Ajira za Itilima-Simiyu

Brother James

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
233
Reaction score
172
Wana jamvi, naomba msaada wa kujibiwa maswali yafuatayo hapo chini:
UTANGULIZI:
Kijana wangu kapangwa ajira ya ualimu wa sekondari ktk Halmashauri ya Itilima, mkoa mpya wa SIMIYU, kwa uzalendo wa hali ya juu nimemshauri aende akafanye kazi kwani Tanzania ni yetu sote na ajira ni popote.
Nimemshauri hivyo angali sina hata ramani ya eneo husika, sasa basi weye unayeifahamu vizuri ITILIMA tafadhali msaada wako kwenye tuta ili tumshushe huyu kijana kwa kunijibu maswali hay;
1. Itilima ina shule ngapi? zitaje kwa majina please
2. Nimeambiwa kuna itilima town na rural, naomba utenganishe shule hizo za sekondari kwa kuzionyesha kuwa hizi ni za vijijini na hizi ni za pale mjini
3. Ni usafiri upi utampeleka moja kwa moja hadi itilima (nitajie na nauli zake pls) kama atapandia ubungo, ingawaje yeye yupo Tanga.
4. Vipi kuhusu changamoto za mahitaji ya muhimu (maji, malazi, mavazi, usafiri, chakula,utamaduni) ajipangeje-yeye ni binti
5. Mengineyo kama unaweza kuniongezea nitashukuru.
PAMOJA TUTAIJENGA NCHI YETU
 

Si useme tu ni wewe?? Kweli mzaz huna rafiki hadi ulete uzi hapa????
 
UJENZI, Imekuwa kasumba ya vijana wengi sana kutotaka kuonyesha kuwa wanafani gani na wanafanya kazi wapi lakini kwa umri wangu wa miaka 36 na elimu yangu hata kama ningekuwa naanza ajira sidhani kama ningethubutu kujificha kiasi hiki kwani mimi si mharifu wala sidaiwi na mtu. Naitwa James Jawawi, nafanya kazi katika chuo kikuu cha mandela (The Nelson Mandela African Institute of Science and Technology) kama Assistant Lecturer idara ya IT/Math, karibu sana.
Hadi nimeleta thread hii hapa JF ujue kweli ninashida ya kujibiwa hayo maswali, very seriously kwani anae kwenda huko ni ndugu yangu wa damu na si busara kumpakia ktk basi bila ya kumpa A,B,Cs za sehemu husika, kama una msaada wowote juu ya hili tafadhali tujuzane. Nina imani kuwa wenye ufahamu na hii sehemu watachangia hii thread.
MAWAZO
Si useme tu ni wewe?? Kweli mzaz huna rafiki hadi ulete uzi hapa????
 
Nadhani swali namba 3 ndo lamsingi kuliko yote,madam kashapata kazi ni bora aende tu mengine atayakuta hukohuko.
 
Jiandae na hali ngumu. Utashuka Bariadi mjini na utakamata gari zisizikuwa na uhakika kupitia Mahaha-Kilulu-Budalabujiga na kuibuka Lagangabilili makao makuu ya Itilima, hapo hakuna cha mji ni kijiji na hakina miundombinu ya kimjini uliyozoea. Kazi ni popote japo ni ngumu.
 
ha ha ha ha ha h, Mbishi 4 real, maadam umeona swali la msingi basi kabla hajasafiri naomba tumtafutie majibu ya hilo swali just pa kuanzia tu.
Nadhani swali namba 3 ndo lamsingi kuliko yote,madam kashapata kazi ni bora aende tu mengine atayakuta hukohuko.
 
Uliza_Bei, nashukuru kwa muongozo wako mzuri, vipi kuhusu nauli yake kama ataanzia safari yake Ubungo hadi Bariadi then Itilima??, na kama hapo lagangabilili hakuna miundombinu ya kiofisi, ofisi za Halmashauri ya ITILIMA zipo sehemu gani?? kama hutojali ni-PM contacts zako ili niku-call kwa ajili ya maelezo zaidi pls!!!!
 
Hilo ni eneo jipya ambalo lilikuwa kata tu. Hakuna ofisi za maana lakini inaelekea matajiri wameomba ubia waweke ofisi na nyumba za watumishi kwa baadaye. Nauli siyo kubwa usiogope kuna Bus kama Simiyu zinakwenda hadi Bariadi siku moja kwa bei ya 35 hadi 50 elfu. Pumzika Shinyanga/Mwanza au Bariadi ndiyo uanze safari ya Itilima hakuna haraka. Ukipenda Toka Bariadi chukua pikipiki tu kama mvua siyo nyingi uende kwa raha kidogo
 
Nakushukuru sana kwa maelezo mazuri ndugu yangu Uliza_Bei
 
Hamana kitu kinachoitwa ITILIMa mjini itilima yote ni chaka tu..... labada kidogo shule moja inaitwa ITILIMA SEC SCHOOL ndio ipo njiani,rahisi kwenda SIMIYU MJINI nauli 1000 kwa basi
 
Hamana kitu kinachoitwa ITILIMa mjini itilima yote ni chaka tu..... labada kidogo shule moja inaitwa ITILIMA SEC SCHOOL ndio ipo njiani,rahisi kwenda SIMIYU MJINI nauli 1000 kwa basi
si ningeshangaa japo nimetoka huko miaka mingi,itilima nilikua najua ni kijiji tu,kumbe wameendelea imeshakua wilaya ndani ya miaka 10 tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…