A
Anonymous
Guest
Waziri wa fedha na mipango Dk. Mwigulu Lameck Nchemba amewaita vijana mbalimbali toka Kanda ya Ziwa na kukutana nao mkoa wa Singida mnamo tarehe 22.02.2023 kwa kile alichodai kuwa ni kumsemea mama huku nyuma yake kukiwa na ajenda ya siri na yenye nio ovu kwa vijana na viongozi wao.
Kikao hiki cha viongozi wa UVCCM Kanda ya Ziwa na Mwigulu alichotumia kupenyeza ajenda zake zenye lengo la kujijenga yeye binafsi ili awe na sauti kwenye jumuiya hiyo, ni muendelezo wa wa vikao vyake na viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wa kanda mbalimbali.
Mwingulu Nchemba anayo platform rasmi ya kumsemea mhe. Rais kupitia Uwaziri wake na vijana wanayo platform ya kumsemea mama ambayo ni jumuiya ya Vijana kupitia Kiongozi wake Taifa na wale wa mikoa, wilaya, kata na matawi kitendo cha Kuwaita vijana kinyume na utaratibu wa Jumuiya yao ni kukiuka taratibu na kujenga chuki na uhasama kati ya vijana na viongozi wao Taifa.
Waswahili walisema fumbo mfumbie mjinga mwerevu ataelewa katika hili Kuna ajenda ya siri kuelekea chaguzi si tu katika Ile ndoto yake ya kuwa Rais wa nchi bali katika kutengeneza safu za uongozi miongoni mwa vijana na kutengeneza sintofahamu.
Haya sawa vijana wa Kanda ya ziwa wamelamba mikono yenye bahasha ya milioni moja kila mmoja na fedha za kujikimu nauli, malazi na chakula Kuna kumsemea Rais kwa bahasha, anayo yafanya mama.Mwigulu kashindwa kuyasema kupitia wizara yake,? je, Jumuiya ya vijana imeshindwa kumsemea Mama ?
Ombi langu kwa Mhe. Rais mama yangu Samia Suluhu Hassan Imani uliyo iweka kwa baadhi ya wasaidizi wako hususani Mwigulu Lameck Nchemba wanaitumia vibaya sana, nakuomba mama jicho lako linaona mara tatu ya jicho langu, una vyombo, unakila aina ya pua la kunusa hili usiliache lipite.
Wakati vijana na viongozi wao wanapambana kuwa wamoja na kupaza sauti zao kwa ajili yako Mwigulu anawagawa na kuwatumia kwa ajenda zake binafsi.
Hii nchi ni ya watanzania wote na wote wanayo haki ya kula keki ya Taifa kwa haki na sifa stahiki na si kwa kuwekwa na watu wanotumia madaraka na nafasi walizopewa vibaya kwa maslahi binafsi.
Mhe. Rais hotuba zako mara zote ulipokutana na vijana ulisema mafanikio ya Vijana ni UMOJA, MSHIKAMANO na UPENDO umenukuliwa mara kadhaa mhe. Rais ukisema VIJANA WASITENGENEZEANE AJALI, chuki na Wivu visiwe sehemu ya vijana na badala yake Vijana wafanye kazi.
Sasa Mwigulu amekuwa kinyume nawe katika hili sasa ajenda yake ni Kuwagawa vijana, kuwatumia vijana, kujenga chuki na kufarakanisha vijana na kuweka makundi kwa maslahi yake.
Moja ya wajibu wangu kama kijana mzalendo wa nchi hii ni kuilinda nchi yangu, kukilinda chama changu na jumuiya zake na kuwalinda viongozi wangu kwa wivu mkubwa anacho kifanya Mwigulu hakivumiliki kwa mzalendo yoyote nchini.