Ajali mbaya yaua 14

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,465
Watu 14 wamefariki dunia katika ajali ya Fuso iliyotokea katika Kijiji cha Luguru. Gari lilikuwa na wafanyabiashara na mizigo, wakiwa wanakwenda mnadani katika Kijiji cha Mwamapalala.

Chanzo: Ndugu zangu waliopo eneo la tukio.
 
RIP KWA WALIOFARIKI, POLE KWA MAJERUHI! MUNGU WETU ATULINDE KILA TUWAPO SAFARINI, amen!
 
Ishathibitiswa na daktari kama kapokea idadi hiyo ya maiti?
 
Hizi ajali zilivyoshamili sijui lini idara husika watakaa chini waanze kufikiri nini cha kufanya
 
R.I.P marehemu wote,get well soon majeruhi wote!
 
Ajali ya kwanza kuchukua maisha ya watu wengi tangu mwaka uanze. Ee Mungu utusaidie .... Nuru ya milele uwape ee Bwana, na mwanga wa milele uwaangazie. Wapumzike kwa amani. Amina
 
Mkao wa hawa watu kwenye Malori ni mbaya sana sana, hasa hawa wanaoenda Minadani WANAKAA vibaya sna sana ,,,wanajaza lori halafu wanakaa juu ya ile mizigo ni hatari sana sana...
 
R.I.P marehemu wote. Ila jamani hizi ajali na madereva wetu ni kitu gani? Naona pia leseni ni za kubabaisha. Kuna kisa cha kweli mtu aliomba leseni ya daraja D ambayo alisoma driving tu na wala gari hakuwahi kuendesha, na ni katika leseni hizi mpya!! Unajua eti pale watoa leseni wana vishoka pale na akapewa leseni class E!! Sasa huyu akiendesha fuso si hatari? maana leseni ni valid!!
 
Huko nako kumezidi, kama sio Zakaria utaskia Bunda bus na kama sio Bunda bus utaskia Zuberi yaani mwanzoni mwa mwaka, katikati na mwishoni lazima hizo bus zitoe kafara ndugu zangu wasukuma na wakurya.Sasa kama kafara zimehamia na kwenye fuso twafa lelo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…