Morgan Fisherman
JF-Expert Member
- Dec 10, 2017
- 1,924
- 2,315
ni kweli sijaingia deep sana lakini mchango wako pia ni muhimu sana unaweza kutuelezea from your point of view.mkuu umeishia hapo hapo au unaemdelea?
Anyway ninachoweza kukuambia mpaka sasa ni kwamba bado hujaifikia vizuri kuisoma akili ya mwanadmu, umeishia kusoma maandiko ya larne ya 17 ya akina Rene Descarte, Freud Sigmund n.k
Ni sawa na safari ya kutoka Dodoma mpaka Dar wewe umeishia kongwa bado hujafika sehemu unayotakiwa kufika, bado hujaelewa maana ya akili
Nitafafanua vizuri
Hapo zamani wanasayansi walikuwa wanajiuliza je akili ni nini (what is Mind?), what is Memory, what is emotions? Je zinahifadhiwa vipi kwenye mwili wa binadamu? Na hupatikana sehemu gani?
Wanasayansi mbali mbali wakaanza kufanya uchunguzi na tafiti mbali mbali, akiwemo rene discarte na Freud Sigmund wakawa wanakuja na nadharia mbali mbali
Una nondo sema una ka uvivu kwenye uandishi...aidha device unayotumia sio rafiki kuandika makala ndefuMkuu kasone uje umalizie uzi wako au kama vipi niulize maswali nikueleweshe
pia rejea andiko la bwana PAVLOV kuhusu conditioned reflex action utaelewa vizuri hayo mambo ya subconcious na coinsciousness
😆😆😆😆Una nondo sema una ka uvivu kwenye uandishi...aidha device unayotumia sio rafiki kuandika makala ndefu
Eleza hapo namna ndoto inavyotokea maana kuna ndoto nyingine tunaota ni vituko.Baadae wakaanza kutafuta kuelewa mechanism ya jinsi kumbu kumbu zinavyohifadhiwa kwenye ubongo,
wataalam wa molecular biology
Neuroscience
psychology
Radiology
chemistry
computer science
wote hawa walihusika hadi kuja kuelewa jinsi kumbu kumbu zinavyohifadhiwa, pia ndoto zinavyotokea ukilala
Endelee kushusha nondo mkuu...Tuendelee,
Kamba kamba (neurons) zilizo ktk mpangilio maalum kwenye ubongo zinaunda kitu kinacho itwa circuit (kitu kama bala bala), yaani namaanisha hizo kamba kamba ukizipanga zikaunda uzi mrefu ndio circuit yenyewe.
kikawaida ubongo una mabilioni ya circuit (kamba kamba zilizojipanga kuunda kitu kama uzi), hizi circuit ukisema uzipange zote ziunde uzi mmoja basi zinaweza kufikia au kuzidi umbali wa kutoko duniani mpaka juani au mwezini.
jinsi kumbu kumbu zinavyohifadhiwa
Ukipita kwenye tope kisha ulaingia sebuleni kwenu ukanyoosha moja kwa moja hadi chumbani kwako, utaacha nyayo au alama sakafuni, hicho unachokiacha sakafuni kinaitwa kumbu kumbu, hivyo basi ukipita mara nyingi zaidi na tope lako mguuni alama za unyayo zitakuwa nyingi zaidi, zitatengeneza kumbu kumbu nzito au ya kudumu mpaka siku utakayo amua kusafisha au kupiga deki
Hivyo hivyo kwenye ubongo, kila tukio hupita kwenye circuit ktk mfumo wa umeme, mfano ukiambiwa huyu ni shangazi circuit moja itapitisha umeme na kurekodi tukio lote, ukiambiwa huyu ni Ronaldo circuit ya pili itapitisha umeme na kurekodi, hivyo basi taarifa hurekodiwa kwa mfumo huo, siku ukiulizwa Ronaldo anafananaje, utaanza kumuelezea jinsi alivyo au kumchora kabisa sababu ulisharekodi picha yake au video kwenye circuit ya ubongo wako,
Binadamu tuna mabilioni ya circuit huwezi kuyajaza yote kwa kurekodi taarifa au matukio.