Hadi matuta yanayo haribu barabara na MAGARI yatakapo ondolewa na Sheria za Usalama zitakapo zingatiwa na kusimamia na kila muhuska ndo hizi ajali zembe zitaondoka
Ni kero sana kuendesha gari ktk barabara za Tz ambazo nyingi zimejengwa chini ya viwango na watumiaji kuanzia watembea kwa miguu mpaka madereva hawana habari na usalama barabarani!
Hata hivyo Songea napo ni mbali sana Mkuu na abiria wanapenda kuwai kufika. Ukichelewa kufika unaanza kuskia wanalichamba gari! Mara Oooh gari lenyewe halikimbii! Kesho yake unakuta abiria wote wamehamia Mbeya Express na Sai Baba. Wewe mwenyewe jiulize, watu wa Songea wanajua kabisa Superfeo linakambia sana lakini kila siku wanajazana humo humo! Ni kwa sababu wanapenda huo mwendo ila yakitokea majanga wanawageuka madereva. Utaskia Oooh Dereva alikuwa anaendesha kwa spidi sana! Ila wakifika salama hawalalamiki!