Aliyekuwa Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Mwanza ajivua uanachama

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
CHADEMA-LOGO.png

Aliyekuwa Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mwanza, Adrian Tizeba ametangaza kujivua uanchama na kuachana na siasa.

Tizeba aliyesimamishwa uongozi na Baraza la Uongozi la CHADEMA tangu Mei 4, mwaka jana, alisema hatajiunga na chama chochote cha siasa.

Kwa uamuzi huo, Tizeba amepoteza nyadhifa zake zote ikiwamo ya uenyekiti wa Baraza la uongozi la mkoa na ujumbe wa Baraza la Uongozi Kanda ya Ziwa.

Mei 5, mwaka jana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, wakati huo, Dk Willibrod Slaa, alimuandikia barua Tizeba yenye Kumb Na C/HO/ADM/KK/08,kumsimamisha uongozi wa chama hicho.

Akizungumzia uamuzi wa kiongozi huyo kujivua uanachama na kuachana na siasa, Mratibu wa CHADEMA Kanda ya Ziwa, Renatus Bujiku alisema chama hicho kimepokea kwa mshtuko taarifa hizo kwa sababu bado suala lake lilikuwa linashughulikiwa.

“Utaratibu wa chama ulikuwa unaendelea kushughulikia suala lake, nadhani kachukua uamuzi wa haraka,”*alisema Bujiku.
 
Huwezi kusaliti chama halafu uachwe hivihivi tu, aende huko akavue samaki ziwa Victoria au akalime au akafuge sungura lakini kwenye chama hatufai
 
Huu ndio uzuri wa chadema "hakuna maarufu zaidi ya chama" ulete upuuzi uachwe tu hakunaga, hayo yanapatikana ccm tu, hata hawa wala rushwa ccm haitathubutu kuwafutia uanachama kwa hofu tu ya kupoteza majimbo yao, kwa ccm ni bora wananchi waongozwe na kiongozi mbovu lakini ni wa chama chao kuliko kiongozi mahiri kutoka upinzani, ccm chama kwanza nchi baadae.
 
Bila tizeba na wilson mushumbusi chadema imekula kwenu
 
Mkuu salaam,
Comment yako inaonyesha kuwa huelewi vizuri historia ya chadema mwanza kwanza Mshumbusi na Tizeba hawajawahi kufanya kazi ya uongozi wa chadema kwa. Wakati mmoja maana Wakati Tizeba anaanza kuongoza mkoa wa mwanza tayari Mshumbusi alishavuliwa uongozi na baadae akahama chama.
 
Aliyekuwa Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mwanza, Adrian Tizeba ametangaza kujivua uanchama na kuachana na siasa.

Tizeba aliyesimamishwa uongozi na Baraza la Uongozi la CHADEMA tangu Mei 4, mwaka jana, alisema hatajiunga na chama chochote cha siasa.

Kwa uamuzi huo, Tizeba amepoteza nyadhifa zake zote ikiwamo ya uenyekiti wa Baraza la uongozi la mkoa na ujumbe wa Baraza la Uongozi Kanda ya Ziwa.

Mei 5, mwaka jana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, wakati huo, Dk Willibrod Slaa, alimuandikia barua Tizeba yenye Kumb Na C/HO/ADM/KK/08,kumsimamisha uongozi wa chama hicho.

Akizungumzia uamuzi wa kiongozi huyo kujivua uanachama na kuachana na siasa, Mratibu wa CHADEMA Kanda ya Ziwa, Renatus Bujiku alisema chama hicho kimepokea kwa mshtuko taarifa hizo kwa sababu bado suala lake lilikuwa linashughulikiwa.

“Utaratibu wa chama ulikuwa unaendelea kushughulikia suala lake, nadhani kachukua uamuzi wa haraka,”*alisema Bujiku.

Hahahaaaa ndio maana mie hua nasema "African democracy and its application is total different from the democracy of Europe and America....."
Tangu mwaka jana eti suala lake linashughulikiwa..... halafu eti mkija huku nje mnadai eti CCM hawana democracy, hii ni nini sasa, kumbe na nyie ni wabakaji tu wa-democrasia.

Eti ".....kimepokea kwa mshtuko taarifa hizo kwa sababu bado suala lake lilikuwa linashughulikiwa..." unafiki mtupu
 
Al
View attachment 334592

Aliyekuwa Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mwanza, Adrian Tizeba ametangaza kujivua uanchama na kuachana na siasa.

Tizeba aliyesimamishwa uongozi na Baraza la Uongozi la CHADEMA tangu Mei 4, mwaka jana, alisema hatajiunga na chama chochote cha siasa.

Kwa uamuzi huo, Tizeba amepoteza nyadhifa zake zote ikiwamo ya uenyekiti wa Baraza la uongozi la mkoa na ujumbe wa Baraza la Uongozi Kanda ya Ziwa.

Mei 5, mwaka jana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, wakati huo, Dk Willibrod Slaa, alimuandikia barua Tizeba yenye Kumb Na C/HO/ADM/KK/08,kumsimamisha uongozi wa chama hicho.

Akizungumzia uamuzi wa kiongozi huyo kujivua uanachama na kuachana na siasa, Mratibu wa CHADEMA Kanda ya Ziwa, Renatus Bujiku alisema chama hicho kimepokea kwa mshtuko taarifa hizo kwa sababu bado suala lake lilikuwa linashughulikiwa.

“Utaratibu wa chama ulikuwa unaendelea kushughulikia suala lake, nadhani kachukua uamuzi wa haraka,”*alisema Bujiku.
Aliyekuwa....!
 
Back
Top Bottom