Ajali ya basi Gairo

testa

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
442
Reaction score
183
Wakuu kwa yeyote mwenye taarifa zaidi atufahamishe nimepigiwa simu na ndugu yangu kuwa kuna ajali ya basi imetokea muda si mrefu maeneo ya Gairo ni basi la kampuni ya Champion na lori la mizigo watu sita wamefariki hapohapo na majeruhi ni wengi yeyote mwenye taarifa zaidi atujulishe
 
Daah mwenye update yoyote atujuze hapa.....
 
Ni kweli kabisa Basi la Champion limegongana na lori la mafuta (Semi-Treller) na watu watano wamekufa hapohapo huko Gairo leo hii
 
Malori yamezidi barabarani! Watunga sera ndio hao wanaomiliki malori. Wameiua reli. Hivi vifo vutaendelea kutokea, na hakuna anayejali. Kwa wastani sasa wanakufa watu 3,000 kwa mwaka. Fikiria, hata ukikuta mahali inzi 3,000 wameuawa, lazima ushituke! Tanzania tuamke! Polisi wanakagua kadi ya gari badala ya kukagua breki na mataili!
 
sikuwahi kuliwaza hili suala lakini sasa nalielewa kidogo. Mbali na uzidishaji uzito lakini reli inaweza kuyapunguza kwa zaidi ya 60% endapo itafunction kwa 95% angalau. Hakuna mwizi ambaye yuko tayari kuyaona maloli yake yakikosa kazi kisa treni iko njiani!
Poleni sana waliopatwa na mkasa pamoja na familia husika
 

Pamoja na suruhisho la kisiasa lililotolewa 1993 kutokana na ajali ya bus la Yarabi Salama kwamba magari yote ya abiria yasafiri mchana kuepuka ajali lakini bado zinazidi kutokea, kiukweli malori ni mengi sana
 
Ni kweli kabisa Basi la Champion limegongana na lori la mafuta (Semi-Treller) na watu watano wamekufa hapohapo huko Gairo leo hii

asante mkuu kwa taarifa
 
Basi lililohusika ni Super Champion Na. T 277AJR limegongana na Lori la mafuta Na. T 494 BDG dereva a wa basi kakimbia na wa Lori yupo anahojiwa na Traffic police.
 
bas lilikuwa likitokea wap na lilikuwa lina enda wapi? ajali imetokea mda gani?
 

Manyerere Jackton

Licha ya Malori kuzidi lakini pia madereva wa mabasi hawazingatii sheria za barabarani na sio waangalifu!

Unakuta dereva anaovatake kwenye kona, anaovatake magari zaidi ya mawili kwa wakati mmoja, wanaenda kwa kasi kama unafikiri wanawahi kwenda sayari ya Jupiter!

Hebu angalia picha hapa chini na ndio kawaida yao ya kuendesha magari sasa kwa hali kama hii ajali zitaepukika?



 
Rip wote waliokufa na get well soon waliojeruiwa.
 
Hizi ajali kwa kweli ni Mwenyenzi Mungu mwenyewe ndiyo atuepushe nayo!
Na wote wale walipotokewa na Ndugu poleni sana na Mungu awajaze nguvu katika kipindi hiki kigumu!
Na marehemu wote wapate pumziko la milele shambani mwake Bwana wetu!
 

Wewe unafikiri ni kwa nini kipaumbele cha maisha ya watanzania leo hii kimegeuka kuwa barabara bora kuliko maisha bora? hebu chukua matrilioni yanayomwagwa kwenye mabarabara kwa mwaka mmoja tu uyaelekeze kwenye reli kama hununui vichwa vipya na mabehewa kibaaao na kujenga reli mpya hadi kigoma. Sasa hiyo ni bajeti ya mwaka mmoja je ya maiaka kumi? barabara inajengwa leo baada ya miaka miwili inajengwa upya watu wanajali matumbo yao bhana
 
Vizibiti mwendo viliishia wapi?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Its so sad maana mimi binafsi.nimeishuhudia.nikiw kwenyr gari nyingine. Malori yaliyohusika.ni mawili na kuna watu na vidumu wanagaka.mafuta sema polisi wapo. Basi limepigwa pasi upande wa kulia limeharibika vibaya na matairi ya mbele yamechomoka.

RiP waliofariki.
 
Vizibiti mwendo viliishia wapi?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Ilikuwa deal ya watu, washapiga hela wameona hailipi tena,
wanapanaga new mkakati wa-introduce another related deal!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…