Aina 10 za ndoa tunazofunga kwa kujua au pasipo kujua

Mtanzanyika

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
370
424
1. NDOA YA MKEKA
Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu. Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika mwaka mmoja tu baada ya wanandoa kugundua hawakuwa wakipendana!

2. NDOA YA MIHEMKO (NYEGE)
Hufungwa na vijana wenye umri wa miaka kati mume18 mke 16. Huvunjika baada ya miaka 3 au 4 ya ndoa.

4. NDOA YA MAONYESHO
Wenye ndoa Hii hupenda kujionyesha barabarani. Ila ndani hazina utii. Hupigana kila wanaporudi kutoka kwenye mizunguko. Cha kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa zinazoongoza kwa kuchepuka!

5. NDOA YA UHAMISHO.
Hufungwa na watumishi wa vijijini na mjini. Ili wa kijijini ahamie mjini. Mahari hutoa anayetaka kuhamia mjini. Hata kama mahari atatoa mume lakini hii ndiyo ndoa yenye ukakasi zaidi.Huvunjika mara tu wanapoanza kuishi wote mjini. Salama ya hii ndoa ni kuhama kutoka mjini kwenda kijijini.

6. NDOA YA MIMBA.
Hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki kuonekana makwao kuwa wamezaa nje. Au muolewaji alikuwa hampendi muoaji kwa dhati.Muoaji hutumia mimba kama mtego wa kuingia ndoani. Hii huvunjika mtoto akizaliwa na kufikisha mwaka 1.

7. NDOA YA MALI (UTAJIRI)
Muolewaji miaka 18 au 28 Muoaji 65 au 70.Ndoa hii pia huitwa ndoa ya babu na mjuukuu. Ndoa ya aina hii hudumu, kwasababu mwenye kauli ni mwenye mali. Asilimia kubwa ya waume wa ndoa hizi hulea watoto wasio wao.

8. NDOA YA KWA SABABU.
Hufungwa ili mradi muoaji au muolewaji aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au kaolewa. Huwa hazina utii wala upendo dhati. Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka 4 huwa hazivunjiki wahusika huishi kwa mazoea.

9. NDOA YA UPENDO.
Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya vita vya Kagera. Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote.

10. NDOA KUCHUMA
Ndoa hii ufungwa ili mradi muoaji au muolewaji akapate kitu au vitu fulani kutoka kwa upande mmoja wapo. Hii hudumu miaka kadhaa kutegemea na malengo ya mhusika. Wengine husubiri mpaka mhusika afe,lkn hujikuta wanakufa wao kwanza
 
Nasubiri episode 02 huenda kuna kategori ya 11 Si kuna hizi ndoa ambazo zipo tu kwa kuwa nafasi fulani ya uongozi haimtaki mtu asiye na ndoa? Hata nanihii na mama watoto si walikuwa singo singo hadi alipochukua ndo wakayunaiti? alafu naomba kuulizia hivi ndoa ya yule wa tatu toka tano ama ukipenda kuanzia moja bado ipo baada ya kumaliza? Natanguliza shukrani!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom