Tetesi: Ajali Lucky Vincent School: Uzembe, Tamaa, Ubadhirifu na Kutokujali Usalama wa Wanafunzi

Ntate Mogolo

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
403
677
Wazazi poleni kwa msiba huu uliowapata watoto wetu wapendwa wa Lucky Vicent na walimu wao! Hakika ni majonzi makubwa sana! Lakini yafaa tutafakari kwa kina kwanini janga kama hili liwafike watoto hawa, tumaini la maisha yetu! Maswali ni mengi, na kwa kweli yana hitaji majibu ya kina.

Kwa tunaozunguka kutwa barabarani, mtakubaliana na mimi kuwa, vipo viashiria vingi hatarishi kwa watoto wetu wanapotumia mabasi ya shule zao. Shule nyingi zinatumia mabasi ambayo zamani yalitumika kama daladala, na baada ya kuchoka yakabadilishwa na kuwa mabasi ya shule. Huku madereva wakiendesha kwa mwendo usiostahili kabisa kubeba watoto.

Hatari zaidi, mabasi haya ya shule hubeba idadi kubwa ya wanafunzi kuzidi uwezo halisi wa gari, na kutokuzingatia taratibu zote za kiusalama kama vile kufunga mikanda. Mfano wa hili ni hii ajari ya Lucky Vicent. Wanasema "eti gari lili feli breki" ndo sababu ya ajari! Binafsi sikubaliani nalo.

Kwa wale ambao wameendesha magari makubwa kwa weledi na kwa kipindi kirefu, watakubaliana na mimi kuwa, kubeba uzito zaidi ya uwezo wa gari pamoja na mwendo kasi husababisha mfumo wa breki za gari kushidwa kuhimili, hivyo kutokukamata pale dereva anapozitumia.

Sababu nyingine ya kujiuliza, je ni kweli haya mabasi ya shule yanafanyiwa matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara, kwa maana ya motor vehicle service! Hapa inatiashaka! *A motor vehicle service is a series of maintenance procedures carried out at a set time interval or after the vehicle has travelled a certain distance.* Shule ya Lucky Vicent lazima ithibitishe kwa kuonyesha *service na log books* za hilo gari, majibu utayaona, hakuna kumbukumbu ya service.*The completed services are usually recorded in a service book which is rubber stamped by the service centre upon completion of each service.* Mashule mengi yanahuo udhaifu, na hii inatokana na uzembe, tamaa, ubadhirifu wa watendaji wao, kutokujali maisha ya wanafunzi na kutokuwa waangalifu huku wakiweka mbele masilahi yao na kupata faida.

Matengenezo muhimu na ya mara kwa mara kwa gari *motor vehicle service* ni kama ifuatavyo;
-Change the engine oil & oil filter
-Replace the air filter & fuel filter
-Tune the engine
-Check level & refill brake fluid/clutch fluid
-Check Brake Pads/Liners, Brake Discs/Drums, and replace if worn out.
-Check level and refill power steering fluid
-Refill Manual Transmission Fluid,Grease and lubricate components inspect.
-Check condition of the tires
-Check for proper operation of all lights, wipers etc.

Vipuri vingine vyote vinavyo weza kulifanya gari lisiwe salama kwa matumizi ya barabara hukaguliwa na kubadilishwa wakati wa kufany *service* je mashule yetu wanafanya haya! Kama haya hayafanyiki ni wakati sasa wazazi wa watu wote wenye matashi mema kuchukua hatua za kuwawajibisha wahusika wote ili kuokoa maisha ya watoto wasio na hatia.
 
inasikitisha sana ni sahihi ulichokiandika lakini mkuu kaa ukijua ajari haina kinga gari linaweza kuwa na hayo yote na dreva ni mzoefu wa miaka mingi ninachoweza kusema yawezekana dreva alikuwa mzembe sawa lakini! ! mazingira yalichangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa ajari yani mvua, ukungu na mahali penyewe yote kwa yote tunapata fuzo kubwa sana sisi tuliobaki Mungu awalaze mahali pema watoto wetu majeruhi awaguse pole kwa kwawalio fikwa na msiba

kinachonipa shida ni mtoto alietoka akiwa hana ana mchubuko zinazunguka picha 2 tofauti za jinsia tofauti sijui ninani kati yao muhusika
napia wanasema aliepona alikuwa kwenye gari la nyuma tofauti na lile lililo pata ajari maana gari zilikuwa wengine wanasema 4 inasikitisha sana kwakweli
 
Mkuu kwa haraka basi lile siyo basi la shule Ile sababu mabasi yao ni mawili Na daladala lile lilikodishwa asubuhi sana kwa akili ya safari hiyo Na dereva hajawahi kuendelsha gari bara bara ya karatu ambayo inakona na milima mikali pia gari ilikuwa Na tatizo la brake system na stearing ilikuwa Na shida iliyopelekea kushindwa kupiga gari ukutani wala kukamata brake hata za ghafla Na gari kupaa hadi kutua chini
 
d703cfe4628c0e6e291c7ffda54c81e1.jpg
90449aafb608d9a5c8e3dae8e90c7460.jpg
 
Hilo gari limepita sehemu hatarishi kuliko hata sehemu ya ajali...


Kama kingekuwa bovu kama unavyotaka tuamini basi lisingeweza kutoboa eneo linaitwa Kilima Tembo.
Fafanua. Kwahivyo tatizo ni nini kilichopelekea ajali hii yenye kuhuzunisha
 
Kwa balabala iyo ya serekali ya chama tawala unaionaje?. Gali inabeba kwa wingi na uzito. IVI uzito wa watoto hap na uzito wa kupakiwa na basi ilo unadhani ilizidiwa?Hapana. Barabara mbovu. Pili izo motor vehicle ni biashara zaidi. Nina gali na huwa tunauzia njiani tu kwa miaka mingi. Nano anakagua?. Tatu utamuona veko anakagua mabasi ubungo saa Kumi na mbili kabla hayajaondoka ndani ya saa nzima anakuwa amemaliza! NDIO kituko kingine. Maajabu hayataisha.
 
Back
Top Bottom