Agizo la Usafi la Mh. Raisi ni mwiba kwa wasaka tonge...!!

barwani

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
238
160
Leo katika taarifa ya habari ya Itv,imemulika jinsi watu maeneo mbalimbali nchini walivyoonyesha muitikio HASI juu ya agizo la usafi la kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi alilotoa Mh. Raisi;Najua ndugu zangu wengi mtakua mkijiuliza sababu haswa ni nini hadi wananchi kuto_support agizo hilo,hz ni baadhi ya sababu;
1. Jumamosi ni siku ya ibada kwa baadhi ya madhehebu ya dini mf; wasabato
2. Jumamosi ni siku ya mapumziko kwa wafanyakazi wengi wa serikali mf; walimu
3. J'mosi ni siku ambayo wafanya kazi wengi wa serikali waliokua bze 5days wanasaka pato nje ya mishahara yao ya serikali ambayo ni midogo
4.J'mosi na hata kama sio J'mosi muda wa asbh ambao ndio kazi ya usafi inapaswa kuanza ndio muda mzuri wa kutengeneza pesa kwa waendesha bodaboda,bajaj,mabasi/daladala,mama lishe n.k(biashara asubuhi jioni mahesabu)
5. Zoezi limetawaliwa na vitisho,lugha chafu ambazo hutolewa na wasimamizi,makatibu tarafa na watendaji wengine
6. Ukosefu wa vitendea kazi mf;gloves,tolori na dustbin;kuna shusha morale ya kazi yenyewe;kazi/zoezi linaenda kiujanja ujanja na ni hatarishi kwa watekelezaji
7. Usafi wa siku moja ndani ya mwezi mzima ni sawa na kumpiga kwenzi kinyago;so wananchi wengi wanakosa Logic ya zoezi hili
8. Wengi wa wananchi wanaona km wameshikiliwa uhuru wao;unaweza kuhoji ni kwa siku moja tena ni kwa masaa ilaunapaswa kujua kua maisha ya watanzania wengi ni ya kuganga njaa,wengi hawaijui kesho yao
USHAURI;Serikali kupitia halmashauri za miji ziunde/zitoe tenda kwa makampuni ya usafi,pia mamlaka zinazohusika;mabwana afya wawe wakari na kuwachukulia sheria wale wote watakaoweka mazingira yao ktk hali ya uchafu;wananchi tuachwe na jmosi yetu,tufanye yetu..
 
Mie nashangaaa sana eti usubuhi subuhi unagonhewa hodi, ukiitikia unaambiwa mitaro michafu, sijui maana yake nini hii
 
Wengine siku ya jumamosi ni siku ya kufanya usafi kwa kufua nguo zote nk. Leo nimefanya usafi wa mazingira kwasababu nmeona mzee tunayeishi (mfanyakazi wa halmashauri) anajikanyaga na jembe huko nje; ndpo nikamhurumia na kufanya kwa ajili yake
 
Back
Top Bottom