Aliyekuwa rais Korea Kusini Park Geun-hye 'kukamatwa'

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Waendesha mashtaka wamesema wataomba idhini ya kumkamata aliyekuwa rais wa taifa hilo Park Geun-hye, kwa mchango wake katika kashfa ya ulaji rushwa nchini humo.

Alipoteza kinga ya rais dhidi ya kfuunguliwa mashtaka mapema mwezi huu na akaondolewa rasmi madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kudumisha uamuzi wa bunge wa kumng'oa madarakani.

Bi Park anatuhumiwa kumruhusu rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kudai pesa kwa lazima kutoka kwa kampuni kubwakubwa.

Bi Park amekanusha madai hayo. Rais huyo wa zamani aliomba radhi kwa umma wiki iliyopita, kabla ya kuhojiwa na maafisa wa mashtaka kwa saa 14.

Waendeshaji mashtaka walisema Jumatatu kwamba "wameamua kwamba ni vyema, kwa kufuata sheria na maadili nchini humo, kuomba kibali cha kumkamata".

_95247301_7f120ee1-d900-419b-a8ba-77bc4a19a215.jpg

Wanasema ushahidi, ambao unapatikana katika diski za kompyuta huenda ukaharibiwa iwapo Bi Park hatakamatwa.

Bi Choi amefunguliwa mashtaka ya ulaji rushwa na tayari kesi dhidi yake imeanza.

Park aling'olewa vipi madarakani?

Bi Park aliondolewa madarakani kutokana na uhusiano wake wa karibu na Bi Choi.

Bi Choi anatuhumiwa kutumia uhusiano wake na rais huyo kushinikiza kampuni kutoa mamilioni ya dola kama mchango kwa nyakfu za kusaidia jamii ambazo alikuwa anazisimamia.

_95063889_gettyimages-631002210.jpg

Kaimu mkuu wa kampuni kubwa ya vifaa vya kielektroniki ya Samsung, Lee Jae-yong, alikamatwa kuhusiana na kashfa hiyo.

Bi Park, 65, anadaiwa kuhusika moja kwa moja katika hili, na kwamba alimruhusu Bi Choi uhuru wa kiwango kisichokubalika wa kufikia nyaraka rasmi za serikali.

Chanzo: BBC
 
Wakati mnalalama kwa wakorea kuwa Na utawala WA kiimla lakini wamethubutu kwa Hilo sasa sidhani viongozi WA tawala za kiafrika wanaliweza Hilo labda Ghana Na Nigeria lakini Gambia tuliona mbinde lake
 
Wakati mnalalama kwa wakorea kuwa Na utawala WA kiimla lakini wamethubutu kwa Hilo sasa sidhani viongozi WA tawala za kiafrika wanaliweza Hilo labda Ghana Na Nigeria lakini Gambia tuliona mbinde lake
Korea kusini kuna democracy ila north Korea ndio kuna utawala wa kiimla
 
Back
Top Bottom