Ajira Kwanza Vs Elimu Kwanza!

Ajira Kwanza Vs Elimu Kwanza!

HKigwangalla

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2008
Posts
722
Reaction score
971
Ajira Kwanza Vs Elimu Kwanza...

Mwaka 1994, Bwana Tony Blair alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani Bungeni. Mwaka 1997 alikiwezesha chama chake kushinda nafasi ya uwaziri mkuu, na yeye akawa waziri mkuu. Aliweka kipaumbele cha kwanza, elimu, cha pili, elimu na cha tatu elimu. Mhe. Edward Lowassa jana ameeleza kuwa #AjiraKwanza siyo muhimu, na badala yake #ElimuKwanza ndiyo. Mjadala wa ajenda ndiyo haswa unahitajika kwenye majukwaa ya siasa zetu katika zama hizi. Sikubaliani naye kabisa. Nikiamini mfano anaoiga haukai kwenye ulinganifu sawia, sababu, Uingereza ya mwaka 1997, Mei, Bw. Blair alipoingia madarakani ni tofauti sana na Tanzania ya 2015. Uingereza ya Bwana Blair haikuwa na changamoto ya usalama wa chakula, changamoto ya ajira na wala changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi na ukosefu wa mvua kama Tanzania yetu ya 2015. Pamoja na kuthamini elimu na ukombozi wote unaokuja nayo, bado tu ukweli utabakia kwamba mtu hauwezi kupeleka shule mtoto mwenye njaa! Ama hauwezi kulipa ada ya shule wakati nyumbani hauna uhakika wa chakula.

Msingi wa pendekezo la kipaumbele changu cha #AjiraKwanza ni kwamba, kwa vyovyote vile ni lazima tupambane kuondoa umaskini na kukuza uchumi kwa malengo ya kuzalisha ajira za kutosha. Na ili tufikie malengo yetu kwa haraka, ajira tunazotakiwa kuzalisha zinapaswa zitokane na kilimo, viwanda vidogo vidogo vyenye linkage na kilimo na kuimarisha masoko ya bidhaa za shambani na za viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo. Tukifanya haya tutaajiri watu wengi zaidi, tutajihakikishia uhakika wa chakula, tukikuza biashara ya ndani tutakusanya kodi kwa watu wengi zaidi na uchumi ukiimarika ndipo sasa tutaweza kuboresha huduma za elimu, afya na maji kwa uhakika zaidi, tutakuza uchumi kwa haraka zaidi na uchumi utawagusa watu wengi kwa mara moja, tutapunguza uagizaji wa bidhaa toka nje - zaidi ya yote haya, hili ni wazo linalotekelezeka!
 
Kigwangala sema yakwako bila kumtaja mgombea mwenzako! Ongea utatufanyia nini na hizo sera au maono uliyonayo. Hapa utasababisha mjadala uwe wa Lowasa badala ya kuwa wa sera zako!
Jiongelee wewe na sera zako
 
Ni kweli ajira kwanza au unalenga tu kupata kura za vijana?

Hivi mbona mnapokuwa Bungeni hamuonyeshi hii concern yenu kwa watanzania zaidi ya kusema ndio tu kwa kila kitu?!
 
Nakuomba Utowe Sera Zako Siku Zote Ata Ukuwa Unamtongoza Mwanamke Ukimponda Mwanaume Mwenzako Umempatiya Yule Mwanya Wa Kukubalika Ni Sawa Na Wewe Unapo Ponda Sera Ya Lowassa Auwezi Kupata Ajira Bila Elimu, Auwezi Kupata Wataalamu Bora Tz Bila Kuwapatiya Elimu Bora, Tz Ipo Nyuma Sana Ktk Soko La Ajira Tatizo Elimu Finyo, Na Hitimisha Nakubali Maneno Ya Mwisho Ya Lowassa Ktk Kutangaza Niya Yake Ktk #Safari #ya#matumaini Namnukuu Alisema Auwezi Kupinganiya Umasikini Japo Nawe Ni Masikini Lazima Ukipata Urais Utaiji Kurudisha Fedha Za Walipa Kodi Tanzania Pia Amekusudia Kuondowa Umasikin Ktk Nchi Yetu, Michezo, Kuinuwa Uchumi, Na Pamoja Na Elimu, Tatizo La Lowassa Ameficha Kuzungumzia Richmond Tu
 
Ajira Kwanza Vs Elimu Kwanza...Mwaka 1994, Bwana Tony Blair alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani Bungeni. Mwaka 1997 alikiwezesha chama chake kushinda nafasi ya uwaziri mkuu, na yeye akawa waziri mkuu. Aliweka kipaumbele cha kwanza, elimu, cha pili, elimu na cha tatu elimu. Mhe. Edward Lowassa jana ameeleza kuwa #AjiraKwanza siyo muhimu, na badala yake #ElimuKwanza ndiyo. Mjadala wa ajenda ndiyo haswa unahitajika kwenye majukwaa ya siasa zetu katika zama hizi. Sikubaliani naye kabisa. Nikiamini mfano anaoiga haukai kwenye ulinganifu sawia, sababu, Uingereza ya mwaka 1997, Mei, Bw. Blair alipoingia madarakani ni tofauti sana na Tanzania ya 2015. Uingereza ya Bwana Blair haikuwa na changamoto ya usalama wa chakula, changamoto ya ajira na wala changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi na ukosefu wa mvua kama Tanzania yetu ya 2015. Pamoja na kuthamini elimu na ukombozi wote unaokuja nayo, bado tu ukweli utabakia kwamba mtu hauwezi kupeleka shule mtoto mwenye njaa! Ama hauwezi kulipa ada ya shule wakati nyumbani hauna uhakika wa chakula. Msingi wa pendekezo la kipaumbele changu cha #AjiraKwanza ni kwamba, kwa vyovyote vile ni lazima tupambane kuondoa umaskini na kukuza uchumi kwa malengo ya kuzalisha ajira za kutosha. Na ili tufikie malengo yetu kwa haraka, ajira tunazotakiwa kuzalisha zinapaswa zitokane na kilimo, viwanda vidogo vidogo vyenye linkage na kilimo na kuimarisha masoko ya bidhaa za shambani na za viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo. Tukifanya haya tutaajiri watu wengi zaidi, tutajihakikishia uhakika wa chakula, tukikuza biashara ya ndani tutakusanya kodi kwa watu wengi zaidi na uchumi ukiimarika ndipo sasa tutaweza kuboresha huduma za elimu, afya na maji kwa uhakika zaidi, tutakuza uchumi kwa haraka zaidi na uchumi utawagusa watu wengi kwa mara moja, tutapunguza uagizaji wa bidhaa toka nje - zaidi ya yote haya, hili ni wazo linalotekelezeka!
Mbona misemo ya kijinga imewajaa sana....kutwa mna quote watu ktk nchi zenye fikra na maadili tofauti na nyie?Sasa mmeacha ku quote kwa wajamaa wenzenu?Hembu muache tutia kichefuchefu bhana...CCM ni wepesi kupandisha mizuka ktk vitu vya hovyo.Elimu Elimu na ambilioni ya Lowasa masaia wanasomeshwa kwa hela za misaada ya wazungu na makanisa hadi leo?Ujamaa ni laana..wajamaa wote huwa hawajui wanachosema,wanachoamini wanapotoka au wanapokwenda..huwa ni wadandia hoja .Kwa vile ubunifu wao umeishia kuangalia magharibi na kutafuta cha kupinga kwa mdomo na sheria kwa wengine ,ila wao kiutendaji wanayataka maisha ya kimagahribi bila jasho.
 
Mtu akupata elimu anaweza kutengeneza ajira. So elimu 1stly coz u would got better oppottunities bcoz of that.
 
Nyie wanasiasa mnachekesha sana. There's no such a thing like Ajira Kwanza, Elimu Baadae. Every element in any system has direct impact to each other. Stop these gimmicks. What happens to Kilimo Kwanza? How successful was that one?
 
Ajira Kwanza Vs Elimu Kwanza...

Mwaka 1994, Bwana Tony Blair alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani Bungeni. Mwaka 1997 alikiwezesha chama chake kushinda nafasi ya uwaziri mkuu, na yeye akawa waziri mkuu. Aliweka kipaumbele cha kwanza, elimu, cha pili, elimu na cha tatu elimu. Mhe. Edward Lowassa jana ameeleza kuwa #AjiraKwanza siyo muhimu, na badala yake #ElimuKwanza ndiyo. Mjadala wa ajenda ndiyo haswa unahitajika kwenye majukwaa ya siasa zetu katika zama hizi. Sikubaliani naye kabisa. Nikiamini mfano anaoiga haukai kwenye ulinganifu sawia, sababu, Uingereza ya mwaka 1997, Mei, Bw. Blair alipoingia madarakani ni tofauti sana na Tanzania ya 2015. Uingereza ya Bwana Blair haikuwa na changamoto ya usalama wa chakula, changamoto ya ajira na wala changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi na ukosefu wa mvua kama Tanzania yetu ya 2015. Pamoja na kuthamini elimu na ukombozi wote unaokuja nayo, bado tu ukweli utabakia kwamba mtu hauwezi kupeleka shule mtoto mwenye njaa! Ama hauwezi kulipa ada ya shule wakati nyumbani hauna uhakika wa chakula.

Msingi wa pendekezo la kipaumbele changu cha #AjiraKwanza ni kwamba, kwa vyovyote vile ni lazima tupambane kuondoa umaskini na kukuza uchumi kwa malengo ya kuzalisha ajira za kutosha. Na ili tufikie malengo yetu kwa haraka, ajira tunazotakiwa kuzalisha zinapaswa zitokane na kilimo, viwanda vidogo vidogo vyenye linkage na kilimo na kuimarisha masoko ya bidhaa za shambani na za viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo. Tukifanya haya tutaajiri watu wengi zaidi, tutajihakikishia uhakika wa chakula, tukikuza biashara ya ndani tutakusanya kodi kwa watu wengi zaidi na uchumi ukiimarika ndipo sasa tutaweza kuboresha huduma za elimu, afya na maji kwa uhakika zaidi, tutakuza uchumi kwa haraka zaidi na uchumi utawagusa watu wengi kwa mara moja, tutapunguza uagizaji wa bidhaa toka nje - zaidi ya yote haya, hili ni wazo linalotekelezeka!

Ongea ni nini utaifanyia nchi, na si kutafuta umaarufu kwa mgongo wa mgombea mwingine. #kampenidhaifu
 
una ajiri vipi watu wasiokuwa na elimu?
NI nchi imetushinda tuu si kila mtu lazim awe na elimu ili maisha yawe mazuri, hata hayo maccm yaliyosoma hayajaweza jikomboa hata pale yalipoiba hela nyingi.Yamekuwa na elimu na hela ila bado maisha kwao ni magumu achilia mbali ymekuwa ni tatizo kwa wengine waliokosa hivyo vitu.
 
Ongea ni nini utaifanyia nchi, na si kutafuta umaarufu kwa mgongo wa mgombea mwingine. #kampenidhaifu
Sasa km wao wana elimu na hela walizotuibia ila bado wamebaki kuwa tatizo ktk majimbo yao?Elimu wanayoiongelea ni ipi?Huyu Jamaa na wenzie naona wamegraduate ktk kuwapa shida watu ktk majimbo yao sasa wanataka eneza shida kwa watanzania.
 
samahan kama nitakukwaza kama mch.Peter Msigwa. Wewe kama doctor na mbunge,je uliajiriwa kwanza ndio ukaupata udoctor na ubunge ama ulipata kwanza elimu ndio ikakupa ajira na ubunge?kwa mfumo wa elimu tulio nao wa kufuta masomo ya kilimo shulen na kuyarudsha kwa baadhi ya shule,kukosa mtahala wa elimu unaoeleweka,kufuta ada elf 20 na kuruhusu michango mingine zaidi ya lak 1,migomo ya walimu na hali zao duni,aliefeli mitihani ndio anaepewa nafas kubwa ya kuwa mwalimu,wanafunzi kukosa madawati vtabu, chaki,vifaa vya sayansi na walimu wa sayansi,kusomea chini mti,shule yenyd wanafunz zaid ya 100 kua na mwalimu mmoja,Utapata wapi wataalamu wa kilimo cha kisasa chenye tija? Utapata wap wataalamu wa kuendesha viwanda vidogo vidogo?kwa mfumo huu wa elimu wako wap wataoweza kujiajiri kwa viwanda na kilimo? Kwa elimu hii,wangapi wanaweza kufanya biashara za kimataifa(kuuza bidhaa nje ya nchi).Samahan tena,naamini udoctor wako sio ule alieusema mh.Peter Msigwa,na naamini doctor ni mtu wa kufanya TAFITI SANA TENA ZA KIN
 
Bw. Kingwangala, nilidhani kwa wewe ni moja wa wanaotarajia kutangaza nia haukustahili kuanza kujadili ya wenzako kabla wewe haujatangaza yako. Aidha, uchambuzi wako unakosa mashiko kwa kiwango kikubwa. Huenda ukawa una hoja ila unavyoiweka inaonyesha kabisa haujaitafakari kwa undani ili kuona utofauti wa anachokisema Lowasa na unachodhania. Pamoja na kuwa Lowasa hakusema kuwa Serikali yake itaweka nguzvu zote kwenye elimu as an isolation agenda, uhalisia unabakia kuwa ni kweli kuwa elimu inauwezo mkubwa wa kukomboa kila mtanzania kwa nafasi yake kwa wakati huu ambao tunazidi kufungua mipaka yetu. Kumbuka industrilization is not an overnight project its a process ambayo inahitaji nguvu kazi yenye uelewa wa ngazi zote. Ni vyema ukaeleza vyema unafikiaje uchumi wa vinwanda na kutengeneza ajira katika taifa ambalo halina wasomi. Asilimi 70 ya WTZ wapo vijinini wanategemea kilimo shule watoto wao wakijitahidi sana wanaendelea kwenda Sekondari ni asilimia ndogo sana na mwisho wa asilimia zaidi ya 90 wanaishia form four division 4 au 0, je hao ndio unaofikiria kuwajengea viwanda. No, tunahitaji an integrated system elimu ikiwa ndiyo core ili kuwa na multiplier impact kubwa kwa matawi ya mfumo wa kujitegemea in an inclusive way. Wewe ni shahidi umeona namna ambavyo watanzania wa jimbo lako wanavyoonewa katika migodi kwa kulipwa kidogo, au kufukuzwa katika mashimo ambayo yameonekana kuwa na rasilimali. Hawa unataka kuwapeleka kwenye uchumi wa viwanda wakiwa hivyo. Tunahitaji Elimu as central element ya kuwakomboa watanzania katika kujitambua na kutambua utajiri walionao na kuwaandaa kwenda katika uchumi wa viwanda na kipato cha kati. Kwa hiyo Mhe. endapo unatarajia kuntangaza nia badilisha speech yako iwe na mshiko na ionyeshe kweli uanelewa Tanzania ya sasa inahitaji nini. Sisemi Lowasa alichosema kuwa anamaanisha ila kwa kulenga ELIMU KAMA CORE ELEMENT YA UKOMBOZI nakubaliana naye. Dhamira ya nia ya dhati na namna anavyotarajia kufanya bado hatujaelewa.
Ajira Kwanza Vs Elimu Kwanza...

Mwaka 1994, Bwana Tony Blair alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani Bungeni. Mwaka 1997 alikiwezesha chama chake kushinda nafasi ya uwaziri mkuu, na yeye akawa waziri mkuu. Aliweka kipaumbele cha kwanza, elimu, cha pili, elimu na cha tatu elimu. Mhe. Edward Lowassa jana ameeleza kuwa #AjiraKwanza siyo muhimu, na badala yake #ElimuKwanza ndiyo. Mjadala wa ajenda ndiyo haswa unahitajika kwenye majukwaa ya siasa zetu katika zama hizi. Sikubaliani naye kabisa. Nikiamini mfano anaoiga haukai kwenye ulinganifu sawia, sababu, Uingereza ya mwaka 1997, Mei, Bw. Blair alipoingia madarakani ni tofauti sana na Tanzania ya 2015. Uingereza ya Bwana Blair haikuwa na changamoto ya usalama wa chakula, changamoto ya ajira na wala changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi na ukosefu wa mvua kama Tanzania yetu ya 2015. Pamoja na kuthamini elimu na ukombozi wote unaokuja nayo, bado tu ukweli utabakia kwamba mtu hauwezi kupeleka shule mtoto mwenye njaa! Ama hauwezi kulipa ada ya shule wakati nyumbani hauna uhakika wa chakula.

Msingi wa pendekezo la kipaumbele changu cha #AjiraKwanza ni kwamba, kwa vyovyote vile ni lazima tupambane kuondoa umaskini na kukuza uchumi kwa malengo ya kuzalisha ajira za kutosha. Na ili tufikie malengo yetu kwa haraka, ajira tunazotakiwa kuzalisha zinapaswa zitokane na kilimo, viwanda vidogo vidogo vyenye linkage na kilimo na kuimarisha masoko ya bidhaa za shambani na za viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo. Tukifanya haya tutaajiri watu wengi zaidi, tutajihakikishia uhakika wa chakula, tukikuza biashara ya ndani tutakusanya kodi kwa watu wengi zaidi na uchumi ukiimarika ndipo sasa tutaweza kuboresha huduma za elimu, afya na maji kwa uhakika zaidi, tutakuza uchumi kwa haraka zaidi na uchumi utawagusa watu wengi kwa mara moja, tutapunguza uagizaji wa bidhaa toka nje - zaidi ya yote haya, hili ni wazo linalotekelezeka!
 
NAAMINI KUA DOCTOR NI MTU ANAYEFANYA TAFITI SANA TENA ZA KINA(kiufupi ni mwenye data sahihi),JE,UNATAKA KUTUAMINISHA WATANZANIA KUA KWA TAFITI ULIZOFANYA KAMA MSOMI UMEGUNDUA KUA AJIRA NI BORA KULIKO ELIMU KWA SASA?sisi watanzania tumepata fursa mbil kwa pamoja,na tunatakiwa tuchague moja(yaani wewe ndugu AJIRA KWANZA,na LOWASA ndugu ELIMU KWANZA).mfano,wewe kama mzaz mshauri,una mwanao ama nduguyo amepata fursa hizo,yaan apewe ajira ama apewe elimu,Ungemshauri achague kipi ambacho kitamsaidia ktk maisha yake hasa ya baadae kwamaana ya kutimiza ndoto zake? NITARIDHIKA KAMA NITAJIBIWA MASWALI MADOGO NLIYOKUULIZA KAMA MPIGA KURA MTARAJIWA INGAWA BADO BVR HAIJANIFIKIA.
 
Huyu jamaa anatumia nguvu kubwa Sana kutaka kuwin watu.Kaka soma alama za nyakati,ni heri ungetumia nguvu hii kwenye biashara zako.Watu watapataje Ajira bila kusoma,au ndio mpango wa kuwafanya Watz vibarua kwenye biashara zenu?
 
...hueleweki hata kidogo, unaleta ushindani wa mijadala ya shule za upili (fedha ni bora kuliko elimu). Wewe ni mgombea jisimamie mwenyewe masuala ya kusubiri mtia nia mwenzako aseme ndo na wewe unadandia hapo aliposema ni kukosa maarifa na hakuna shaka huna unachoweza kukisema, kukianzisha na kusimamia hoja zenye mashiko.
 
Ni ukichaa kutojifunza kwa walotutangulia.ccm kila ck kuomba misaada toka kwa wazungu kujifunza kwa nn wameendlea hamtak
 
Mbona huwa haurudi kujibu hoja unazozitoa. Kuna umaaana gani wewe kuleta hizi nyuzi nyingi kisha ukashindwa kuzisimamia. Hiyo ni dalili tosha kuwa haujiwezi (dhohofu ili hali), katika siasa. katafute kick ya mama lowasa
 
huyu naye sijui amerogwa na nani? wakati anaangaika kwa kurudia rudia shule kama muongo mbona akwenda kulima kwanza akapata fedha za kujisomesha. udaktali wake aliutoa kwenye kilimo? ujui mwenye njaa ndiye ana shauku ya kusoma aondoe balaa hii, yeye alivyougua kwskoo si kwa sababu wazaz walikosa elimu ya kumtunza?
 
Back
Top Bottom