AJALI: Fuso na Hiace zagongana na kuu watu SITA, kujeruhi NANE huko Same, Kilimanjaro

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Watu sita wamefariki Dunia na wengine nane wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha basi dogo la abiria aina ya Hiace lililokuwa likitokea Mjini Same likielekea Njoro Wilayani Same, ambapo liligongana na gari ya mizigo aina ya Fuso muda mfupi baada ya kuondoka katika Kituo cha abiria cha Same Mjini.

Daktari aliyezungumza na Mwandishi wa JamiiForums katika Hospital ya Wilaya ya Same, Dkt Mlay, amesema wamepokea Maiti sita ambazo amebainisha kuwa wanaume ni watano na mwanamke ni mmoja.

Aidha, ameongeza kuwa Majeruhi nane walipatikana kufuatia ajali hiyo, ambapo katika Majeruhi hao nane wanawake ni wawili na wanaume sita na kati yao waliopewa rufaa kuelekea Hospitali ya KCMC ni watatu, wanaume wawili na mwanamke mmoja.

Majeruhi Noel Bakari Kanumba, aliyekuwa anatokea Mjini Same kwenda Kavambughu, akizungumza na Mwandishi wa JamiiForums katika wodi ya Wanaume katika Hospitali ya Same, amesema alikuwa amekaa Kiti cha mbele na Dereva ambapo aligundua kuwa Dereva alikuwa amelewa akamwonya asikimbize gari lakini hakutaka kumwelewa, ndipo gari lilimshinda na kuhama upande wake na kuelekea upande wa pili na kugonga Fuso upande wa Dereva la Fuso hali iliyosababisha ajali ambapo Dereva na abiria mwenzake waliokuwa wamekaa Kiti cha mbele walifariki Dunia papo hapo.

Majeruhi wengine ni Musa Chikira (35), alikuwa anatokea Mjini Same kwenda Njoro na Mariam Omary Mbaga aliyekuwa katika wodi ya wanawake.

Chanzo: Mwandishi wa JamiiForums

========
PICHA:
Ajali yenyewe:
image.jpeg

image.jpeg

image.jpeg

image.jpeg


Majeruhi:

image.jpeg

Majeruhi wa ajali hiyo, Musa Chikira (35), akiwa amelazwa katika wodi ya wanaume, hospital ya Wilaya ya Same.

image.jpeg

Majerhi wa ajali hiyo, Noel Bakari Kanumba (36), alikuwa anatokea Same Mjini akienda Kavambughu.

image.jpeg

Majeruhi wa ajali hiyo, Mariam Omary Mbaga akiwa amelazwa wodi ya wanawake
 
Pele kwa wafiwa wote japo dereva wa hiace ndo aliifuata fuso.

Ndio habari kubwa hapa ktk viunga vya mji mdogo wa same.
 
Kuna siku nilipanda daladala seat ya mbele, nikagundua dereva alikua amelewa, kiustaarabu nikamwambia aniachie niendeshe nikamwwonesha na leseni yangu, akajidai kubisha nikatishia kumshushia mangumi ya mohamed Ali, akaufyata, nikaendesha break ya kwanza kituoni akawekwa ndani mwenye gari akatuma dereva mwingine safari ikaendelea. Tusipende kupuuzia jambo tunapoona dereva amelewa, hakuna usalama hapo.
 
Back
Top Bottom