Ali Kamwe: Kocha wa APR anatakiwa kuomba msamaha hadharani

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,860
24,340
Kocha wa APR aombe radhi

"Mapinduzi Cup ni Tournament Maalum yenye heshima kubwa hapa Afrika Mashariki na Kati.. Timu nyingi kubwa, Wachezaji wengi wakubwa wameshiriki.

Tunapaswa kuyalinda, kuyaheshimu kwa nguvu zetu zote.. Hata mtu anapotaka kuyaongelea ni Lazima ayaongelee kwa Nidhamu.. Isionekana mtu anakuja kushiriki kama 'msaada' tu kwa wenye mashindano.. Hii sio sawa Kabisa.

Mistake za waamuzi kwenye Football zinatokea mpaka World Cup.. Hata ujio wa VAR bado kuna makosa mengi ya waamuzi yametokea.

Inakuaje mtu mwenye Taaluma ya Ukocha anayakosea Heshima mashindano ya Mapinduzi kirahisi tu kwa sababu ya Waamuzi?

Video hapo juu (Ipo kwenye ukurasa wa Ally Kamwe Instagram) Timu yake ya APR ilipewa BAO LA MCHONGO dhidi ya JKU kutoka ZANZIBAR mbona hakusema Hatushiriki Tena kwa sababu Waamuzi wanatupendelea?

Wakikosea Waamuzi kwa wengine Meno yote Nje na kujiona bonge la Kocha.. Wanashangilia mpaka wanavua Nguo uwanjani.. Wakikosea wengine Mnasusa??

Sasa Kwa Tukio la Jana na Hilo hapo la mechi ya JKU Lipi lina upendeleo wa wazi kabisa??? Nafikiri Kocha wa APR anatakiwa KUOMBA MSAHAMA HADHARANI kwa kauli yake.

Mwenyekiti wa Wasemaji Afrika Ally Kamwe." Ameandika Kamwe.
 
Hoja yake ni ya msingi sana hata mimi nimemuelewa.

Ila asivuke mstari kwa kuwataka APR waombe radhi kwenye madai ambayo yamegusa ukweli.

Kwamba ni uongo kuwa swala la waamuzi haliwezi kuitia aibu soka la Tanzania?

Mwezi October Ally Kamwe alipewa adhabu na TFF kwa kumdhihaki mwamuzi Tatu Malogo.

Na hata humu minions wake walikuwa wanakejeli watu wengine kwa kutumia jina la Tatu Malogo.

Lini Ally Kamwe alijitokeza hadharani kumuomba radhi Tatu Malogo?
 
Aache upuuzi!, Kma mashindano yana heshima yake hiyo heshima ilipaswa ianze kuoneshwa kwa kuheshimu jasho la kila timu na sio kutengeza matokeo kwa timu wazipendazo.

APR waombwe msamaha kwakupotezewa muda na kudhulumia haki yao yakucheza fainal.
 
Kwani huyu bwana amekuwa msemaji wa APR hadi amsemee kocha wake?

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Huo uenyekiti ameupata kwny chama kipi?
Kutokana na sifa zifuatazo

1.kuwa ni mtu mwenye madini ( kumbuka alikuwa mchambuzi before)

2. Mtu mwenye fact

3. Haropoki ivyo

4,.si mtu mwenye mzaha ( kama Mr . Kispika)

Hivyo wasemaji wakampa uenyekiti
 
Aaah 3 malogo alizingua sana mkuu
 
Hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatu hatuombi msamaha.
Yeye na APR ndio wanatakiwa kuombwa msamaha kwa kudhulumiwa magoli waliyoshinda jana.
Basi hamtapewa mualiko tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…