Ahadi Za Wanachama Wa Chama Cha Mapinduzi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,045
Inasikitisha lakini CCM ndiyo ilivyo hivi sasa na hizi hapa chini ndiyo zingestahili kuwa ahadi za wanachama wa CCM kwa jinsi wanavyoiongoza nchi yetu


(1) Mafisadi wote ni ndugu zangu na Afrika si moja
(2) Nitawatumikia mafisadi wenzangu kwa nguvu zangu zote
(3) Nitajitolea nafsi yangu kuwalinda mafisadi.
(4) Rushwa si adui wa haki, nitapokea na kutoa rushwa ili nibaki madarakani.
(5) Cheo si dhamana, nitatumia cheo changu na vya mafisadi wenzangu kwa faida yangu.
(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya mafisadi.
(7) Nitashirikiana na mafisadi wenzangu wote kuibomoa nchi yetu.
(8) Sitasema kweli daima, fitina kwangu si mwiko.
(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa Chama Cha Mafisadi na fisadi mkubwa wa Tanzania na Afrika.
 
Back
Top Bottom