Ajali ya kutisha Mandela road

Ajali ya kutisha Mandela road

Naibili

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,878
Reaction score
1,060
kuna ajali imetokea hapa Tabata Relini mda huu,
imesababishwa na Lori la kubeba makontena, likiwa linatokea ubungo, dereva wa lori alikuwa akitaka kupitiliza taa nyukundu zilizokuwa zikimtaka asimame, akajaribu kuwahi na kuongeza kasi mbele akakutana na mwendesha boda boda akitokea upande wa tabata dampo ili apite fasta, ndipo walipokutana kati kati ya mataa, mwenye lori gari ikamshinda akaingia upande wa gari zitokazo buguruni, ambazo zilikuwa zimeruhusiwa na taa, hapo
ndipo hatari ilipotokea, kwani lori limegonga gari zisizo pungua tano, dereva kakimbia, kuna vitz ilikuwa imetoka bandarini nayo imeharibika vibaya mnoo, mwenye boda boda amefariki dunia, na kuna majeruhi wengine wawili.

idadi ya waliokufa na ajali hii inaweza kufika watu nane na zaidi, kwa kweli inasikitisha saana,

nnaripoti kutoka eneo la tukio
 
Hiyo vtz haijaua kweli kwan the way ulivosimulia najua drv hatoka
 
kuna ajali imetokea hapa Tabata Relini mda huu,
imesababishwa na Lori la kubeba makontena, likiwa linatokea ubungo, dereva wa lori alikuwa akitaka kupitiliza taa nyukundu zilizokuwa zikimtaka asimame, akajaribu kuwahi na kuongeza kasi mbele akakutana na mwendesha boda boda akitokea upande wa tabata dampo ili apite fasta, ndipo walipokutana kati kati ya mataa, mwenye lori gari ikamshinda akaingia upande wa gari zitokazo buguruni, ambazo zilikuwa zimeruhusiwa na taa, hapo
ndipo hatari ilipotokea, kwani lori limegonga gari zisizo pungua tano, dereva kakimbia, kuna vitz ilikuwa imetoka bandarini nayo imeharibika vibaya mnoo, mwenye boda boda amefariki dunia, na kuna majeruhi wengine wawili.

nnaripoti kutoka eneo la tukio
Accidents don't just happen!!
Poleni.
 
Lo !balaa hii.
Madereva wa magari makubwa wengi wao si waadilifu ,vile vile madereva wa mabasi.
Wameathirika kisaikolojia kutokana na kutoa rushwa kwa traffics mara kwa mara ili waendelee kuvunja sheria.
Taa za barabarani ndio haziheshimiki kabisa.Hilo dhahiri shahiri limemshinda kamanda Mpinga.
 
hapo dereva alishavuta mibangi, hizo taa nyekundu alikuwa anana kjani zote. Pole waathirika wote.
 
swahiba simu yako haina uwezo wa kuchukua picha? au unayo kama yangu ya tochi?
 
inasikitisha..usiku una mengi..madereva wengi..wanasahau kabisa kuzingatia sheria..Mungu atunusuru
 
huu mchezo wa kufosi kupita kwenye taa nyekundu sijui utaisha lini
 
Duh jamani natamani nihame Tanzania na nisirudi kbs, vifo vya uzembe hivi jamani!! Pole kwa wafiwa na majeruhi Mungu awaponye na kuwapa wepesi

Na hiyo vitz ukute mtu kajiwekeza miaka2 ndio amenunu ama mkopo wa Bank, mweeeeee
 
kwakweli anaesema mitandao inafelisha ni mpuuzi maana fikiria habari kama hii badala ya waandishi kujichukukia ujiko saa nbili usiku lakin sasa tumefahamu.Mungu awape pumziko la milele
 
Acha ajali za magari kugongana na kupinduka kuna hawa jamaa wenye bodaboda kuanzia polisi na hawa wahuni wa Dar ambao wanchokoza watu makusudi ili wawapige risasi:rockon:
 
Back
Top Bottom