Ahadi za JK kwenye kampeni za kusakaurais 2010
============================
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria- Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi- Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba- Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu- Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba- Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika- Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote- Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa- Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga ¨CRukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani ¨CKihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)- Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa-Musoma
36. Kulinda haki za walemavu- Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma¨CMto wa Mbu Arusha-Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni- Kigoma¨C Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi- Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng¡¯ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha ¨C Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo- Busekera, Wilaya ya Musoma, .
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti ¨C Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
52. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
53. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania- Iringa
54. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
55. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
56. kuwapa wanawake nafasi zaidi- Kilolo ,Iringa
57. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
58. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa- Kabandamaiti mjini Zanzibar
59. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
60. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
61. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
62. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) ¨CRuvuma
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania ¨CRuvuma
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda ¨CMtwara
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa- Kibaha
66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha