DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 161
- 200
Moja ya mbinu ambazo kwa muda mrefu wanasiasa wamekuwa wakizitumia kufanikisha malengo yao ya kisiasa ni kutoa ahadi za kimkakati zinazolenga makundi maalumu ndani ya jamii.
Siku chache baada ya kuapishwa, nimemsikia Waziri mpya wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, akitoa ahadi kwa wamiliki wa vyombo vya habari vya mtandaoni (Online Media) kwamba atatafuta kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa lengo la kuwawezesha. Binafsi, naona ahadi hii ina viashiria vya kuwa mtego.
Uzoefu wangu wa kuwa karibu na vyombo vya habari unaanzia kipindi ambacho Makonda alipotangazwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa. Katika kipindi hicho, alianzisha mtindo wa kukodi waandishi wa habari wa vyombo vya mtandaoni kutoka taasisi mbalimbali za habari, zikiwemo baadhi ya wanachama wa JUMIKITA.
Waandishi hao wamekuwa wakipewa posho pamoja na maelekezo ya masuala wanayotakiwa kuyaandika au kuyatolea taarifa wakati wa ziara zake. Kutokana na changamoto za kiuchumi zinazovikabili vyombo vingi vya habari vya mtandaoni, waandishi wengi wamejikuta wakitii maelekezo hayo.
Mtindo huu aliendeleza pia wakati alipokuwa Mkuu wa Mkoa, ambapo waandishi wa habari walikuwa wakisafiri kwa magari kutoka Dar es Salaam hadi Arusha wakifuatilia ziara zake. Hadi sasa, Makonda ana mtandao mpana wa vyombo vya habari ambao amekuwa akivitumia kueneza taarifa zake, hususan zile zenye mwelekeo wa kipropaganda. Mtandao huo huo ulitumika wakati wa mvutano wake na Gambo, kabla hata ya mchakato rasmi wa kampeni kuanza.
Kwa muktadha huo, ni halali kujiuliza: anaposema ataomba shilingi bilioni mbili kwa ajili ya Online Media, fedha hizo zitatumika kweli kuboresha mazingira ya kazi na uhuru wa vyombo hivyo, au ni malipo ya shukrani kwa kazi waliyoifanya awali? Zaidi ya hapo, je, vyombo hivyo hasa vile vinavyolengwa vitaendelea kuwa huru kutekeleza wajibu wao wa kihabari kwa maslahi ya umma?
Kwa mtazamo wangu, ahadi hii inaweza kuwa mtego kwa wamiliki wa vyombo vya habari vya mtandaoni, hususan vile ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa na misimamo huru katika kuripoti taarifa zenye maslahi mapana ya wananchi.