Ni aibu kwa mtu aliyefikia ngazi ya ujaji na uanasheria mkuu kufanya aibu kama hizi. Suala la Zanzibar linapindishwa, linatetewa na kuhalalishwa. Si wengine bali ni wale wale watawala walafi na wapindishaji mambo.
Jaji lubuva amekaririwa katika kauli tata mbili ndani ya kipindi hiki cha mkwamo wa kisiasa Zanzibar. Kwanza alithibitisha kuwa kwa upande wa Zanzibar, uchaguzi wa Jamuhuri ya Muungano ulikuwa sawa na akaendelea na taratibu hadi kumtangaza mshindi wa urais wa JMT na wabunge na madiwani. Kipindi chote hicho alinyamaza kimya hasa wakati wa mjadala wa uhalali wa kikatiba na kisheria kuhusu Jecha kufuta uchaguzi uliokamilika. Hakuja kuthibitisha nguvu za kisheria juu ya hilo. Kauli hii iliwaaminisha watu kuwa atasimamia Ukweli kwamba NEC ilitumia resource za ZEC katika uchaguzi ule vikiwemo vituo, wasimamiaji, idadi ya wapiga kura, mazingira na hata usafiri. Watu waliamin alitumia busara kutangaza kuwa uchaguzi wa NEC haukuwa na dosari ili kupata muda wa kutumia uungwana kuwa HAKI ITENDEKE kwa upande wa ZEC. Hakufanya hivyo na sura yake kamili imeonekana katika kauli ya pili.
Kauli kwamba Rais wa JMT (Magufuli) hana mamlaka ya kuingilia Tume ya ZEC wala NEC lakini akatuaminsha kwamba mazungumzo ya kupata suluhu ni muhimu hii ni aibu.
Azungumze nani tena ili suluhu ipatikane? na mazungumzo yaweje ili suluhu ipatikane? Maana kama ni mazungumzo tayari na imeshindikana. Ndio imeshindikana kwa sababu msingi wa Hoja uko kwenye KATIBA NA SHERIA na TAYARI WATAWALA HAWATAKI KUZIFUATA.
Wengine tulitamani akina Lubuva na JECHA watuwekee hadharani huo ukiukwaji uliofanywa huko pemba kiasi cha kuufuta uchaguzi wote hata sehemu ambazo hakukuwa na dosari mbona imeshindikana na hatimae wanalazimisha uchaguzi. Tazama AIBU hii eti leo tume ile ile ndio inaitisha uchaguzi? Badala ya watu akina Lubuva kuwasaidia watanzania, ndio kwanza wanazidi kuwapoteza, Ukweli usipindishwe. Tatizo ni WATAWALA kushindwa kule Zanzibar. Hii n i aibu..
Tume ya ZEC iko kwenye mgogoro, watu wamevurugana, ZEC imepoteza mwelekeo. Baada ya kuleta mawazo ya kuondoa matatizo haya ya ZEC kwa nchi ndio kwanza wanazidi kupewa jukumu la kuchafuwa zaidi.