zikionyesha hakuchomwa chanjo ya Covid-19 zimechezewa

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Arusha. Mkuu wa idara elimu msingi halmashauri ya Jiji la Arusha, Omary Kwesiga amesema ameshangazwa kusimamishwa kazi akidaiwa kufanya igizo la kuchomwa chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 .

Amesema picha za video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha kuwa hakuchomwa chanjo hiyo zimechezewa, na kubainisha kuwa alichanjwa.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Agosti 6, 2021 Kwesiga amesema anashangazwa na video hiyo, "nimezuiwa kuongea na vyombo vya habari kulingana na maadili ya kazi na kikubwa mimi nimechanjwa nina ushahidi na nipo Salama."

Ofisa huyo na ofisa muuguzi msaidizi wa hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Scolastica Kanje leo wamesimamishwa kazi na mamlaka zao kwa tuhuma za kufanya igizo la kuchanja.

Kwa takribani siku tatu video hiyo inayomuonyesha Kwesiga na Kanje wakifanya kile ambacho kimetafsiriwa ni maigizo imebua mjadala mitandaoni.

Mwananchi

My Take:
Inaonekana hata waliohukumu walifuata Mhemko tu, Hawakufuata "Natural Justice Principle". Ummy Mwalimu amekimbilia kwenye Media kuclear the air lakini walipaswa kuwahoji.
Muhusika anasema halikuwa Igizo, Waziri anasema lilikuwa Igizo.

Ha ha ha haaa
 
Anamtunishia msuli Waziri!
Anaonekana ana jeuri,si ajabu hata kwa mkurugenzi wake ni jeuri.
Apishe nafasi,apangiwe kazi idara ya habari,akaitumie simu yake vizuri.
 
Huyu Mkuu wa Idara ya Elimu Bwana Kwesiga anasalimiwa "Shikamoo Mume wangu" na kajimwalimu fulani Cha kike ambacho kina Mume Makini tuu hapa Arusha Kidongo Cheusi. Avune apandacho.

Mkuu wa Idara kama unasoma hapa jirekebishe maana muda c mrefu nakulipua endapo huyo ticha "ataninyima".
 
Wamesimamishwa kazi hawajafukuzwa wana nafafasi ya kutoa maelezo yao.
 
Huyu Mkuu wa Idara ya Elimu Bwana Kwesiga anasalimiwa "Shikamoo Mume wangu" na kajimwalimu fulani Cha kike ambacho kina Mume Makini tuu hapa Arusha Kidongo Cheusi. Avune apandacho.

Mkuu wa Idara kama unasoma hapa jirekebishe maana muda c mrefu nakulipua endapo huyo ticha "ataninyima".
Jamaa unasarandia kifaa ya mkurugenzi 😃😃😃 nimecheka Hilo biti lako sasa unapaswa umwambie huyo ticha akikunyima unamwambia nakulipua kwa mumeo.

Mkurugenzi Hana kosa maana sio yeye anayekunyima papuchi.
 
Apost ile original ambayo haijachezewa ili amuumbue Odo Mwaalimu
Kwakuwa alirekodi kwenye simu yake kupitia dereva wake,na akairusha mwenyewe kwenye groups tofauti,atakuwa anaongopea tu,ni jeuri za kijinga.
 
ile video hata mimi nimeona kama kuna kipande kimekatwa au ni wenge langu tu labda?
 
Anamtunishia msuli Waziri!
Anaonekana ana jeuri,si ajabu hata kwa mkurugenzi wake ni jeuri.
Apishe nafasi,apangiwe kazi idara ya habari,akaitumie simu yake vizuri.
Haki ya kikatiba. Uonevu wa aina yoyote hautakiwi
 
Huyu Mkuu wa Idara ya Elimu Bwana Kwesiga anasalimiwa "Shikamoo Mume wangu" na kajimwalimu fulani Cha kike ambacho kina Mume Makini tuu hapa Arusha Kidongo Cheusi. Avune apandacho.

Mkuu wa Idara kama unasoma hapa jirekebishe maana muda c mrefu nakulipua endapo huyo ticha "ataninyima".
duh
 
Back
Top Bottom