Kabla ya kukujibu imebidi nipigwe na butwaa
Kwa kweli inatibika bila ya wasi muhimu kuswaki japo mara tatu kwa siku, kusugua ulimi hadi ndani kwa chini karibu na kolomelo, tena ajitahidi sana kuuzungusha mswaki kila kona ya mdomo kwa ndani, bila ya kusahau mashavuni, ikiwezekana kila baada ya mlo, asipokuwa karibu na mswaki, ajitahidi kusukutua mara kwa mara
Anaweza tumia mouthwash pia kabla au baada ya kuswaki, lakini akumbuke mouthwash haitomsaidia kwa kutwa nzima inaweza kusaidia kuzuia kaharufu kwa muda wa nusu saa baada ya hapo hali ya kawaida inarudi
Kama ujuavyo mdomo una bacteria wengi sana
Hebu jaribu haya machache halafu uje kutupa maendeleo yakoje
Kama hakuna mabadiliko inaweza kuwa hako kaharufu kanatokea tumboni hapo anahitaji kwenda kumuona daktari haraka iwezekanavyo