Ajali nyingine Kibaha!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,353
Reaction score
26,194
Baada ya Jumapili kutokea ajali ya gari Visiga Kibaha,leo kumetokea mlipuko katika Kiwanda cha Nondo Zogowale Kibaha. Kiwanda hicho kinamilikiwa na wachina. Taarifa zinadai kuwa mlipuko huo umetokea katika moja ya mitambo ya kutengenezea nondo. Hadi sasa,taarifa zisizo rasmi,zinaonesha kuwa watu wanne,akiwemo mchina mmoja,wamefariki. Wengine kadhaa wamejeruhiwa. Taarifa zaidi zitafuata kadiri zitakavyopatikana..
 
...aha! hiki Kiwanda ndicho kinachoitwa HONG YU STEELS (T) Co.LTD kiko maeneo ya Madafu kelekea Mlandizi???? ndo kilikuwa kinafanyiwa TEST uzalishaji rasmi ulikua haujaanza Dah! basi tu
 
...aha! hiki Kiwanda ndicho kinachoitwa HONG YU STEELS (T) Co.LTD kiko maeneo ya Madafu kelekea Mlandizi???? ndo kilikuwa kinafanyiwa TEST uzalishaji rasmi ulikua haujaanza Dah! basi tu
Ni hichohicho Mkuu.Kipo Zogowale ukiingilia Visiga-Madafu
 
Mlipuko tena ya kiwanda cha wa china, kama milipuko ya migodi ya kule China. Mola atunusuru

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ni hichohicho Mkuu.Kipo Zogowale ukiingilia Visiga-Madafu
Umesomeka mkuu: huo mlipuko usije kuwa ni Bomu ambalo lilikua limefichika ndani ya vyuma chakavu wanavyonunua Uswahili kama materials za kuzalishia Nondo, niliendapo juzi kikazi nikakuta vyuma chakavu vimemwagwa karibu na mtambo, nikawashauri wawe wanavisogea mbali kidogo kwa usalama wao wakadai vikiwa mbali sana ni usumbuvu wakati wa kuviitaji.
 
Yawezekana Tanzania haiko tayari kwa maendeleo kama haya ya viwanda?
 
Jamani si waende wakachukue chuma pale Liganga Ludewa chuma kipo tele
 

Uko sahihi mkuu kuna jirani yangu hapa mdogo wake ni mmoja wa waliokufa,ametoka hapa Mbezi Beach kuelekea Tumbi Hospital kutambua mwili wa marehemu mdogo wake na taarifa alizopewa ni kuwa mlipuko unaosadikiwa kuwa bomu ndio umesababisha vifo hivyo.
 
pole zao waliopoteza ndugu na jamaa hiyo ni ajali, japo tahadhali ni muhimu.
 

Mkuu yani hapa ninamajonzi ya kutosha sababu katika hao wanne amefariki mtoto wa mama yangu mdogo, yani mikono imechomwa na vuma miguu na kadhalika.

Huo mlipuko umetokana na Bomu ambalo liliokotwa kama skrepa bila kujua. Kilichotokea walikua wanamwaga hivyo vyuma kwenye vitu kama mitungi mikubwa kwa inayochoma hivyo vyuma, matokeo yake ndo hayo ndugu yangu duuu...
 

sasa vimewahitaji wao na vimewaletea usumbufu wao
 

Huruma zake Mola zinahitajika sana katika kipindi hiki kifugumu.

Eeh Mola wetu tunakuomba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…