Aina 10 za wanawake zitakazofanya maisha yako kuwa magumu

Mr.Thinker

Senior Member
Dec 13, 2013
125
141
Ok. Katika kuangalia tabia za wanawake, nakuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

1. Mtumiaji

Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

2. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

3. Mlalamishi

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.

4. Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.

5. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

6. Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.

7. Nusa Nusa
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.

8. Asie na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.

9. Mcheza ndondi
Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

10. Mtoto wa mama
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.
 
Mpangaji wangu mm mkewe hana akili ya maisha ht kidogo namsikitikia huyu baba

Ana mke ambae kazi yake ni kuringisha kula,kuvaa na kutumia wakati nyumba wamepanga!

Huyu mama ana sifa balaa wao wanachujua kujichana tu wakati kwa vipato vya sie masikini waweza kuunga unga tu na kula kwa kujibana mpk upate sehemu yako ht chumba mbili

Yeye anasema kujenga ghali wakati ana uwezo wa kuingiza elf30 kwa Siku maana ni
mfanyabiashara namuonea huruma sana maana maisha haya pale akipata matatizo au ugonjwa ishakula kwake

Mdogo wangu na mmewe walikua watu wa kutumia tu shosti yuko mkoani likizo akija dar anaweka km laki6 ya shopping hivi za kununua nguo nk

Kwao wanakunywa maji safi wanajichana tu na luxuries zote wote watumishi wa umma huu mwaka wa nne sasa wapo wapo tu

Mwezi October nikaongea nae nikawaambia hivi kwa nn msinunue Kiwanja huko mliko ht km hamkupendi ardhi inapanda thamani jengeni ht mkihama mtapangisha na nikamrusha roho kuna kitu nimefanya aiseeh walipagawa haswaa..

Juzi kaja likizo kaniambia tumennua Kiwanja tunataka kuanza kujenga na amekuja km na laki 3 tu za shopping sasa hivi
 
hongera sana kwa moyo wa ushauri gene
kuna mdada jirani napoishi nyumba laki saba hana kazi ana mtoto mmoja mume tu ndo anafanya kazi. kuna mdada wa usafi anakuja kwa week mara tatu analipwa elf kumi kila siku.mume anamdharau analetya michepuko hadi ndani .nimemshauri afanye hata biashara hataki kila siku anadai subiri kidogo .hapo ujue hana hata wazazi ni yatima kwao choka mbaya ila anajifanya kuishi kama malkia .hela yote ya mume inatumika hapo kwa hapo maana wana matumizi balaa.
KUNA WANAWAKE MIZIGO KWELI .hata nguo zikifuliwa hawezi kuanua zinakaa kwenye kamba kama huyo dada wa kufua hajaja zinakauka mpaka zinaomba maji ya kunywa
 
Kumbe ndo unakuja kutuanika hivi jamii forums mama mwenye wetu, asante sana i
 
hongera sana kwa moyo wa ushauri gene
kuna mdada jirani napoishi nyumba laki saba hana kazi ana mtoto mmoja mume tu ndo anafanya kazi. kuna mdada wa usafi anakuja kwa week mara tatu analipwa elf kumi kila siku.mume anamdharau analetya michepuko hadi ndani .nimemshauri afanye hata biashara hataki kila siku anadai subiri kidogo .hapo ujue hana hata wazazi ni yatima kwao choka mbaya ila anajifanya kuishi kama malkia .hela yote ya mume inatumika hapo kwa hapo maana wana matumizi balaa.
KUNA WANAWAKE MIZIGO KWELI .hata nguo zikifuliwa hawezi kuanua zinakaa kwenye kamba kama huyo dada wa kufua hajaja zinakauka mpaka zinaomba maji ya kunywa
mpumbavu huyo Dada loohh!binti wa kazi elf10!
hajielewi ht chembe akili za kijinga hizo
 
fanya ujenge starehe haziishii!!kula hakuishi,kuvaa hakuishi
Kila kitu kitaisha pale tutakaisha maisha yenyewe mafupi haya. Utajinyima mwisho waje wafaidi wengine kabisa wakati huo we Haupo tena, maisha ndo haya mwenye kujenga maghorofa na ajenge, kula kulewa na alewe mwenye madem 20 awalale tu yani kila mmoja aishi awezavyo ila asivunje taratibu zikizowekwa na mamlaka.
Na umeme umepanda gharama 8.5% badala ya 20% iliyopendekezwa awali, tutanyooka tu
 
haya bwana Ila waweza jikuta unaenda mpk 80yrs ndo utakapochanganyikiwa sasa
 
Back
Top Bottom