Alichosema Dyran Kerr baada ya kutimuliwa Simba

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,673
1,571
Pluijm amtetea Kerr
Wakati kocha Yanga, Hans Pluijm akiituhumu Simba kufanya uamuzi wa kukurupuka kumfukuza Dylan

Kocha wa Yanga, Han Pluijm (kushoto) akizungumza na aliyekuwa kocha wa Simba, Dylan Kerr. Picha ya Maktaba.
Dar es Salaam. Wakati kocha Yanga, Hans Pluijm akiituhumu Simba kufanya uamuzi wa kukurupuka kumfukuza Dylan Kerr, mwenyewe ameiitaka Simba imlipe stahiki zake ili waachane kwa amani.

Simba imevunja mkataba na Kerr tangu juzi na jana kocha huyo aliliambia gazeti hili kuwa, hana tatizo na uamuzi huo, lakini akasisitiza anachosubiri ni kulipwa mshahara wake wa miezi miwili na nusu, ambao Simba haikumlipa tangu Novemba pamoja na stahiki zake nyingine ili waachane kwa amani.

“Ninadai mshahara wangu wa miezi miwili na nusu, uongozi haujui nakula nini, haujui naishi vipi, siyo mimi tu hata wachezaji wangu hawajapewa mishahara, watachezaje kwa raha, watajitumaje?”

“Ni nani anaweza kufanya kazi akiwa na njaa? anasumbuka kupata haki yake, nakwambia tulipotoka Mtwara kwenye mechi ya Mwadui wachezaji wangu walishagoma kwenda Zanzibar wakishinikiza wapewe mishahara yao, nusura

Simba isishiriki yale mashindano, lakini niliwasihi tukaenda Zanzibar. Sijali kuondolewa Simba hiyo ni moja ya kazi za makocha,” alisema.

Kerr alikuwa akipokea kiasi cha Dola 9,000 (Sh 20 milioni ) kila mwezi, dola 6,000 (Sh13.2 milioni ) ikiwa ni mshahara kwa mwezi na kiasi kilichobaki kutumika kumlipia gharama mbalimbali zikiwamo za nyumba na usafiri.

Kutokana na hali hiyo Simba italazimika kumpa Kerr kitita cha zaidi ya Sh40 milioni.

Rais wa Simba, Evance Aveva akizungumzia kauli za wadau wa michezo juu ya Simba kumtoa ‘kafara’ Kerr, alisema suala hilo litajadiliwa katika mkutano maalumu ambao Simba imepanga kuufanya wakati wowote kuanzia leo. Aveva alisema, tayari klabu yao imeanza mchakato wa kumpata kocha mkuu atakayechukua nafasi ya Kerr, ambaye pia amebainisha kuwa

mipango itakapokamilika wataweka wazi kwenye mkutano huo.

Kauli ya Pluijm kuondoka kwa Kerr Hata hivyo, kitendo cha Simba kumtimua Kerr kimetafsiriwa kama cha kukurupuka na Kocha wa Yanga, Hans Pluijm, ambaye amesisitiza kuwa

klabu hiyo haikuwa na sababu za msingi za kufanya uamuzi huo.

“Sidhani kama Kerr kafukuzwa kwa uwezo wa timu, labda kuna sababu nyingine tu, lakini siamini kama Simba ipo sahihi kumfukuza kocha ambaye katika msimamo wa ligi timu yake ipo nafasi ya tatu.

“Hata ukiangalia mechi alizoshinda tangu amejiunga na Simba bado rekodi yake ipo vizuri, kwa hili napingana na uamuzi wa Simba, Kerr hakustahili kufukuzwa,” alisema Mdachi huyo wa Yanga, ambaye timu yake pia iliondolewa katika hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Mapinduzi kama ilivyokuwa kwa Simba.

Mbali na Kerr, pia Kocha wa Makipa, Mkenya Salim Idd alisema hawezi kutoa mguu wake kwenye ardhi ya Tanzania hadi pale Simba itakapompa stahiki zake na kuwataka viongozi wa Simba wajikague wenyewe upungufu wao badala ya kuwadhalilisha kuwa timu ni dhaifu.

“Unaposema timu dhaifu hakuna mchezaji tuliyemsajili sisi, wote wamesajiliwa na viongozi, viongozi wajitathmini kwa upande wao wametekeleza majukumu yao kwa kiasi gani?

“Timu ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, imecheza mechi 30 imeshinda mechi 19, tumepoteza michezo mitano na tumetoka sare sita hicho, sio kigezo cha kutuondoa. Kikubwa ninafarijika kuona wachezaji wapo nyuma yetu,” alisema Idd. Mayay aipa neno Simba Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Ally Mayay alisema kitendo cha Simba kufukuza makocha mara kwa mara kitazidi kuwarudisha nyuma.

“Kilichopo Simba wanahitaji mafanikio ya haraka, kukosa kwao nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa kwa muda mrefu kunawasumbua na kufanya mabadiliko ya mara kwa mara
 
Simba wako hoi kifedha ndo tatizo kubwa, timu wamkabidhi MO mambo yaende
 
Kuna kitu zaid naimani wanafahamiana wao kwa wao coz sioni sababu ya kumtimua MTU ghafula hivyo hata mambele mambo hayoko kihivyo kama kushinda ama kushindwa yote heri ukitaka uwe wewe mshindi tu kila siku then utakuwa unashindana na nan sasa?
 
Soka la afrika linaongozwa na watu wanaofikiri kama manyani.

Kwa mtindo huu unategemea ufanye vizuri kimataifa?
 
Naomba niseme tena, SIMBA inaendeshwa kienyeji sana.
 
miezi miwili na nusu alikuwa anaishije

pole sana Kerr

wanachama wa simba tumelala sana
 
Pluijm amtetea Kerr
Wakati kocha Yanga, Hans Pluijm akiituhumu Simba kufanya uamuzi wa kukurupuka kumfukuza Dylan

Kocha wa Yanga, Han Pluijm (kushoto) akizungumza na aliyekuwa kocha wa Simba, Dylan Kerr. Picha ya Maktaba.
Dar es Salaam. Wakati kocha Yanga, Hans Pluijm akiituhumu Simba kufanya uamuzi wa kukurupuka kumfukuza Dylan Kerr, mwenyewe ameiitaka Simba imlipe stahiki zake ili waachane kwa amani.

Simba imevunja mkataba na Kerr tangu juzi na jana kocha huyo aliliambia gazeti hili kuwa, hana tatizo na uamuzi huo, lakini akasisitiza anachosubiri ni kulipwa mshahara wake wa miezi miwili na nusu, ambao Simba haikumlipa tangu Novemba pamoja na stahiki zake nyingine ili waachane kwa amani.

“Ninadai mshahara wangu wa miezi miwili na nusu, uongozi haujui nakula nini, haujui naishi vipi, siyo mimi tu hata wachezaji wangu hawajapewa mishahara, watachezaje kwa raha, watajitumaje?”

“Ni nani anaweza kufanya kazi akiwa na njaa? anasumbuka kupata haki yake, nakwambia tulipotoka Mtwara kwenye mechi ya Mwadui wachezaji wangu walishagoma kwenda Zanzibar wakishinikiza wapewe mishahara yao, nusura

Simba isishiriki yale mashindano, lakini niliwasihi tukaenda Zanzibar. Sijali kuondolewa Simba hiyo ni moja ya kazi za makocha,” alisema.

Kerr alikuwa akipokea kiasi cha Dola 9,000 (Sh 20 milioni ) kila mwezi, dola 6,000 (Sh13.2 milioni ) ikiwa ni mshahara kwa mwezi na kiasi kilichobaki kutumika kumlipia gharama mbalimbali zikiwamo za nyumba na usafiri.

Kutokana na hali hiyo Simba italazimika kumpa Kerr kitita cha zaidi ya Sh40 milioni.

Rais wa Simba, Evance Aveva akizungumzia kauli za wadau wa michezo juu ya Simba kumtoa ‘kafara’ Kerr, alisema suala hilo litajadiliwa katika mkutano maalumu ambao Simba imepanga kuufanya wakati wowote kuanzia leo. Aveva alisema, tayari klabu yao imeanza mchakato wa kumpata kocha mkuu atakayechukua nafasi ya Kerr, ambaye pia amebainisha kuwa

mipango itakapokamilika wataweka wazi kwenye mkutano huo.

Kauli ya Pluijm kuondoka kwa Kerr Hata hivyo, kitendo cha Simba kumtimua Kerr kimetafsiriwa kama cha kukurupuka na Kocha wa Yanga, Hans Pluijm, ambaye amesisitiza kuwa

klabu hiyo haikuwa na sababu za msingi za kufanya uamuzi huo.

“Sidhani kama Kerr kafukuzwa kwa uwezo wa timu, labda kuna sababu nyingine tu, lakini siamini kama Simba ipo sahihi kumfukuza kocha ambaye katika msimamo wa ligi timu yake ipo nafasi ya tatu.

“Hata ukiangalia mechi alizoshinda tangu amejiunga na Simba bado rekodi yake ipo vizuri, kwa hili napingana na uamuzi wa Simba, Kerr hakustahili kufukuzwa,” alisema Mdachi huyo wa Yanga, ambaye timu yake pia iliondolewa katika hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Mapinduzi kama ilivyokuwa kwa Simba.

Mbali na Kerr, pia Kocha wa Makipa, Mkenya Salim Idd alisema hawezi kutoa mguu wake kwenye ardhi ya Tanzania hadi pale Simba itakapompa stahiki zake na kuwataka viongozi wa Simba wajikague wenyewe upungufu wao badala ya kuwadhalilisha kuwa timu ni dhaifu.

“Unaposema timu dhaifu hakuna mchezaji tuliyemsajili sisi, wote wamesajiliwa na viongozi, viongozi wajitathmini kwa upande wao wametekeleza majukumu yao kwa kiasi gani?

“Timu ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, imecheza mechi 30 imeshinda mechi 19, tumepoteza michezo mitano na tumetoka sare sita hicho, sio kigezo cha kutuondoa. Kikubwa ninafarijika kuona wachezaji wapo nyuma yetu,” alisema Idd. Mayay aipa neno Simba Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Ally Mayay alisema kitendo cha Simba kufukuza makocha mara kwa mara kitazidi kuwarudisha nyuma.

“Kilichopo Simba wanahitaji mafanikio ya haraka, kukosa kwao nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa kwa muda mrefu kunawasumbua na kufanya mabadiliko ya mara kwa mara
Nimefedheheka mno na kauli ya Suleiman Matola kumshutum Kerr. Ninapata wasiwasi kama kweli Matola ni kocha hashwa au anaumia kutoka Simba, huyu jamaa kawa kocha msaidizi pale muda mrefu tu akiwaona makocha wake wakifukuzwa kama mbu.
 
Hakuna timu zinazoniudhi kwenye ulimwengu wa soka Kama Simba na Yanga. Nazichukia timu hizi timu mbili basi Tu. Zinahusika moja kwa moja kuua soka la Bongo
 
Msemaji wa Simba jana alikuwa Clouds kipindi cha sports bar.... ameongelea hili. Japo hakuniridhisha
 
In 3 clubs that have employed me in South Africa when they were relegation candidates with no hope in hell of surviving I’ve done it saved the status and made the fans happy. Thank you to all my technical team we did it together at TTM for putting back my faith in assistants.

Dylan ker May 2021
 
Back
Top Bottom