Airtel acheni kutuibia wateja.

Malilambwiga

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
485
296
Ndugu zangu wana jamvi kama nitakosea basi mtanisahihisha.

Mimi nimekuwa mtumiaji wa mitandao mbali mbali ya simu ukiwamo mtansao wa simu wa Aurtel.

Ninaponunua au kuweka muda wa maongezi kuanzia kifurushi cha Tsh.2000 ukichagua kujiunga unapata dakika na Mb.10 za internet.

Tatizo la mtandao huu hata kama ndo umejiunga na hata ktk simu yako haujawasha Data con. bado Mb ulizopewa zinachukuliwa au hata ukijiunga kwa maana ya kupata kifurushi cha Tsh5000 ili upate lGb ukianza kutumia tu hata dakika tatu hazipiti unaletewa sms ya Urushi kukujulisha umeshatumia 90% ya bando lako.

Nionavyo mimi mtandao huu unatuibia wateja na hata TCRA imekaa kimya kufuatilia huduma za kinyonyaji za makampuni haya.

Mfano hivi inakuwaje umejiunga muda wa maongezi wa 5000 kisha kampuni inakuwekea kikomo cha muda wa kutumia. Kwa nini muda wa mwisho wa matumizi usiwe juu ya mteja kwa kiwango alichoweka na kwisha kwa salio lake.

Kwa jinsi nilivyochukizwa na kitendo hiki nimeamua kuachana na Airtel na kuhamia Halotel. TCRA nendeni na kasi ya awamu ya tano.
 
Back
Top Bottom