Alinijibu hivi baada ya kushindwa kumtumia pesa. Naomba ushauri wenu wakuu

khidego

Senior Member
Dec 25, 2016
132
308
Nitangulize pole kwa majukumu kwenu nyote na niende moja kwa moja kwenye lengo!

Kwa utangulizi ni kwamba mimi ni kijana wakiume, wa pekee katika familia ya watoto watatu, nina mchumba ambae tunaelekeana umri na niko nae kwa mda mrefu kidogo... tumepitia changamoto nyingi lakini Mungu mwema tunaendelea kusonga mbele;

Katika maisha yangu kuna kiumbe anaitwa Mama huwa namuheshimu na kumpenda sana, kuna mengi yanayofanya nimpende lakini kubwa ni kutokana na namna alivopitia mengi mpaka kupatikana kwangu (kwa kifupi ni kwamba nlipatikana kama ectopic pregnancy) kitu kilichopelekea afanyiwe oparesheni mara 2 mpaka kupatikana kwangu ni mengi alipitia lakini Mungu mwema mpaka leo mimi na yeye tuko salama.

Siwezi kuandika yote lakini kwa kifupi mnielewe kwamba Mamaangu ndie hero wa maisha yangu mpaka nilipo, na hata kwa huyo mchumba nilisha declare interest juu ya nafasi ya mama kwene maisha yangu.

Kisa kipo hivi, huyu mchumba tumekuwa tukisapotiana mambo mengi sana, ila ilitokea siku ya Valentine ameniomba kihela kidogo tu aenjoy na yeye huko aliko na kwa huo muda mamaangu alikuwa anaumwa na tukawa tunafanya mipango ya kumpeleka hospital, so hela iliyokuwepo nikatuma kwa mama isaidie matibabu yake na nyingine nikaweka akiba endapo niliyotuma haitatosha

Yeye aliponikumbusha juu ya hela aliyoniomba nikamwambia hela nimemtumia mama anaumwa ngoja nione maendeleo yake then ntakutumia alichonijibu ndo huwa kinanipa taabu mpaka leo, bila hata kutaka kujua hali ya mama ikoje alinijibu, "KWANI BABAAKO HUWA HAWEKI AKIBA MPAKA WEWE UTUME HELA MAMA ANAPOUMWA"

Hii sentensi iliniacha na maswali ambayo yananitatiza sana juu ya mtazamo wa huyu mwenzangu kwa sababu yeye nimekuwa nikimsapoti ninapoweza bila kujali ana ndugu na wazazi sasa kwanini yeye aseme hivyo kipindi ambacho mzazi wangu yupo serious anaumwa?

Ninachoomba ushauri hapa ni kwamba,

1. Nifanye nini ili hili alilonijibu lisiendelee kunifanya nimfikirie tofauti, maana tangu kipindi icho najikuta upendo nlokuwa nao kwake unapungua kidogo kidogo

2. Hilo jibu linaleta picha gani juu ya mahusiano yetu huko mbeleni ( Na hasa juu ya kuwakumbuka wazazi waliotupambania mpaka tunafika hatua tuliyopo)

3. Hatua gani nichukue maana ndo kwanza ni wachumba, ama nini nifanye ili nipate amani.

NATANGULIZA SHUKRANI
 
Hatua ya kwanza:kaa naye mwambie kwamba hiyo kauli hukuipenda halafu uone atasemaje.
Hatua ya pili:akinyenyekea na kuomba msamaha msamehe tu akikaza fuvu na kudai hana kosa achana naye fasta.
Sawa mkuu, nitajaribu kufanya ivo pia.. asante kwa ushauri
 
Muda wa daku bado. Kwangu mimi, nadhani siku hiyo hiyo ningekata mawasiliano, wala nisingelihitaji ushauri kutafuta amani kwa nini huyu mwanamke nisimuweke kwenye kundi la watu wasio na utu.

Ukali na uchungu wa maneno yake utaujua vizuri ukiamua kumwambia Mzee au Bi Mkubwa maneno hayo uone povu watakalolitoa. Lakini na wewe una roho ngumu sana, huyo mtu bado upo nae tu... Msalimie!
 
Muda wa daku bado. Kwangu mimi, nadhani siku hiyo hiyo ningekata mawasiliano, wala nisingelihitaji ushauri kutafuta amani kwa nini huyu mwanamke nisimuweke kwenye kundi la watu wasio na utu.

Ukali na uchungu wa maneno yake utaujua vizuri ukiamua kumwambia Mzee au Bi Mkubwa maneno hayo uone povu watakalolitoa. Lakini na wewe una roho ngumu sana, huyo mtu bado upo nae tu... Msalimie!

Niko nae bado mkuu, ila naamini hakuna ambae yuko perfect... ndo mana imebidi niulize na nyie wenzangu nione uzito wa hili swala.

maana naona kila nikikumbuka hilo linanipa shida sana,asante kwa mchango na Daku bado kidogo ila kila la heri na daku njema.. bila shaka tumesogeza sogeza vyungu kibao saizi
 
Niko nae bado mkuu, ila naamini hakuna ambae yuko perfect... ndo mana imebidi niulize na nyie wenzangu nione uzito wa hili swala..
maana naona kila nikikumbuka hilo linanipa shida sana,
asante kwa mchango na Daku bado kidogo ila kila la heri na daku njema.. bila shaka tumesogeza sogeza vyungu kibao saizi
Mkuu ndio maana nakupa hongera kwa kuwa na roho ngumu, mimi ni mwepesi sana kwenye mambo serious kama hayo.

Kauli ya mtu wako sio nzuri, inawezakana aliongea akiwa na hasira. Lakini hata hivyo inaonekana ni mtu asiye na hofu wala utu... Tuache kuchukua advantage ya kuwa hakuna aliyekamilika. Kuna mambo mtu anapaswa kuyafanya yanyooke, wakati unamwambia Mama anaumwa, ilikuwa ni jukumu lake kukufariji, lakini ndio kwanza anaomba pesa ya mtoko na matusi juu.
 
Labda nikushauri kijana mwenzangu,kwenye uchumba Kuna changamoto nyingi na moja wapo ni hiyo uliyo kutana nayo na sio kila changamoto una ichukulia kama kikwazo wakati mwingine hayo tunayaita majaribu ,na kwa dunia ya Leo ni watu wachache wanaoweza kuchukua mapungufu ya wenza wao na kukubaliana nayo.

Mimi kwa ushauri wangu usimuache binti huyo haraka kisa katamuka maneno hayo japo mzazi ni nguzo mhimu jaribu kumuita na kumwambia jinsi alivyo kukwaza na akiomba msamaha msamehe kwa roho moja na msonge mbele ila akiwa kiburi jua huyo sio liziki maana mzazi hapatikani supermarket ila mchumba wapo na bado wanazaliwa
 
lyalya, ]Thanks mkuu, ntajaribu kuzungumza nae, mpaka nakuja kuomba ushauri hapa, nimekaa nalo mda mrefu ila nimeona linanipa shida
 
Kwani tofauti na hiyo kauli yake ambayo imekupa mashaka kuna kingine alishawahi kufanya/kukuambia kabla au baada kikakupa tena mashaka?.....

Kama ndio basi unaweza kuwaza kuchukua maamuzi ILA kama hapana basi haina haja ya hayo yote mzee utaacha wangapi? Unaweza kupotezea tu huwezi kujua alivyokujibu vile alikua katika mood gani maana sisi binadamu tumeumbwa na hisia na wakati mwingine tunashindwa kuzizuia....

Jambo la msingi usiache kuongeanae juu ya hili swala ajue kama alifanya makosa kutoa hiyo kauli na hukuifurahia. Maisha yaendelee
 
nashukuru mkuu kwa ushauri, yapo ambayo tunapishana ila yanavumilika... na linaloendana na iyo kauli ni mala nyingi naonaga hapendi umwambie matatizo unayopitia, yaan mfano ukamshirikisha unataka kufanya kitu fulani afu badae ukashindwa kwa sababu ya changamoto kadha wa kadha, badala ya kukufariji anakulaumu na kutaka mgombane kabisa, ndo mana imebidi nifikirie sana Davet,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom