Aliyekuwa mgombea wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa (CCM) akwama tena kortini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imekwama kuendelea kusikiliza ushahidi wa aliyekuwa mgombe ubunge wa Ukonga, Jerry Silaa (CCM) baada ya kuwekewa pingamizi na upande wa walalamikiwa,

Pingamizi hilo la kukosoa ushahidi wa Silaa limetolewa na upande wa walalamikiwa kupitia Onesmo Kyauke, Wakili wa Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), mbele ya Fatuma Msengi, Jaji katika mahakama hiyo.

Amesema kuwa, shahidi huyo amejibu swali wakati alipoulizwa na wakili wake ambaye ni Dk. Masumbuko Lamwai kuhusu masanduku ya kura kuchelewa kwenye baadhi ya vituo na kujibu nje ya kiapo chake, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Kutokana na sababu hiyo, Wakili Kyauke ameiomba mahakama kumzuia shahidi huyo kutoendelea na ushahidi wake pamoja na kumzuia asijibu hoja nje ya hati za kiapo.

Hata hivyo, Wakili Lamwai ameiomba mahakama kuliondoa pingamizi hilo akidai kuwa kiapo chake kinaweza kujibiwa kwa maneno na sio maandishi bila kuathiri kitu chochote.

Wakili Lamwai ametoa mfano wa rufaa ya kesi ya Zena ambayo aliieleza mahakama kuwa, atajibu kwa hati ya maandishi lakini kwenye maswali alijibu nje ya hati hiyo.

Kutokana na mvutano wa kisheria ambao uliibuka kutokana na pingamizi hilo, Jaji Msengi ameahirisha kesi hiyo hadi kesho kwa ajili ya kutoa uamuzi kuhusu ushahidi wa Silaa kuwa nje hati ya kiapo ama la.

Jana katika ushahidi wa kesi hiyo, Silaa alidai kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walimtishia kuchoma moto nyumba yake wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Pia Silaa alidai Oktoba 27, mwaka jana katika kituo cha majumuisho ya kupigia kura cha Pugu Sekondari idadi ya wapigakura wa Chadema iliongozeka huku wakiwa wamesimama mita 20 kutokea usawa wa kituo cha majumuisho.

Silaa ambaye aliwahi kuwa Meya wa Ilala alidai kuwa, wafuasi hao walianza kuwatishia mawakala na msimamizi wa kituo jambo lililosababisha Polisi washindwe kufanya kitu zaidi ya kuwaonya pamoja na kuzungumza kihenyeji na mlalamikiwa wa pili.

“…kutokana na mazungumzo hayo, mjibu maombi wa pili na wenzake walisema hawatopokea majibu ya kupiga kura na pia watachoma moto nyumba yangu pamoja na kituo chenyewe,” alidai Silaa.
 
Huyu kijana ni kati ya watu wa kuhurumiwa sana ! Huyu ni Meya wa kwanza duniani kuangushwa na Mwenyekiti wa kijiji , kama vipi mkuu waitara iambie mahakama ifute matokeo ili turudi uwanjani , huyo jerry hatopata hata robo ya kura alizopata octoba kudadeki !
 
Wataiba
 
Hatimaye jimbo linarudi tena kwenye uchaguzi
 
Back
Top Bottom