Ahadi ya ajira kwa vijana ni ahadi hewa?

kasabajr

Member
Feb 27, 2013
79
34
Asalaam Aleykum wanajamvi!

Ahadi za 2015 kuanzia kampeni hadi ushindi (japo ushindi huo kila kundi lililoshindana linamuono wake) moja ya ahadi iliyotawala ni ajira kwa vijana.

Kifupi katika idadi ya wa Tanzania iliyozaidi ya milioni45 vijana ndio wengi zaidi.Kwa muono wangu ajira kwa vijana bado ni bomu linaloweza kulipuka muda wowote.

- Vijana walio vyuoni/mashuleni(high school) wanazidi kuongezeka ikiwa nafasi za ajira bado ni zilezile.Serikali bado haijatengeneza ajira au uwezo wa kujiajili,ukiangalia mfumo wa elimu unaotolewa haumwandai kijana kujiajiri bali kuajiriwa.

Miaka ya 90 tulikuwa tunapata elimu ya kujiajili,nakumbuka jinsi nilivyolazimika kibeba jembe shule,kupanda kahawa,kuvuna mahindi shamba n.k kazi hizi zote nilizozifanya shule zilinisaidia kuona kawaida nilipotakiwa na mzazi wangu kuamka alfajiri kwenda shambani.

- Kwasasa vyuoni hata baadhi ya masomo hayana field study(I did International Relations 2011 in all three years there was no framed arrangement from my University for field study)nani ataajiri kijana asiye jua kazi kwa vitendo?
Je,mfumo huu wa elimu hauandai bomu?

- Waliomaliza chuo/high school/form four ni wachache sana walio ajiriwa au kujiajiri.Kwa idadi ya wahitimu 100 kwa kukadiri ni wasio zidi 20 ndio walioweza kujiajiri au kuajiriwa.Idadi ya waliobaki aidha wanafanya vibarua(temporary jobs)au wako mtaani wanazunguka.Je hawa 80 sio bomu?

- Walio na kazi za muda hunyanyasika kila kona!nimeamua kuwa mmachinga kariakoo ili niirishe familia yangu,nakimbizwa kila kona,nimeshuhudia rafiki zangu niliomaliza nao bachelor wakila mkong'oto,sasa ninampango wa kurudi kijijini,am turning old for me ain't gold! Sijui nitapata wapi shamba,sie tunalima mpunga kwetu kyela,sijui ntaazima ng'ombe kwa nani mimi!Kule Tunisia yule kijana aliyejilipua maeneo ya bunge,kwa hali hii walai am next!Hali hii sio bomu kweli?

-Tulipo ahidiwa viwanda,tukajua akiingia tuu,napata ajira kisha nitajiajiri haraka iwezekanavyo.Tunaelekea miezi kadhaa sioni njia,am turning to be a mopper! A worthless mopper on the land of of my father's,yes fore fathers.Vijana huku mtaani tunashindia maji,maji ya kandoro aah kumbe yupo mpya!Maji ya makonda!Hili sio bomu?

Wale tuliotegemea watatutetea sasa wamenyamaza,nilizungusha mikono baada ya kuona babu naye yupo upande ule!ila sasa mikono yangu nimeamua kuwa machinga,machinga asiye na mwelekeo!Fufuka Nyerere,fufuka babu yangu,njoo umsaidie baba yetu wa awamu ya tano!Anapambana,anapigana ila wajanja wanamzidi sasa wamefikia hata kumdanganya,hiyo ni jana tuu,tena uwanja wako wa Taifa hili,eeeh babu,nakumbuka hekaya za baba yangu alizonisimulia alipotoka shule ya sekondari Tosamaganga kwenda Mbeya-Kyela bure,bureee,sio kusoma tuu hata kusafirishwa.Nakumbuka nyimbo alizoimba

JKT mlale,Jua lile literemke mamaaa,
Aiyaaa iyaaa iyaaaa mamaaaa!

Tanzania Tanzania nchi yenye mali nyingi watu wengi wa Ulaya wanaililia sanaaa.

Solidality forever!

Aluta continua...mapambano yaendeleaaa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom