Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Akina 'Fudenge' ndani ya Chadema na mustakabali wa Tanzania
Bila shaka wengi watapenda wajue haswaa 'Fidenge' ni nani? kabla ya kutegua kitendawili hicho nitajikita kuelezea vituko vya akina 'fudenge' na jinsi wanavyowaburuza wafuasi wao wanachadema wasijue la kufanya na kubaki na chuki dhidi ya Watanzania walio wengi.
Akina 'fudenge' walikuwa ni watu waliotaka mikataba yote ikiwamo ya madini na umeme ipitiwe upya bungeni na baadhi ilipendekezwa ifutiliwe mbali, ninakumbuka kwenye mjadala wa sakata la Escrow, Tundu Lissu akiongoza akina 'fudenge' walitoa msisitizo kuwa Seth wa IPTL anyang'anywe kampuni na itaifishwe mali ziingizwe Tanesco hapa pia mdau muhimu katika kundi la akina 'fudenge' ZZK mara kwa mara anamsisitiza raisi Magufuli kwa kuweka takwimu jinsi tunavyopata hasara kuwalipa IPTL na anasisitiza tutaifishe mali hizo. Siku serikali ikianza utekelezaji wa maazimio ya bunge kuhusu sakata la IPTL nina uhakika akina 'fudenge' wakiongozwa na akina Lissu, Zitto wataibuka wakipinga yale yote waliyoagiza yatekelezwe na serikali.
Miaka nenda rudi akina 'fudenge' walipata sifa lukuki za uzalendo kwa kuhoji 'kwanini tunasafirisha mchanga wa madini nje ya nchi?', 'nani anahakikisha kuwa ule ni mchanga na sio madini?' akina 'fudenge' walitoa hoja nzito zilizowaongezea imani kwa wananchi. kwenda mbali zaidi ilifika hatua akina 'fudenge' walipendekeza hata migozi bora itaifishwe au wasitishe uchimbaji ili vizazi vijavyo vije kunufaika' leo hadithi ni tofauti, Raisi Magufuli kachukua hatua ndogo tu ya kusitisha usafirishaji wa mchanga ili ukaguzi ufanyike, ileweke Hajataifisha mchanga wala migodi wala hajazuia uchimbaji' ni kufanya tu ukaguzi. Akina fudenge na wafuasi wao wameibuka mitandaoni huku wakitoa vitisho kuwa nchi itaingia vitani, itawekewa vikwazo ooohh zaidi kuna kundi la akina fudenge linafuatilia kauli za mabepari na kuzishangilia na wengine wanatamani isivuke leo bila nchi hii kupewa vikwazo hizi ni ramli za akina fudenge.
Ajizi nyumba ya njaa, mwezi April,2017 anayesadikiwa ni mmiliki wa akina fudenge aliwapokea wabunge toka kenya wenye asili ya kimasai nyumbani kwake huko Monduli, akawasisitiza 'Uhuru atosha' , hee kama utani vile akina fudenge wakaitisha mkutano wa baraza kuu huko Dodoma tukifikiri wana nia ya kujenga chama au kutoa mawazo mmbadala loh loh loh..Mkuu wa mafudenge akatangaza kuwa ''sisi akina fudenge msimamo wetu Uhuru atosha huko kenya'', akiba fudenge nao kama kawaida yao 'kuvuka mto mara'.....''Serengeti migration'' wamejawa na shauku wameshaanza kumtukana Odinga, wao sasa hivi akili yao ni 'kushinda uchaguzi mkuu wa Kenya' ati furaha yao ni Uhuru ashinde. Ikumbukwe akina fundenge pia walikuwa pamoja na Uhuru na Kenya kwenye mchakato wa kupata tenda ya kujenga bomba la mafuta, ni dhahiri akina fudenge wangefurahi zaidi bomba kupita Kenya japo ndio hivyo tena.
Mwisho, tatizo kubwa la akina fudenge ni kukosa msimamo na muendelezo na masuala na hoja (lack of consistency), wanasema adui mbaya ni yule mliye naye nyumba moja na kwa mienendo hii ya akina fudenge ni dhahiri sasa wamechukua nafasi ya kuwa ndio maadui namba moja wa Tanzania na watanzania.
Mungu ibariki Tanzania.