Ajali haisababishwi na shetani

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,944
Kama wengi wa wanadamu, hasa waamini wa dini mbalimbali wanavyosema mara baada ya kutokea ajali kwamba shetani ndiye msababishaji wa ajali husika. Hii si kweli, kwa hoja zifuatazo;

A.Kama shetani ndiye chanzo kikuu cha ajali, je, Nchi zinazoongoza kwa kiwango kikubwa cha ajali ni sawa kwamba nchi hiyo ina uovu mwingi na shetani kaweka ngome kubwa zaidi ya nchi zingine?

B.Je, shetani makao yake hasa ni mahali penye jiografia tata kama milima mikali, korongo n.k kwakuwa maeneo hayo ndo huongoza kwa ajali zaidi ya eneo tambarare?

Kwa mtazamo wangu ajali husababishwa na mwanadamu na katika kila ajali lazima makosa ya kibinadamu yatokee ndipo itokee ajali. Ajali husababishwa na mambo mengi hata zaidi ya kumi lakini yote hayo mwanadamu lazima awe ndiye kisabibishi. Ngoja tuangalie sababu hizi tatu ambazo ndani yake ndimo sababu zingine hujificha.

1. Gari/chombo, kuna ajali nyingi ambazo gari au chombo ndiyo sababu, mfano:gari kufeli breki, kuchomoka tairi n.k haya yote husababishwa na mwanadamu kutokusimama katika nafasi yake vizuri, kwanini achukue gari ambayo ilikuwa na matatizo na kuiendesha. Laiti ingekaguliwa kwaundani hii hali isingetokea.

2.Barabara/njia, anayepaswa kuhakikisha barabara ina alama zote kwa ajili ya usalama ni binadamu na si shetani, anayesimamia ujenzi wa barabara kwa kiwango kinachostahili ni mwanadamu, anayepaswa kujua kwamba barabara hii inafaa kwa kupita na chombo fulani ni mwanadamu, anayekontrol movement za magari, watu na vyombo vingine ni mwanadamu. Kwahiyo ajali haisababishwi na njia/barabara bali ni mwanadamu.

3.*Mwanadamu/dereva. Dereva anapoacha moja ya kanuni za usalama barabarani tayari yuko katika hatari ya kusababisha ajali, hapa mwendesha pikipiki, anayetembea kwa miguu, anayesukuma mkokoteni mmoja akiharibu tu yatosha kwa kusababisha ajali.
 
Naunga mkono hoja kwamba Lucifer anasingiziwa.
Pili napenda niongezee nyama kidogo kwenye hilo namba moja.
Ni hivi mechanical malfunctioning hujitokeza hata kama gari imekaguliwa...kwa hiyo binadamu asilaumiwe kwa asilimia mia kwenye hili.
Hapa alaumiwe kwa asilimia 30 tu.
Kama ni mtu wa magari utanielewa vizuri.
 
Back
Top Bottom