AIRTEL Money wamenifilisi bila kutegemea, TCRA Mko wapi tunatapeliwa hadharani?

okonkwo jr

JF-Expert Member
Jun 14, 2015
2,419
1,737
Wapendwa wangu amani ya bwana itamalaki kwenu,juzi nilikuwa natuma pesa nyumbani ambayo nilikopa kwa vikundi vya kukopesha,ajabu tangu nimeituma juzi hadi leo haijafika,nimewasiliana na watoa huduma wa airtel hakuna msaada zaidi,ila wananiambia subiri baada ya saa 24,tangu juzi hadi leo ni masaa 70 sasa,wakuu nianzie wapi kudai pesa yangu,je nikienda mahakamani aitel watanilipa?,izingatiwe kuwa mpaka sasa nimepigwa penati mara tatu ya kiasi nilichokopa kwa kuchelewesha kurejesha mkopo Kwa mjibu wa kikundi nilichokopa,nahisi airtel wamenibebesha mzigo nisio stahili,naomba msaasa wenu nahisi kutapeliwa na hawa AIRTEL,
 
Wapendwa wangu amani ya bwana itamalaki kwenu,juzi nilikuwa natuma pesa nyumbani KWA AIRTEL MONEY ambayo nilikopa kwa vikundi vya kukopesha,ajabu tangu nimeituma juzi hadi leo haijafika Na mlengwa hajaipokea,nimewasiliana na watoa huduma wa airtel hakuna msaada zaidi,ila wananiambia subiri baada ya saa 24,tangu juzi hadi leo ni masaa 70 sasa,wakuu nianzie wapi kudai pesa yangu,je nikienda mahakamani aitel watanilipa?,izingatiwe kuwa mpaka sasa nimepigwa penati mara tatu ya kiasi nilichokopa kwa kuchelewesha kurejesha mkopo Kwa mjibu wa kikundi nilichokopa,nahisi airtel wamenibebesha mzigo nisio stahili,naomba msaasa wenu nahisi kutapeliwa na hawa AIRTEL,
 
Hiyo No. ya mpokeaji ni sahihi? Isije umeandika 2 badala ya 5 kwa sababu hizi simu za mtelezo ni shida nazo
 
Katika mkoa uliopo kuna Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Mawasiliano. Hii ni ngazi mhimu katika mkoa ambayo ni Mwakilishi mbadala wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA. Ukifika huko suala lako litawasilishwa ngazi zifaazo.

Hatua ya kwanza ya kuwasiliana na mtoa huduma wako tayari umeifuata tena bila mafanikio. hivyo nenda katika hilo baraza. Wakishindwa watawasilisha TCRA, ikishindikana ni polisi na hatimae mahakamani hadi haki yako ipatikane.
 
Asante mkuu,kiufupi nimeumia sana mpaka sasa sina njia mbadala
 
Endelea kusubiri me ishanitokea zaidi ya mara 2 tatizo kama hilo cha msingi waambie wakurudishie pesa zako
 
Back
Top Bottom