Airtel Wezi

Bingwaman

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Posts
548
Reaction score
288
Kwa mara kadhaa katika siku za karibuni nimejiunga na kifurushi cha dakika 20 cha Airtel kwenda mitandao yote lakini nimeongea si zaidi ya dakika tatu na simu kukatika kwa maelezo kuwa kifurushi kimekwisha. Kibaya zaidi hata unapoangalia salio unakuta hakuna kitu. Kwa mfano, leo nilibakiwa na salio la shilingi 2,000 baada ya kujiunga na kifurushi, lakini nimezungumza dakika tatu tu na simu kukatika, eti kifurushi na salio vimeisha. Huu ni wizi wa wazi kabisa unaofanywa na 'Baba Lao', lakini mamlaka zetu tukufu ziko kimya. Nimeamua kuiweka sandukuni laini yangu ya Airtel.
 
Chukua jukumu la kuwapigia au kuenda ofisi zao.

Wakurekebishie.
 
Chukua jukumu la kuwapigia au kuenda ofisi zao.

Wakurekebishie.

Hivi hao TCRA kazi yao nini haswa? Au ni kusimamia kuuza ving'amuzi tu? Inauma sana kuona wananchi tunanyonywa na hawa wanaojiita wawekezaji kumbe wezi watupu.
 
Hivi hao TCRA kazi yao nini haswa? Au ni kusimamia kuuza ving'amuzi tu? Inauma sana kuona wananchi tunanyonywa na hawa wanaojiita wawekezaji kumbe wezi watupu.

Sasa hao TCRA watajua bila kuambiwa? Sometimes leakage inaweza kutokea somewhere, so its better to get out of blame game and take some measures. I have been using Airtel for years and I've never experienced such a problem.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ