Steven mushi mushi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2016
- 533
- 739
Ni kweli unakipaji cha mziki lakini kwa Diamond bado sana yaani uwezo wako ni mdogo mno hata haufikii nusu ya robo ya uwezo alionao diamond . Diamond yeye ni msanii wa kimataifa hilo lipo wazi na wewe ni msanii wa hapahapa huo ndo uwezo wako inabidi tu ukubaliane nao.
Diamond anafanya kolabo na wasanii wa kimataifa kama kina neyo, Rihanna na p square wakati wewe unafanya kolabo na watoto kama nuhu mziwanda, baraka de Prince na akina ommy dimpoz lakini cha kushangaza unajiita king wa bongo fleva.
Diamond shoo zake ni za kimataifa yeye hufanya kolabo zake nchini Marekani, Uingereza pamoja na Ufaransa wakati wewe shoo zako ni za matopeni ambazo nyingi huwa unazifanyia kwenye viwanja vya ccm kirumba, uwanja wa sokoine pamoja na uwanja wa polisi Dodoma lakini cha kushangaza unajiita king wa bongo fleva.
Huu ni ushauri wangu kwako, kwanza kabisa kubali uwezo wako kama kitu hukiwezi kubali kuwa hukiwezi. Najua mambo mengi unafanya hata yale ambayo huna uwezo nayo ili tu uwaridhishe mashabiki wako, kwa mfano mwaka jana Diamond alitoa msaada wa shilling million 19 kwa ajili ya utengenezaji wa madawati ya shule na mashabiki wako walipoona hivyo walikushinikiza nawe kutoa msaada ambao kwa kweli hukuwa na uwezo nao lakini kwa vile ulitaka kumfunika Diamond ukatoa msaada wa shilling million 21 kwa ajili ya ujenzi wa madawati na ile hela uliyotoa hadi leo unaililia kwani haukuwa uwezo wako kutoa kiasi kile bali tu lilikuwa ni shinilizo kutoka kwa mashabiki wako.
Ni kweli mashabiki wako wana umuhimu mkubwa sana katika kazi yako ya mziki lakini sio kila kitu wanachotaka ufanye basi ufanye bali unapaswa kufanya kile chenye manufaa kwako na kile ambacho una uwezo nacho na sio kufanya mambo ya sifa eti tu ili umfunike diamond.
Kitu kingine ninachotaka kukushauri ni kuwa unapaswa kuwa msikifu na usikilize ushauri unaopewa na watu na sio kujifanya kila kitu unajua wakati hakuna kitu unachojua hata haya mafanikio aliyonayo diamond hakuyapata kwa uwezo wake pekee bali alisikiliza ushauri wa watu mbalimbali na kuufanyia kazi.
Na sisi mashabiki tuache tabia ya kuwapa vichwa wasanii wetu wakati tunajua fika kuwa uwezo wake ni mdogo na hii tabia ya kuwagombanisha wasanii wetu kwani tunasababisha ugomvi usio na tija yoyote katika taznia ya mziki na sanaa kwa ujumla katika nchi yetu.
Mwisho naomba nieleweke kuwa mimi sio timu diamond na wala sina timu yoyote bali tu nimeamua kutoa ushauri wangu kwa Alikiba nikiwa kama mmoja wa mashabiki wakubwa wa mziki hapa nchini Tanzania.