Polisi wa usalama wa barabarani nisikilizeni! Huu sasa ndio wakati wa ninyi kufanya kazi kwa bidii na hasa hizo barabara za masafa marefu mikoani. Gari kama Hood ya Mbeya to Arusha, mabasi kama Ngorika ya Arusha Dar na hili la Mghamba la kwneda Mwanza Arusha, yaangalieni sana kwa umakini ninyi polisi wa Babati na Singida na Tabora, na hawa Polisi wa Pwani hapo Chalinze na Morogoro fanyeni kazi yenu kwa umakini sana ajali ni nyingi sana kagueni magari mpaka ndani, muwahoji abiaria kwenye vituo vya chakula wanaposhuka muwe mna mtu wenu pale ahoji abiria wanapoingia na kabla ya kutoka mwendo wa gari ukoje. watawaambia na toeni namba zenu za simu na wala sio ile namba ya mtu mmoja alieko ofisini Dar.