Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Mtuhumiwa wa ubakaji aliyefahamika kwa jina la john Nkondola mkazi wa manispaa ya Mtwara Mikindani amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Emily Mwambapa, Mwendesha mashtaka wa serikali Peter Museti amesema kulingana na vifungu vya kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho na sheria ya mwaka 2002, mtuhumiwa John Nkondola anatuhumiwa kwa kosa kumuingilia kimwili mtoto wa mwaka mmoja na nusu wakati shtaka la pili mtuhumiwa anashtakiwa kwa kosa la kumlawiti mtoto huyo huyo kinyume na maumbile kulingana na vifungu vya kanuni ya adhabu vilivyofanyiwa marekebisho na sheria ya mwaka 2002.
Hata hivyo mtuhumiwa amekana mashtaka yote mawili na amerudishwa rumande baadaya kukosa wadhamini 2 wa kusaini hati ya dhamana ya shilingi milioni 4 kila mmoja, na kesi imetajwa kusikilizwa tarehe 11-04 -2016.
Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho Salome Juma ameomba Jamhuri kufanya kazi yake, huku akisisitiza kitendo alichofanyiwa mtoto wake ni cha kinyama.