Ajira veta

john kebu

Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
19
Reaction score
7
Mnamo tarehe 25/8/2017 siku ya ijumaa,VETA walitoa shortlist ya watu kwa ajili ya kufanya interview siku ya tarehe 4/9/2017 katika kada mbalimbali zikiwemo Bursar,Accountants,Database Administrator,Network Administrator,ICT teachers na Computer Application Teachers.

Ile attachment ya shortlisted candidates imekaa ijumaa hadi jumapili cha kushangaza leo jumatatu tarehe 28/8/2017 nimeingia kwenye website yao nimekuta document imebadilishwa,candidates wamebadilishiwa nafasi walizo pangiwa na wamewekwa kwenye nafasi zingine kabisa.

Sasa huu ni uhuni hapo naanza kupata picha tofauti kabisa na nafikiri tayari wameshaanza kupanga matokeo yao,inawezekana kuna watu waliwapangia kwenye kada ambazo wanajua hawawezi kupata.

Naatach document zote mbili ile ya tarehe 25/8/2017 na tarehe 28/8/2017 yaani leo kwa ushahidi zaidi ili muone,lakini pia naomba waziri husika wa ajira aingilie kati hili suala kwasababu ninaona kabisa watanzania wenye sifa wanataka kuonewa kwenye hili na kukosa haki yao ya kimsingi.

Ndimi muonewa:
 

Attachments

Mkuu njoo tulime matikiti kibiti huku,

from Katesh using Siemens C55
 
usimlaumu mtu hapo.....hapewi mtu kitu pasipo kuwa na mtu anaye mjua.....inawezekana hapo uliomba na umekosa wa kukushika mkono ili uambulie japo nafasi moja...pole sana....nakuombea kwa Mungu akupunguzie jaziba kisha jaribu nafasi nyingine unaweza ukapata.
 
mkuu nilishakua shortilisted tayari kwa document ya kwanza leo naingia nakuta sipo asee kwenye ile position,dah ina discourage sana asee.PCCB Mko wapi mnyooshe hawa watu
 
Kweli bwana..
Mkuu asa inakuaje kwa mtu ambae aliona ile ijumaa au jumamosi?sababu siyo watu wote wanatembelea kwenye site ya veta kila siku.Inamana wale watu wamebak na wazo la ijumaa hiyo siku ya interview wakifika wataanza kubung'aa macho,alafu kama kweli hawataki kufanya vigisu why not hawajatangaza kama kuna mabadiliko wameweka kimyakimya tu
 
Ukiona hivo ujue walkua hawajapanga vema timu ya ushindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…