Ajira ya muda katika Jamii Media - Afisa Mawasiliano (9)

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,813
1,523
TANGAZO LA AJIRA YA MUDA - AFISA MAWASILIANO (9)

1. UTANGULIZI

Jamii Media ni Kampuni gwiji inayojishughulisha na taarifa na habari kwa kupitia Mitandao ya Kijamii. Kampuni hii inachochea Uhuru wa Kujieleza, Uwazi katika Utawala, na Uwajibikaji kupitia Mtandao wao maarufu uitwao JammiForums.com.

Jamii Media pia inamiliki na kuendesha jarida-mtandao liitwalo FikraPevu.com na kusimamia kurasa zenye wasomaji wengi kwenye mitandao ya Kijamii kama Twitter, Facebook na Instagram.

2. CHIMBUKO

Jamii Media inatarajia kuanza utekelezaji wa Mradi utakaofahamika kama “TUSHIRIKISHANE PROJECT” Lengo la Mradi huu ni kuwawezesha wananchi na kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi, wawakilishi wa kuchaguliwa (hususani Wabunge) na Uongozi wa Wilaya.

Tushirikishane utakuwa Mradi wa miezi kumi na miwili utaotekelezwa kwenye Majimbo tisa (9), ya Uchaguzi na utashirikisha Wabunge tisa (9), Madiwani wa kata katika Majimbo husika, watumishi wa Halmashauri katika majimbo husika na wananchi wa maeneo utakapotekelezwa mradi huu.

Lengo mahsusi la kuhamasisha ushirikiano kati ya wadau wakuu wa mradi huu ni kuharakisha/kurahisisha utekelezwaji wa ahadi za viongozi wa kuchaguliwa, kuchochea ufanisi wa Serikali Wilayani katika kutoa huduma za jamii hususani kwenye Sekta za afya, maji, elimu na mioundombinu. Na mwisho, kuweka mfumo wa kuongeza msukumo wa uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.

Ili kufikia azma hii, ni muhimu wananchi kuwa na uelewa juu ya rasilimali zilizopangwa kwa ajili ya maeneo yao, lazima wajue mipango ya Serikali kwenye ngazi ya Wilaya zao. Uelewa huu unapatikana kwa wananchi kuwa na fursa ya kupata taarifa tena zikiwa katika mfumo ambao ni rahisi kueleweka.

Kwa bahati mbaya kwa sasa taarifa nyingi zinazowagusa wananchi hazipatikani kirahisi na haziko katika mfumo rahisi wa kueleweka na wengi. Jambo hili linalotoa nafasi kwa baadhi ya watu kutumia taarifa kwa manuaa binafsi ikiwemo kuwahada wananchi wakati wa kuomba uongozi. Mradi wa Tushirikishane ungependa kuziba mwanya huu kwa kuhakikisha wakati wote wananchi wanapata taarifa kwa wakati na katika jinsi ambayo zinaeleweka kwa urahisi.

Ili kutekeleza mradi huu kwa ufanisi, Jamii Media imetengeneza nafasi za AFISA MAWASILIANO kwa kila Jimbo litakaloshiriki kwenye Mradi. Maombi yanakaribishwa kutoka kwa watu wenye vigezo wanaoishi kwenye majimbo yafuatayo:
1. Bunda
2. Arumeru Mashariki
3. Amani, Zanzibar
4. Bukoba mjini
5. Kigoma mjini
6. Kigamboni
7. Lindi
8. Nzega

9. Sengerema
10. Lindi (Imeongezwa leo tarehe 5, Julai)

3. VIGEZO VYA MUOMBAJI

- Awe mkazi aliyeshiriki kupiga kura kwenye Jimbo analoomba kuwakilisha na maskani yake ya sasa iwe Jimboni.
- Awe na taarifa za kina kuhusu ahadi za wagombea wa nafasi za ubunge kutoka uchaguzi uliopita na asiwe na upendeleo
- Awe na uwezo wa kuchambua mambo na taarifa pasipo kuathiriwa na itikadi, mapenzi binafsi au upendeleo wa aina yoyote
- Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na ajue kukusanya habari, kuandika taarifa na kufuatilia majibu ya malalamiko au maoni ya wananchi kwa viongozi wa umma.
- Awe mtumiaji mzuri wa mawasiliano ya kisasa hasa mitandao ya kijamii. Na awe mshiriki hai wa mijadala mbalimbali inayogusa jamii.

- Muombaji aliyejisajili na kuchangia mijadala mbalimbali ya JF kwa muda zaidi ya miezi sita ana nafasi pekee

4. JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Watu wote wanaohisi wanakidhi vigezo vilivyorodheshwa hapo juu watume maombi yao kwa njia ya barua-pepe wakijibu maswali yafuatayo:

· Jina lako kamili, anwani yako na
· Ahadi gani zilitolewa na Mbunge wako wa sasa? Taja walau tatu
· Hali ya huduma za kijamii ikoje katika Jimbo unalotaka kuwakilisha?
· Vipaumbele vya Serikali katika Wilaya yako ni vipi?

Majibu yatumwe kwenda vacancies@jamiiforums.com na kwenye kichwa cha habari andika JINA LA JIMBO unalotaka kuwakilisha likifuatiwa na neno AFISA MAWASILIANO. Mfano: UBUNGO—AFISA MAWASILIANO.

Kazi hii itakuwa ya mkataba wa miezi minane (8) kuanzia Julai, 2016 na itamhitaji mhusika kuzunguka katika kata mbaimbali za Jimbo kukusanya taarifa na matukio.

Mwisho wa kutuma maombi na Juni 28, 2016.
 
[QUOTE="Jamii Jobs, post: 16528734,

3. VIGEZO VYA MUOMBAJI
[/SIZE][/FONT]
· Awe mkazi aliyeshiriki kupiga kura kwenye Jimbo analoomba kuwakilisha na maskani yake ya sasa iwe Jimboni.

A. Je km ni mkazi wa Jimbo husika na hakushiriki kupiga kura ktk hilo jmbo anaruhusiwa kuomba kazi?
Kuna watu kipindi cha uchaguzi walikuwa majimboni kwao na walifuatilia mchakato mzma wa uchaguzi lakini hawakupga kura kwa sababu hawakujiandikisha hapo.

B. Je km ni mkazi wa mojawapo wa jimbo lililotajwa na kwa sasa yupo nje ya jimbo hilo anaruhusiwa kuomba? Maana mwingne anaweza kurudi jimboni kwao kwa ajili ya kazi hyo. (Nmezingatia issue ya interview.)

Nitashukuru nikijibiwa hayo maswali.
 
Daaaaah nimepishana na fuko la hela,na hii ningefit sana aiseee.
 
Maskini jimbo langu la Nyamagana halipo! Ahadi za mbunge wetu ningezifanyia kazi na naamini ningeshirikiana naye vizuri, mwenyekiti wangu wa mtaa na diwani wangu wa Igoma tungeonesha mfano.

Ila si bure kuna kitu nimejfunza toka kwenye tangazo hili... nalo ni "WANANCHI KUTOPATA TAARIFA MUHIMU ZA JIMBO / KATA YAO"
 
nashukuru kwa hilo mimi nauliza swali tu la kijinga..

ni vigezo gani mmetumia kuchagua hayo majimbo?

na je vipi kuhusu majimbo mengine ?

je nikitaka kujitolea kuwapa info za Jimbo langu ambalo halijatajwa hapo inawezekana?
 
Kazi kwenu vijana nshindwe nyinyi ukada weka pembeni Toa info..za uhakika mfuko unenepe JF ishaanza kuwasaidia vijana wanaohangaika na ajira kuanzia form IV hadi mwenye elimu kama ya Lipumba
 
Kazi kwenu vijana nshindwe nyinyi ukada weka pembeni Toa info..za uhakika mfuko unenepe JF ishaanza kuwasaidia vijana wanaohangaika na ajira kuanzia form IV hadi mwenye elimu kama ya Lipumba
Asante kakake.
 
A. Je km ni mkazi wa Jimbo husika na hakushiriki kupiga kura ktk hilo jmbo anaruhusiwa kuomba kazi?
Kuna watu kipindi cha uchaguzi walikuwa majimboni kwao na walifuatilia mchakato mzma wa uchaguzi lakini hawakupga kura kwa sababu hawakujiandikisha hapo.

Nafasi hizi zinamuhitaji muombaji awe ni mkazi wa Jimbo aliyeshiriki mchakato wa uchaguzi ikiwemo kupiga kura. Hii ni mahususi kuhakikisha kwamba muwakilishi ana ufahamu wa kutosha juu ya wagombea na ahadi walizotoa. Na lazima maskani yake ya sasa iwe katika hilo hilo Jimbo aliloshiriki ili aweze kuunganisha vema ahadi na hali halisi ya utekelezaji. Suala la msingi hapa ni kushiriki mchakato wa uchaguzi na kuwa na maskani Jimboni.

Kutokupiga kura kwa aliyejiandikisha si tatizo kubwa.

B. Je km ni mkazi wa mojawapo wa jimbo lililotajwa na kwa sasa yupo nje ya jimbo hilo anaruhusiwa kuomba? Maana mwingne anaweza kurudi jimboni kwao kwa ajili ya kazi hyo. (Nmezingatia issue ya interview.)

Nitashukuru nikijibiwa hayo maswali.

Hapana Mkuu. Nafasi hizi zinamhitaji mkazi wa Jimbo mwenye utengamano wa kila siku na Jamii ya eneo husika. Mtu wa kuja na kuondoka atashindwa kuunganisha vizuri mawasiliano kati ya mradi, wananchi, na viongozi.
 
Nafasi hizi zinamuhitaji muombaji awe ni mkazi wa Jimbo aliyeshiriki mchakato wa uchaguzi ikiwemo kupiga kura. Hii ni mahususi kuhakikisha kwamba muwakilishi ana ufahamu wa kutosha juu ya wagombea na ahadi walizotoa. Na lazima maskani yake ya sasa iwe katika hilo hilo Jimbo aliloshiriki ili aweze kuunganisha vema ahadi na hali halisi ya utekelezaji. Suala la msingi hapa ni kushiriki mchakato wa uchaguzi na kuwa na maskani Jimboni.

Kutokupiga kura kwa aliyejiandikisha si tatizo kubwa.
Nmeuliza hilo swali mahususi maana niko interested na hiyo kazi. Jimbo langu ni mojawapo kati ya majimbo yaliyotajwa japo kwa sasa nipo nje ya hilo jimbo. Lakini naweza kurudi kufanya kazi hiyo jimboni kwangu. Ninalifaham vzur jimbo langu na ninafaham ahad za wagombea maana kipnd cha kampeini nilkuwa jimboni na nilishiriki vyema japo sikupga kura na sababu ilkuwa kujiandikisha nje ya jimbo langu.
Nadhan nmeeleweka. Je, naruhusiwa kuomba hyo kazi? Natanguliza shukran
 
Awali ya yote ifahamike kuwa hii ni 'Pilot'. Tukifanikiwa katika hatua hii, basi tutapanua wigo na kufanya kwa majimbo mengi zaidi. Kupata majimbo ya awali tumeangalia vigezo vingi ikiwemo: Utayari wa Mbunge na Jimbo tajwa na Wilaya yake kutoa ushirikiano katika kutekeleza mradiWepesi wa Mbunge kushiriki mijadala na kutoa ushirikiano kwenye mitandao ya KijamiiUrari wa vyama na jinsia za washiriki

nashukuru kwa hilo mimi nauliza swali tu la kijinga..

ni vigezo gani mmetumia kuchagua hayo majimbo?

na je vipi kuhusu majimbo mengine ?

je nikitaka kujitolea kuwapa info za Jimbo langu ambalo halijatajwa hapo inawezekana?
 
Mkuu Black Fire,

Unaruhusiwa kuomba kazi hii. Zaidi yanaweza kuongelewa katika usahili.

Back
Top Bottom